Sunday, August 10, 2014

DIMOND AFUNIKA SERENGETI FIESTA MWANZA
SERENGETI FIESTA YA BAMBA JIJINI MWANZA
TAMASHA la muziki la Sertengeti fiesta linalodhaminiwa na kinywaji mashuhuri cha Premium Serengeti limeanza kwa kishindo mwishoni mwa wiki ambapo zaidi ya wakazi 30,000 walihudhuria na kusababisha msisimko mkubwa kwa wasanii waliotumbuiza tamasha hilo kwenye Uwanja wa CCM kirumba Jijini Mwanza.
Tamasha la Mwanza, ambalo lilikuwa la aina yake, lililojaa shangwe na msisimko mkubwa, lilitumbuizwa na wasanii kama Diamond Platinum, Linah, Shilole, Ally Kiba, Mr. Blue, Young Killer, Ney wa Mitego, Madee, na wengine wengi.
Onyesho la mwaka huu limevuta hisia za wengi hasa wataalam wa burudani walioipongeza kampuni ya Serengeti Breweries kwa kuwa mfano mzuri wa burudani bora.
Kampuni ya Serengeti imewahakikishia watanzania kwamba kwa kipindi chote cha kiezi mitatu ya Serengeti fiesta watatoa burudani ya pekee na isiyo na kifani.
Abaadhi ya mikoa ambako Serengeti itapita ni pamoja na  Kahama, Bukoba, Musoma, Shinyanga, Kigoma,  Tabora, Singida, Dodoma, Tanga, Moshi, Arusha, Mtwara and Dar es salaam na hatimaye Jijini Dar es Salaam Oktoba 18 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo, meneja wa bia ya Serengeti, Rodney Rugambo alisema kwamba uongozi wa kampuni ya Serengeti kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, kutokana na uzoefu kutoka kenywe matamasha mbalimbali ya fiesta kwa miaka iliyopita, tamasha la mwaka huu limekuja na muonekano mpya, vionjo vipya na burudani kabambe.
“kwa mwaka huu, watanzania wajiandae kupata burudani ya kukata na shoka kutoka kwa wasanii maarufu, mashuhuri na wenye vipaji. Fiesta si kunya peke yake, pia kushuhudia vipaji mbalimbali vya mziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wenye vionjo tofauti,” alisema Rugambo.
Amesema ia kwamba kwa kipindi hicho cha miezi mitatu, burudani la fiesta litaambatana na mashindano ya mpira wa miguu yanayojulikana kama Serenegti Soccer Bonanza.
Pia kutauwa na mashindano ya kucheza muziki… Serengeti Dance la Fiesta na vilevile mashindano ya kuimba yatakayo jikita zaidi kwa wasichana – Serengeti Supa Nyota Divas – ambapo mshindi katika kila mkoa atakwenda kushindana na mshiriki kutoka  Jijini Dar es Salaam.No comments:

Post a Comment

Waziri Dk Kigwangalla ataka wavamizi maeneo yaliyohifadhiwa kuondoka

Mwandishi wetu,Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewataka wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi nchini,...