Thursday, February 22, 2018

MWIJAGE MGENI RASMI KONGAMANO LA VIWANDA MNMA


Na Humphrey Shao, Globu Ya jamii
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage anataraji kufungua kongamano kuhusu Maendeleo ya Viwanda Tanzania   litakalo fanyika katika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  February 23 Mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo  Afisa Habari wa chuo Hicho 

Evelyn Mpasha amesema kuwa Kongamano hilo kubwa litawaleta karibu wadau mbalimbali wa masuala ya maendeleo ya Viwanda nchini.

“Kongamano hili litaangazia Masuala ya Maendeleo ya Uchumi , Uwekezaji Endelevu  katika Viwanda, Ujasiliamali katika Uwekezaji katika Viwanda kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya Umma na sekta binafsi” amesema Mpasha.

 Kwa upoande mmoja wa watoa mada katika kongamano hilo Binto Mawazo amesema kongamano hili ni sehemu ya juhudi za chuo kushiriki katika kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuipeleka Tanzania katika uchumi wa Viwanda .


Binto amesema kuwa MNMA kama chuo ni wadau Muhimu sana katika kukiwezesha wananchi kufika malengo ya Rais kuipeleka nchi katika  uchumi wa kati. 

WATAALAMU WA ICT WAKUTANA DAR ES SALAAM KUJADILI ULINZI WA SHERIA YA MITANDAO

 Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Cyber Tanzania, Samson Mwele akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwa ahilo kwa wataalamu wa Masuala ya ICT Tanzania juu ya kupambana na uhalifu wa mitandaoni.
 Mratibu wa Kongamano la Ulinzi wa Mtandaoni,Inocent Mungy, akizungumza wakati wa kongamano hilo lilipokuwa lianaendelea.
 Sehemu ya wataalamu wa Masuala ya ICT nchini wakifatilia kwa Makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na wadau wengine.
Sehemu ya Wadau wakiwa katika Mkutano ulinzi wa Sheria ya Mtandao nchini

Tuesday, February 20, 2018

THE LAUNCH PAD YATUMIA TASISI TATU KUWAELEZA VIJANA UMUHIMU WA NIDHAMU MAHAA PA KAZI

 Mkurugenzi na Mwanzilishi mwenza wa Tasisi ya Launch Pad Tanzania, Henry Kulaya, akizungumza na Vijana waliofika katika mafunzo ya siku mbili ya Ujasiliamali na Kuongeza Maharifa ya kuweza kuajirika katika tasisi mbalimbali nchini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Niajiri Platform, Lillian Madeje akizungumza na Vijana namna ya kuweza kuandaa Cv zao hili ziweze kuwasaidia kupata ajira kw aurais kupitia Mtnadao wake wa Niajiri Tanzania.
 Mkurugenzi ya Tasisi ya kuwezesha Vijana ya Empower Limited, Miranda Naiman akieleza namna tasisi yake ilivyojikita katika kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi katika kipindi hiki ambacho Dunia inapitia changamoto ya uhaba wa ajira.
  Mkurugenzi na Mwanzilishi mwenza wa Tasisi ya Launch Pad Tanzania,Carol Ndosi akichangia jambo katika mjadala wa kuongeza maharifa kwa vijana hili waweze kupata ajira kwa uraisi hili waweze kujikwamua kiuchumi
 Mmoja wa Vijana walioshiriki katika Kongamano hilo akieleza jambo juu ya umuhimu wa Vijana kuwa na Maadili kazini
 Sehemu ya Vijana waliokuwa katika makundi wakifanya kazi ya kujadili namna ya kuwa na maadili mahala pa kazi kunavyoweza kusaidia kukua kiuchumi na kupandishwa cheo.
Vijana walioshiriki kongamnao la Vijana Ujasiliamali na kuongeza maharifa hili waweze kuajirika katika mashirika mbalimbali lililoandaliwa na Tasisi ya The Launch Pad

Monday, February 19, 2018

Dk 30 ZA ASLAY ALIVYOWALIZA WATU ESCAPE ONE


Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii
Ilikuwa siku ya feb 17 ambapo Msanii wa Muziki wa BONGO Fleva Aslay Isihaka alivyoweza kubadilisha Histori aya kimziki katika Maisha yake kwa kuweza kufanya shoo kubwa ya Mapenzi na Muimbaji Mwenzie Nandy ambae ameshirikiana katika nyimbo nyingi.

Licha ya usiku huo kufikiriwa kuwa wa nyimbo za Mahaba mambo yalikwenda tofauti kwa nusu saa nzima pale Aslaya alipopanda jukwaani na kibao cha “Angekuwepo” wimbo ambao aliumba kwa ajili ya kumkumbuka Mama yake Mzazi.

Aslay ambaye aliimba kisha kuishia kati na kwenda kumsogelea Mama Mzazi wa Nandy na kusema kuwa “natamani muda huu Mama yangu muda huu angekuwa hapa lakini sio mapenzi yangu natamani namimi ningekuwa kama Nandy naimba Mama yangu anaona hivyo nikuombe Mama Nandy kuanzia leo uwe mama hili niweze kupata faraja kama anayopata mwanao” alisema Aslay .

Maneno hayo ambayo yaliteka hisia za watu wengi na kumfanya Mama yake Nandy kuamka na kwenda Mbela kucheza na Aslay kisha watu wengi kuinuka kwenda kumwambia mwanamuziki huyo aendelee kuimba na kuacha kulia.

Aslay ambaye aliendelea kuimba wimbo huo huku akiwa amekaa chini na uzuni mkubwa na kutengeneza Simanzi kubwa ndani ya ukumbi wa Escape One kwa zaidi ya Dk 30 Jambo ambalo liliwafikirisha watu na kusema kuwa Mama ni wa muhimu kuliko kitu chochote
 Mwanamuziki wa Muziki wa kizazi Kipya Aslay Isihaka akionyesha kidole juu kumshukuru Mungu kwa yote yaliyotekea katika maisha yake.
 Aslay akimuomba   Mama yake Nandy  kuwa Mama yake wa kumlea wakati anaimba wimbo wake angekuwepo
 Aslay akicheza na Mama yake Nandy  mara baada ya kukubali kuwa Mama Mlezi
 Mmoja wa Mashabiki wakinyamazisha Aslay asilie wakati anaimba wimbo angekuwepo
Mashabiki wa muziki wakiwa wamesimama kwa Huzuni mara baada ya Aslay kuimba wimbo huo

CHEMBA WAKOSA HUDUMA ZA AFYA KWA MIAKA MINNE


WANANCHI wa Kijiji cha Magasa, Kata ya Mrijo wilayani Chemba, wamekosa huduma za afya kwa muda mrefu, licha ya jengo la zahanati yao kukamilika kwa zaidi ya miaka minne sasa.
Wakizungumza na Ripota wa Jijiletu  mwishoni mwa wiki, wananchi hao walisema wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita saba hadi vijiji vya Soya na Mrijo kufuata huduma za afya, jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwao.
Jengo hilo ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi na baadae Serikali kumalizia, linadaiwa kukaa kama pambo kijijini hapo bila huduma zozote, licha ya ujenzi wake kukamilika tangu 2014.
“Jengo letu tangu limekamilika linazaidi ya miaka minne, pia tumeletewa daktari hapa alikuja kuripoti, tuliambiwa baada ya mwezi mmoja atakuja kuanza kazi, tumesubiria hadi leo hatujamwona,” alisema Ramadhan Rajabu.
Mwananchi mwingine Hamisi Kijaji alisema kinachowaumiza zaidi ni pale wajawazito wanavyopata shida, kwani wanatumia usafiri wa baiskeli na mikokoteni na wakati mwingine wanapoteza maisha njiani kutokana na ubovu wa barabara.
Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Mussa Ninga, alikiri kukosekana kwa huduma hiyo na kueleza watumishi wawili wameripoti kijijini hapo, lakini waliondoka katika mazingira ya kutatanisha.
Ninga alimtaja daktari mmoja kwamba aliripoti kijijini hapo Novemba 28, mwaka jana akitokea Kituo cha Afya Makorongo, lakini aliondoka bila taarifa ambapo hadi sasa haijulikani alipo.
“Awali tuliletewa mtumishi anaitwa Prisca alikuja 28/10/2016 na saini yake ipo ofisini kwenye kitabu alipokuja kuripoti, baadae tuliambiwa ameondolewa kwa sababu ya vyeti feki,” alisema.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Idd Baba, alisema zahanati hiyo imegeuka mzigo kwake, kwani amefanya jitihada kufuatilia ngazi za juu lakini hajapata majibu ya kuridhisha.
“Kila siku mara leo mara kesho, naletewa daktari mara tunaambiwa ni feki, naanza tena kufuatilia nikaletewa mwingine mara nikasikia naye amehamishwa,” alisema.
Diwani wa Kata ya Mrijo, Hamisi Msakati (CCM), alikiri wananchi hao kupata shida licha ya jengo kukamilika muda mrefu na kueleza kuwa alipofuatilia wilayani kuhusu watumishi aliambiwa zahanati hiyo haijasajiliwa.
“Mwaka jana walileta doctor mwingine alikuja akaripoti nikapata na barua, lakini mazingira aliyoondokea ni ya kutatanisha. Nilipofuatilia wilayani Mganga Mkuu wa Wilaya akaniambia hii zahanati haijasajiliwa.
“Nilimwambia kuna watumishi wawili mmewaleta kule, wakati mnafanya hayo hili la usajili mlikuwa hamlijui? Kwa kweli sikupata majibu ya kuridhisha, hayatoshelezi hata kwa akili za kawaida,” alisema.
Mwandishi alilazimika kumtafuta Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Dk. Semistatus Mashimba,  ambaye alishangazwa na taarifa hizo na kuahidi kuchukua hatua mara moja ili wananchi hao wapate huduma.
“Hili ndiyo nalisikia kutoka kwako, kwanza nikushukuru kwa kunipa taarifa hili nalifuatilia kuanzia sasa, yaani hata diwani ameshindwa kufika ofisini kwangu hata simu ameshindwa kunipigia tukalimaliza?
“Miaka minne watu hawapati huduma na jengo limekamilika kama ni usajili taratibu zake zipo wazi kinachokwamisha ni nini? Uzembe huu hauwezi kuvumiliwa,” alisema Dk. Mashimba.

THE LAUNCH PAD YAWANOA VIJANA MABALIMBALI JUU YA MAHARIFA YA KAZI NA UJASILIAMALI

 Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw Makbel akizungumza juu ya mpango wa uanagenzi ulivyoweza kuwasaidia Vijana wengi kuingia katika sekta rasmi na kuweza kushindana na wasomi wengine ambao walipata ujuzi katika mfumo wa kawaida.
 Mwakilishi wa Tasisi ya Vijana Think Tank akizungumza namna Vijana wanavyotakiwa kufikiri zaidi hili waweze kujikwamua katika wimbi la kukosa ajira kwa kusema kuwa kila mwaka kundi la Vijana wasiokuwa na ajira wanavyoongezeka
 Mtaalamu wa Masula ya ushauri wa kujikwamua na ajira kutoka Shirika la kazi Duniani ILO, Comoro Mwenda akitoa somo ya namna vijana nini waweze kufanya hili kufikia malengo yao ya kuajiriwa au kujiajiri popote pale duniani
 Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Launch Pad Tanzania, Caroline Ndosi akizungumza wakati wa akiongoza Meza ya mjadal awakati wa kongamano la kuwajengea Vijana uwezo wa ujasiliamali na kuweza kuajirika katika Tasisi mbalimbali.
Sehemu ya Vijana kutoka sehemu mbalimbali ya Tanzania walioshiriki Kongamano la Kuongeza Maharifa ya ujasiliamali na kuajirika lililoandaliwa na Tasisi isiyo ya Kiserikali ya The Launch Pad

MAMA SALMA KIKWETE MAMLAKA KUTOA HAKI KWA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete amezitaka mamlaka zinazojihusisha na utoaji haki, kuwasaidia wanawake kupata haki zao pindi wanapofungua mashauri ya kudai matunzo ya watoto.
Mama Salama amesema ahayo juzi Jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la wanawake wanaolea watoto peke yao Single Mothers lililoandaliwa na kituo cha Radio cha Efm na Tv E.

amesema kuwea ni vyema wanaume kutambua majukumu yao ya kulea watoto kwani ni matakwa ya sheria watoto kulelewa na wazazi wote na sio kuwatelekeza  na kusema  watoto wanatakiwa kupata malezi mema  na ya upendo.

"Wanawake wanatekesa wanapotafuta haki zao  kutokana na unyonge na umasikini waliokuwa nao hivyo haki itendeke ili wanawake watembee kwa kujiamini katika nchi yao," amesema Mama Salma.
Aliongeza kuwa watoto wana haki ya kupata malezi mema kutoka kwa wazazi wote, elimu na afya ili kukua vizuri kiakili na kijamii.

"Ukiona wanawake wanatupa watoto jiulize kuna nini, bila tatizo hawawezi kutupa mtoto kwani anauma sana na ndio maana wengine wanapojifungua wanawaviringisha na kuwaweka mahali pazuri  akijua kwamba lazima watu watapita na kumuokota na kwamba atalelewa vizuri," alieleza.
Alisisitiza kuwa wanaume wanapaswa kutambua mazingira ya wake zao pindi wanapokuwa wajawazito na wawatunze, kuwathamini na kuwajali watoto.

Mama Salma alisema wasiwaachie malezi wanawake pekee kwani hakuna mtoto asiye na baba.
Pia alisema kuwa kampeni hiyo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi inayofanywa na Kituo cha Redio Efm na TV E inapaswa kuungwa mkono kwani ndio muelekeo wa Siku ya Wanawake duniani inayoadhimishwa kila mwaka Machi 8.

Naye, Mhariri wa kituo hicho cha redio, Scholastica Mazura alisema ni wakati wa kutoa elimu kwa vijana wanaoingia kwenye ndoa ili kupunguza idadi ya watoto wanaolelewa na mzazi mmoja. 
Alisema wanawake wengi wanaishi nje ya ndoa zao  kwa sababu mbalimbali na hivyo tatizo la malezi ya upande mmoja kuwa kubwa nchini.

Alieleza kuwa wanawake wamekata tamaa kwani wapo ambao wametelekezwa nao wanatelekeza watoto lakini wengine wanawalea kwa shida ili wapate malezi bora.
"Tuwacheke wanaume wanaokimbia majukumu yao na kuwaachia wanawake pekee kwa kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa kwani mnauwezo mkubwa wa kulea nasi tutawasaidia ili mjikwamue kiuchumi," alisema Mazura.

 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa Kongamano la Single Mothers lililoandaliwa na Efm na Tv E 
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete Akicheza na Wanawake waliojumuika katika Tamasha la Sinle Mothers lililoandaliwa na Efm Radio kwa kushirikia na Tv E
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono wanawake walioshiriki Tamasha la Sinle mothers wakati anaingia ukumbini
 Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige akizungumza na kuwatia moyo wanawake hao na kusema pia hata yeye ni Single Mothers na bado maisha yanenda
 Mhariri wa kituo hicho cha redio Efm na Tv E, Scholastica Mazura akizungumza  na vijana wanaoingia kwenye ndoa ili kupunguza idadi ya watoto wanaolelewa na mzazi mmoja. 
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akipoke Zawadi kutoka kwa Meneja Tukio wa Efm na Tv E , Jesca Mwanyika.
 Mbunge wa Viti Maalum Rita Kabati akizungumza na wnawake wanaolea Watoto peke yao juu ya umuhimu wa kumtegeea Mungu hili kufanikiwa
 Waziri Mstaafu na Mbunge , Hawa Ghasia akieleza ugumu wa kulea mtoto peke yako na kuwatia moyo wanawake wote waliotelekezwa
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Efm Radio na Tv E ambao ni Single Mothers 

MWIJAGE MGENI RASMI KONGAMANO LA VIWANDA MNMA

Na Humphrey Shao, Globu Ya jamii Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage anataraji kufungua kongamano kuhusu Maende...