Tuesday, September 23, 2014

CHAKUPAU YAWAFIKIA WADAU WA USTAWI WA MTOTO KIGAMBONI

CHAMA CHA KUPAMBANA NA ATHARI ZA UKIMWI (CHAKUPAU)

1.0        UTANGULIZI
CHAKUPAU kwa ushirikiano na The Foubdation For Civil society inatekeleza mradi wa stadi za malezi na haki za watoto WKMH,taarifa hii inakusudia mutoa picha halisi ya mwenendo wa shughuli ya mafunzo ya malezi na haki za watoto walio katika mazingira hatarishi kama shughuli ya utangulizi katika mradi huu.

Katika taarifa hii kuna maelezo ya mchakato wa mafunzo kwa ujumla yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu,ikiwemo ufunguzi wa mafunzo,viongozi wa darasa,kanuni za mafunzo,Mada zilizofundishwa.kazi za vikundi,visa mkasa pamoja na tathmini ya mafunzo.

Washiriki wa mafunzo haya walizingatia kada mbalimbali katika jamii zinazoguswa ustawi wa mtoto kwa uwakilishi ngazi ya kata kama ifuatavyo:-wazazi/walezi,watu mashuhuri,Viongozi wa dini,Polisi kata,afisa maendeleo jamii,Mratibu wa elimu,watendaji wa mitaa,wenyeviti wa mitaa,katibu baraza la kata na watoto wenyewe WKMH.Jumla ya walengwa walikuwa 32,me 22 na ke 10.

2.0. MCHAKATO WA MAFUNZO

2.1. UFUNGUZI WA MAFUNZO
Mafunzo yalifunguliwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Kimbiji Ndg Joakim D. Mwando  ambaye aliwataka washiriki kuwa makini na wasikivu,ili waweze kuyafanyia kazi mafunzo yatakayofundishwa na wawezeshaji.
Aliishukuru taasisi ya Chakupau juu ya kuona umuhimu wa kuiwezesha jamii  Stadi za malezi na Haki za Watoto walio katika mazingira Hatarishi, ili ione ni na mna gani itaweza kusaidia watoto hao.

2.2. VIONGOZI WA DARASA
Kabla ya kuanza kwa mafunzo,washiriki walipata fursa ya kuchagua viongozi wao wa darasa,ambao ni:
1. Ndg         SILVERY KALIKISHA                Mwenyekiti  
2. Ndg         REHEMA MANYANDA          Katibu
3. Ndg          SAIDI MMADI                        Mtunza muda

2.3. KANUNI ZA DARASA
Washiriki walihainisha kanuni za darasa ili kuliweka darasa katika mwenendo wa utaratibu,kanuni zilizowekwa ni:
1. Simu zote ziwekwe kwenye mtetemo.
2. Kuheshimu mawazo ya kila mtu/mawazo ya mtu yaheshimiwe.
3. Kusiwe na darasa ndani ya darasa.
4. Unaposhirikishwa ushiriki

2.4 Mbinu zilizotumika
Ili kuwezesha washiriki kuelewa kwa kufuata umri,wadhifa na hali zao mbinu mbalimbali zilitumika kama ifutatavyo:-
·        Muhadhara
·        Maswali na majibu
·        Visa mkasa
·        Majadiliano ya vikundi pamoja na
·        Bungua bongo

2.5. MADA ZILIZOFUNDISHWA
Mada zilizofundishwa katika mafunzo ni:
1. Haki za Watoto
2. Stadi za malezi
Mwezeshaji mafunzo ya stadi za malezi na haki za watoto Kutoka halmashauri ya  Manispaa ya Temeke bwana Halphan Sabuni, akitoa mada ya stadi za malezi kwa washiriki wa mafunzo ya kata ya Kimbiji katika ukumbi wa afisa mtendaji kata ya kimbiji.Mafunzo haya yamefadhiliwa na The Foubdation For Civil Society  LTD.

2.5.1. MADA YA KWANZA HAKI ZA WATOTO

Lengo;- Kuwawezesha wazazi, walezi, familia, jamii na wadau mbalimbali kujitoa kwa dhati katika kusaidia WWKMH ili waweze kuishi kama watoto wengine.

Shabaha hasa ya somo hili ni kuwawezesha walengwa kujua:-
a.          Tafsiri sahihi ya malezi.
b.          Mambo muhimu katika malezi.
c.          Mambo yanayochochea malezi na makuzi ya mtoto.
d.          Majukumu ya wadau mbalimbali katika malezi ya mtoto.
e.          Changamoto mbalimbali na namna ya kukabiliana nazo.

Ili kupata uelewa wa pamoja katika maana ya masuala yanayohusinana na stadi za malezi maswali ya bungua bongo yalitumika ili kupima uelewa wa walengwa.Maswali yalikuwa kama ifutatavyo:

SWALI : HAKI NI NINI?
Majibu ya Washiriki

-          Ni kumpa mtoto, haki zake za msingi.
-          Ni kumuwezesha mtoto kupata mahitaji muhimu.
-          Ni kumpa mahitaji yanayostahili kwa mtoto.
-          Kucheza michezo mbalimbali.
-          Kusikilizwa.


Tafsiri ya Haki kutoka kwa mwezeshaji

-        Haki ni mambo ya msingi ambayo mtu anapaswa kuyapata pasipo masharti yoyote kutoka kwa mtu mwingine.

WAJIBU NI NINI?
-        Wajibu ni mambo ya msingi unayotakiwa kutenda ili haki itimizwe.Haki za mtoto ni zipi?

Katika mkataba wa kimataifa wa haki a watoto ambao ulipitishwa na jumuiya ya kimataifa mwa ka 1989, umelipa kipaumbele haki za mtoto mkataba huu umepitishwa na baraza kuu la umoja wa mataifa na kisheria ulianza kutumika 1990.  Tanzania iliridhia mkataba huu mnamo mwaka 1991.
Kulingana na mkataba huu, umegawa haki za watoto katika makundi makuu manne (4) nayo ni:-
           i.       Haki ya kuendelea kuishi.
          ii.       Haki ya kuendelea kukua.
          iii.      Haki ya kulindwa.
          iv.      Haki ya kushiriki katika maswala ya jamii.

1.       HAKI YA KUENDELEA KUISHI
-        Haki hii inahusu mahitaji ya msingi ikiwepo, chakula bora, mahali pazuri pa kulala mavazi na kupatiwa huduma za afya.

2.       HAKI YA KUENDELEA KUKUA
-        Haki hii inahusu mambo yote wanayohitaji watoto yatakayo wasaidia kuendelea kukua, kimwili, kiakili na kiuadilifu.
3.        HAKI YA KULINDWA
Haki hii inahusu kumlinda mtoto dhidi ya mambo mengi ikiwemo ukatili,  ubakaji, mateso au kufanyishwa kazi ya malipo.

4.        HAKI YA KUSHIRIKI KATIKA MASUALA YA KIJAMII
Haki hii inamama ya kuwa nna uhuru wa kutoa maoni ya kushiriki katika maamuzi ya kijamii
Wanajamii wa kimbiji walilalamika kuwa pamoja na kwamba mtoto ana haki ya kuishi na kuwa serikali imeondoa gharama za afya kwa watoto walio chini ya miaka 5 lakini bado Zahanati ya Kimbiji inatoza gharama kwa watoto walio chini ya miaka 5.Washiriki walikubaliana kwa pamoja kulifuatilia suala hili na kuchkua hatua.
 


MADA NO. 2  STADI ZA MALEZI KWA WWKMH
LENGO:-     Kuwawezesha wazazi, walezi, jamii na wadau mbalimbali kujitoa kwa dhati katika kusaidia WWKMH ili waweze kuishi kama watoto wengine.

 Baada ya mafunzo tutapata uelewa wa:-
-          Maana sahihi ya stadi za malezi
-          Hatua za ukuaji
-          Mambo muhimu katika malezi na makuzi ya mtoto
-          Nafasi ya wakala wa malezi ya mtoto na changamoto zake
-          Majadiiliano

Maana ya stadi za malezi:-
-        Ni mbinu/vitendo vinavyowezesha jamii kumlea, kumtunza, kumsadia, na kumwendeleza mtoto kwa kufuata uelekea unaofaa kwa ustawi wake.

Stadi:-
-          Ni usimammiajii wa jambo katika ukamilifu
-          Uboreshaji
-          Ujuzi/Elimu inayotolewa kwa uwezeshaji wa maisha na malezi ya mtoto

Malezi
-          Kuweka mambo yawe sawa
-          Utoaji wa huduma/mahitaji ya mtoto
-          Kuwezesha watoto waweze kuajua mila + Desturi.

Maana ya stadi za malezi
-        Ni matendo yote anayofanya na mzazi, mlezi, jamii na wadau mbalimbali kwa LENGO la.
Ø  Kumlea
Ø  Kumtunza       
Ø  Kumlinda na
Ø  Kumwendeleza mtoto 
§  Kimwili
§  Kiakili
§  Kihisia
§  Kimaadili
§  Kijamii ili
Aweze kuishi, kukua kuendelea vizuri na kukubalika na jami

HATUA ZA UKUAJI:-
H/Maendeleo ya mtoto         0 - 8
1.        Ukuaji wa mtoto kimwili
2.        Ukuaji wa mtoto kiakili
3.        Ukuaji wa mtoto kihisia
4.        Ukuaji wa mtoto kimaadili
5.        Ukuaji wa mtoto kijamii

Mambo muhimu katika malezi na makuzi ya mtoto
1.        Lishe
2.        Afya
3.        Uangalizi
4.        Uchangamshi


KAZI ZA VIKUNDI
1.        Mambo yanayochochea malezi na makuzi ya mtoto
           -       Hali ya kiuchumi
           -       Mahusiano katika jamii
           -       Utamaduni

2.        Eleza nafasi ya wakala wa malezi ya mtoto na changamoto zake
           -       Familia
           -       Makundi Rika
           -       Taasisi za Elimu
           -       Imani za kiroho (dini)
           -       Vyombo vya Habari

KUNDI  No: 1
SWALI
KAZI
JIBU
- Hali ya kiuchumi
- Kilimo
- Biashara
- Lishe kwa ajiri ya mtoto
- Uwezo wa kumpa elimu
- ukuaji wa mtoto

Mahusiano katika jamii
- Tabia
- Wazazi

- Utamaduni

- Makabila mbalimba 
  utandawazi
- Mila potofu
- Rika tofauti
- Jamii inayomzunguka 
   ikuwa na tabia mbovu
   husababisha
   kumpotosha mtoto.


Pichani juu;-Washirki wa mafunzo ya stadi za malezi na haki za waotot wa kata ya kimbiji wakiwa katika majadiliano ya makundi kabla ya kuwasilisha .
Pichani  kulia:-Ndg Mbaraka Abdallah akifanya uwasilishaji wa kundi lake.
Pichani kushoto:-Ndg  Nicki M. Tajili akifanya uwasilishaji wa kundi lake
 
KUNDI No. 2:
NAFASI YA WAKALA WA MALEZI YA WATOTO NA CHANGAMOTO ZAKE:-
1.       Familia:
-        Familia ina wajibika kumpatia mtoto huduma muhimu kama chakula, makazi, Elimu mavazi n.k.
          
Changamoto:
-        Hali ngumu ya maisha kiuchumi kwa baadhi ya familia.

2.       Makundi rika:
-        Yanamfanya mtoto kuchangamka na wenzake, kujumuika katika maongezi michazo n.k.

Changamoto:
-        Baadhi ya makundi rika yanakuona tabia ambazo wakati mwingine sio nzuri. Mfano:-Ngono, Kamati, ulevi n.k.

3.        Taasisi za Elimu:-         
-        Kutoa stadi na maalifa ambazo zitakuwezesha mtoto kukabiliana na changamoto za maisha.

Changamoto:
-        Hali ngumu ya kiuchumi.

4.        Imani za kiroho (dini):-
-        Inasaidia kuwajenga watoto kuwa na tabia nzuri kwa jamii na mwenendo mzuri kwa jamii.

Changamoto:
-        Mtoto ambae hakupata maadili ya kiroho ana kuwa na taabia ambazo sio nzuri hazipendezi kwa jamii.

5.        Vyombo vya habari:-
           -       Vinasaidia kuelimisha na kupata taarifa kwa haraka \


Changamoto:
-        Habari nyingine zinakuwa ni za kupotosha jamii Mfano:- badhi ya mitandao mbalimbali.

3.0 TATHIMINI
1.          Je, mada za leo zimeeleweka kama ndiyo
-           Kipi umeelewa kama hapana, kwanini? kipi unahitaji kiwekewe mkazo zaidi katika eneo letu Kimbiji.

2.         Je, uwezeshaji umekwenda vizuri?
-           Kama ndiyo eleza kwa ufupi kilichukugusa/furahisha/pendeza.
-           Kama hapana eleza kwa ufupi unadhani kwa nini?

3.         Toa maoni yako kwa ufupi, nini kifanyike kusaidia WWKWMH, kwa wadau hawa:-
            1.         Wazazi
            2.         Jamii
            3.         Wadau mbalimbali
            4.         Serikali

3.1 MATOKEO YA TATHMINI

ENEO LA TATHMINI
MATOKEO YA TAHMINI
HATUA YA KUCHUKULIWA
Uelewa walengwa kuhusu mada zilizofundihswa
90% ya washiriki wa mafunzo walisema kuwa wameelewa mafunzo katika mada zote.
Kwa kuwa asilimia kubwa ya washiriki walionesha kuelewa mbinu zilizotumika zitatumiwa zaidi ili kuboresha mafunzo.
Mada iliyoeleweka zaidi
Asilimia 60 ya walengwa walisema wameelewa zaidi mada ya haki za watoto na asilimia 40 stadi za malezi
Kwa kuwa stadi za malezi ni somo pana tutajaribu kulitilia mkazo zaidi kwenye shughuli zinazofuata.
Mada ambayo hazijaeleweka
Hakuna mada ambayo haijaeleweka
Kwa kuwa asilimia kubwa ya washiriki walionesha kuelewa mbinu zilizotumika zitatumiwa zaidi ili kuboresha mafunzo.
Uwezo wa wawezeshaji
Washiriki walionyesha kulidhishwa na wawezeshaji hasa kwa kuwa walizingatia jinsi.

Maoni kuhusu nini kifanyike kwa hatua za baadae
-Serikali isimamie sheria za kulinda ustawi wa mtoto.

-Jamii ishiriane katika malezi ya watoto kwa kuwa watoto ni mali ya jamii.

-Jamii isifumbie macho masuala ya ukiukwaji wa haki za watoto.

-Mafunzo yanatakiwa kwenda hadi ngazi ya chini ya familia.

-Elimu itolewe katika mikutano ya mtaa.

-Haki ya mtoto iwe ni somo mashuleni

Kutakuwa na shughuli ya uundaji wa vikosi kazi vya jamii.Moja ya kazi za vikosi kazi hivi itakuwa ni kuweka katika vitendo makubaliano na masuala yatakayowekwa katika mpango kazi wa kata.

CHAKUPAU itaratibu na kusimamia shughuli za vikosi kazi vya kata ili kuhakikisha mpango kazi unatekelezwa kwa vitendo.

Kutakuwa na kikao cha watunga sera moja ya masuala yatakayozungumziwa ni kuweka vipaombele vya masuala ya haki za watoto katika mipango ya Halmashauri.


4.0 Hitimisho
          Shughuli hii ya mafunzo ni moja ya shughuli kumi  za mradi wa stadi za malezi na haki za watoto walio katika mazingira hatarishi .Baada ya mafunzo haya tunategemea kuwa CHAKUPAU kwa kushirikiana na wadau katika kata hii ya kimbiji wanatekeleza shughuli zinazofuatia ili kuleta mabadiliko katika kata hii ya kimbiji na kuleta mwanzo wa sura ya mabadiliko katika kata nyingine za Manispaa ya Temeke na Tanzania kwa ujumla.
          Mwisho wa shughuli hii ya mafunzo ndiyo mwanzo wa shughuli nyingine zinazofuatia ni mategemeo yetu kuwa walengwa na wanufaika wa mradi huu watatoa ushirikiano kama ilivyokuwa kabla ya mafunzo haya ili kurahisisha shughuli zinazofuata.

No comments:

Post a Comment

MWENGE WA UHURU WAINGIA GAIRO NA KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA MILIONI MIASABA NA ZAIDI

 Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Morogoro Regina Chonjo mara ulipofika katika eneo la Ma...