Tanzania
Albino Unity ni kikundi cha walemavu wa Ngozi (Albino) kilichoanzishwa mwaka
2013 chenye lengo na madhumuni ya kupunguza makali ya maisha na mazingira
magumu ambayo watu wenye ulemavu wanakumbana nayo.Taasisi hii
iliyoanzishwa.inayoongozwa na inayosimaiwa na watu wenye ulemavu imesajii brela
chini ya majina ya kampuni.kwa usajili namba 275829 Kwa sasa Asasi imeamua
kujikita katika eneo la ufugaji wa kuku wa nyama kama njia ya kuongeza ajira
binafsi kwa watu wenye ulemavu ikianzia Manispaa ya Temeke na tunategemea
kutafuta ufumuzi wa changamoto za ajira kwa albino katika wilaya na mikoa
mingine ya Tanzania.
Tanzania
Albino Unity kwa uwezeshaji kutoka, Tume ya uwezeshaji imepata nafasi ya
kuwakilisha Maalbino 6 kushiriki mafunzo ya siku 14 ya ufugaji wa kuku wa nyama
katika chuo cha wakala wa vyuo vya mifugo kilichopo Vetenari, Temeke,
Dar-es-salaam.Malengo ya mafunzo mafunzo haya ni kuwezesha maalbino kuwa na
uelewa na mbinu za kufanya ufugaji bora na wa kisasa wa kuku wa nyama ili
waweze kuendesha mradi wa ufugaji na kukuza kipato chao.
Taarifa hii inatoa
kwa muhutasari mchakato wa mafunzo haya toka siku ya kwanza mpaka siku ya
mwisho wa mafunzo.
1.0 MCHAKATO WA MAFUNZO
Mafunzo ya
ufugaji wa kuku yalichukua muda wa siku 14 yakihusisha mafunzo ya darasani na
mafunzo kwa vitendo ili kuwezesha walengwa kuelewa kwa undani hatua mbalimbali
za ufugaji wa kuku.
2.1 MUDA WA MFUNZO NA IDADI YA WALENGWA
Muda wa
mafunzo ulikuwa ni siku 14 na idadi ya walengwa ilikuwa ni Maalbino 6
2.2
MAFUNZO TULIYOJIFUNZA
Katika muda wa
siku 14 tuliweza kupitia maeneo mbalimbali muhimu katika ufugaji wa kuku ambazo
tunazieleza kwa muhutasari hapo chini kutokana na utaratibu na ratiba
iliyopangwa na wakufunzi:-
2.2.1 Utunzaji bora wa kuku
Hapa
tulifunza dhana nzima ya utunzaji wa kuku yakuwa kuku ni kama ndege ambaye
anafugwa nyumbani ambao wanagawanywa katika makundi makuu 2.Ambao ni kuku wa
kienyeji na kuku wa kisasa.Na kuwa kuku wa kisasa pia wamegawanyika katika
sehemu 2 ambazo ni kuku wa nyama na kuku wa mayai.Kuku hawa wa kisasa
wanatakiwa kufugwa kwa taratibu za kitaalam ikiwa ni pamoja na ujenzi wa banda
linalokidhi mahitaji ya kuku hao.
2.2.2 Magonjwa ya kuku
Pamoja na
utunzaji bora wa kuku tulijifunza magonjwa yayodhoofisha ukuaji wa kuku pamoja
na kusababisha vifo kwa kuku kuwa ni:-
-Mdondo/kideri unaonekana katika mifumo
ya hewafahamu, chakula na mfumo wa uzazi ugonjwa huu unaweza kuua kuku kwa 80%
mpaka 100% katika banda.
-Respiratory disease complex –Ugonjwa
huu wa mfumo wa hewa unaweza kuua kuku katika banda kwa 5 hadi 10%
-Mafua ya kuku-hugonjwa huu huweza
kuambukiza kuku wengine kwa haraka katika banda kiwango cha vifo vya kuku huwez
kufikia 20% na huambukizwa kwa njia ya jicho au pua.
-Ugonjwa wa viungo vya ndani-njia za
maambukizi za ugonjwa huu ni kwa njia ya chakula na kiwango cha vifo vya kuku
huwa ni kwa 5-20%
-Gumbolo-ugonjwa uliogunduliwa kwa mara
ya kwanza 1962.uwezekano wa kuambukizana ni kubwa sana.Kiwango cha vifo
kinaweza kuwa kwa 20%-60%
-Ugonjwa wa kuharisha njano-huua kuku
kwa 70-80% bandani
Lakini pamoja
na kujifunza magonjwa tumejifunza dalili,njia za kwalinda kuku dhidi ya
magonjwahayo kwa kutumia chanjo mbalimbali za magonjwa hayo.
2.2.3 Lishe ya kuku
Pamoja na
kujifunza lishe za kuku wa nyama tulianza na vifaa vya kulishia kuku ambavyo ni
pamoja na vifaa vya kulia chakula(feeder),vifaa vya kunywea maji(drinker) na
chanzo cha joto kama vile umeme,jiko la mkaa,taa ya mafuta.
Kushoto pichani: Buruda la kukuzia
vifaranga linavyoonekana likiwa na
miundo mbinu ya umeme chakula na maji, buruda hili lilitumika katika mafunzo
ya vitend.Kulia ni walengwa
wamafunzo wakiwa katika mafunzo ya vitendo.
|
Lishe ni pamoja na:-
Chakula cha kuanzia, hupewa kuku wa
kuanzia umri wa siku 1-siku 21(wiki ya 1 hadi 3)
Growers, Chakula hiki hupewa kuku
kuanzia umri wa siku 22 –siku 28
Chakula cha
kumaliziachakula hiki huanzishwa mwishoni mwa wiki ya tatu na huwa kinachanganywa
na starter kwa muda wa siku 3-4 kabla ya kuacha kabisa kuwapa starter.
Maji –kuku wa nyama huitaji maji safi
na salama wakati wote yanayowekwa katika vyombo visafi, salama na
vinavyowezesha kuku kunywa maji kwa usalama.
Pia
tumejifunza kuhusu utunzaji wa chakula cha kuku.
2.2.4 Utunzaji wa kumbukumbu
Katika
utunzaji wa kuku tumejifunza kuweka kumbukumbu ya matukioa kadhaa muhimu katika
ufugaji wa kuku, kama vile:-
·
Kumbukumbu za mfugaji mwenyewe
·
Taarifa kuhusu kuku wenyewe toka kuwasili
·
Kumbuumbu za vifo
·
Kumbukumbu ya manunuz ya chakula
·
Kumbukumbu ya tiba na chanjo
·
Kumbukumbu Matumizi ya maji
·
Kumbukumbu Huduma mbalimbali
·
Kumbukumbu Mauzo y kuku
2.2.5 Mafunzo kwa vitendo
Baada ya
kujifunza kwa nadharia tulipata nafasi ya kujifunza ufugaji wa kuku kwa vitendo
tukianzia na kuku 100.Mambo muhimu tuliyojifunza ni pamoja na:-
-Kundaa banda
kabla ya kuweka vifaranga
-Kutenegeneza
mahala pa kulelea vifaranga (buruda)
-Kupokea
vifaranga
-Kutengeneza
miundombinu ya joto
-Kulisha vifaranga
na
-Kuchanja
vifaranga
3.0
MAFANIKIO
Ø Kuongezeka
kwa uelewa wa walengwa (maalbino) 6 walioshiriki katika mafunzo kwa muda wa
siku 14.
Ø Washiriki
walishiriki kwa siku zote 14, hakukuwa na mgonjwa wala utoro.
Ø Tumejenga
husiano mwema na wakufunzi na mafunzo na kuwa pamoja kwa hali wakati na baada
ya mafunzo.
4.0 MAPENDEKEZO
4.1 Mapendekezo ya walengwa wa mafunzo.
ü Washiriki
wanashukuru kwa hatua muhimu katika mradi lakini wanapendekeza kuwa ufadhili
uendelee ili kuwezesha mradi huu kutekelezwa mpaka mwisho.
ü Wadu
zaidi wajitikeze ili kuwezesha mafunzo haya kuwakifikia walengwa zaidi hata
kama italazimika kutumia walengwa 6 waliowezeshwa kipindi hiki.
4.2 Mapendekezo ya wakufunzi
ü Wakufunzi
walipendekeza kuomba fedha ili kulipia mabanda ya chuo kwaajili ya shughuli za
mradi wa ufugaji.
ü Kuendelea
kupeleka wanachama wa Albino unity na maalbino wengine ili kuwezesha mafunzo
zaidi kwa albino.
5.0 HITIMISHO
Tanzania Albino Unity kwa uwezeshaji kutoka, Tume ya uwezeshaji
imepata nafasi ya kuwakilisha Maalbino 6 kushiriki mafunzo ya siku 14 ya
ufugaji wa kuku wa nyama katika chuo cha wakala wa vyuo vya mifugo kilichopo
Vetenari, Temeke, Dar-es-salaam.
Wawakilishi hawa kwa uchache wake, tumedhamilia kuhakikisha kuwa
tunajitahidi kwa kadili itakavyowezekana kuweka mafunzo tuliyopata katika
vitendo.Tunamatarajio ya pamoja na kuyatuia kwaajili ya kwetu binafsi katika
mradi, tutawasambazia Maalbino wengine ili kusambaza manufaa ya mafunzo haya.
Rai yetu ni kwa wadau mbalimbali kuunga mono juhudi za Tume za kutoa
ufadhili ili kuwezesha utekelezaji wa mradi wote,kwa kuwa mafunzo ni sehemu tu
ya mradi mzima wa ufugaji wa kuku wa nyama.Mradi huu ukifanyika utawezesha
kuinua kipato cha Maalbino na hivy kupunguza hadha ya kuombaomba. Tunawasilisha.