Wednesday, September 24, 2014

Diamond kuuza nyimbo mtandaoni

 

NA HUMPHREY SHAO, DAR ES SALAAM
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, jana aliingia makubaliano na mtandao wa Muziki Family, ambao utakuwa ukitangaza nyimbo zake kwa njia ya mtandao.
Akizungumza jijini jana, Mkurugenzi mtendani wa kampuni ya Spice Vas Afrika, ambao ndiyo wamiliki wa mtandao huo, Arun Nagar, alisema makubaliano hayo yatamuongezea mashabiki wengi msanii huyo.
 
kwanza Tanzania kuingia mkataba na Alisema kuwa Diamond ni msanii wa kampuni hiyo ambayo ina jumla ya wasanii 100 wa kimataifa.
“Tutashirikiana kwa kila kitu kuhakikisha muziki wa Diamond unafanya vizuri Afrika, huku mashabiki wakiongezeka upande wake na wetu pia,” alisema Nagar.

Wakati huo huo, Diamond alisema kuwa anashukuru kuingia makubaliano hayo yatawawezesha mashabiki zake kusikiliza nyimbo zake kupitia mtandaoni Afrika.

No comments:

Post a Comment

TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE JUU YA MFUMO WA UNUNUZI WA LUKU

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa Umeme kwa ...