Saturday, September 20, 2014

Yanga yashikwa shati na mtibwa leo
TIMU ya Yanga jana ilishindwa kufurukuta mbele ya Mtibwa Sugar

baada ya kuchapwa mabao 2-0, katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi

Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini

hapa.

Mpira ulianza kwa timu zote kushambuliana, ambapo Yanga ndio

waliokuwa wa kwanza kufika katika lango la Mtibwa dakika ya

kwanza kabisa baada ya Genilson Santana Santos ‘Jaja’ kupiga

shuti kali nje ya 18 lakini mpira ukapaa juu.

Dakika ya tisa Mtibwa Sugar walifanya shambulizi la kustukiza,

ambapo beiki wao Andrew Vicent alipiga shuti lakini kipa wa

Yanga aliliona na kudaka.

Dakika ya 16 Mtibwa walipata bao la kwanza kupitia kwa

mshambuliaji wa zamani wa Simba Mussa Hassan 'Mgosi' baada ya

kupigwa pasi ndefu na Ali Shomari, baada ya bao hilo nyuki

wakavamia uwanjani hali iliyowalazimu wachezaji pande zote mbili

kulala uwanjani kwa sekunde kadhaa.

Dakika ya 31 Yanga wanakosa bao la wazi kupitia kwa Jaja baada

ya Haruna Niyonzima kupiga mpira wa kona na kumkuta Jaja ambaye

alipiga mpira wa kichwa lakini kipa wa Mtibwa akaokoa.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Mtibwa walikuwa wakiongoza

bao 1-0, katika kipindi hiki timu zote zilikuwa zikishambuliana

kwa zamu na kosa kosa za hapa na pale.

Kipindi cha pili kilianza, huku kila timu ikitafuta bao la

ushindi.Dakika ya 46 Yanga wanakosa bao baada ya Shaaban Nditi

kunawa mpira eneo la hatari, lakini Jaja akakosa penalti hiyo.

Baada ya mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Yanga Marcio Maximo

kumtoa Kiiza na kumwingiza Simon Msuva mpira ulibadilika sana,

dakika 51 Yanga walikosa bao la wazi kupitia Nadir Haroub

Cannavaro aliyewahi mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna

Niyonzima.

Dakika ya 61 Yanga walikosa bao tena kupitia kwa Jaja akiwa

ndani ya 18 huku kipa akiwa anaufuata mpira, alipiga mpira nje.

Dakika ya 82 Mtibwa walipata bao la pili kupitia kwa Ame Ally

baada ya mabeki wa Yanga kujua aliotea, mpira ulipigwa wa pasi

ndefu.

Dakika 15 za mwisho Yanga walishambulia sana lakini bahati

haikuwa yao.

Kikosi cha Yanga: Deogratius Mushi, Juma Abdul, Oscar

Joshua/Omega Seme dk 31, Nadir Haroub 'Cannavaro, Mbuyu Twite,

Kelvin Yondan, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Khamis

Kiiza/Simon Msuva 46, Genlson Santos 'Jaja' na Mrisho Ngassa.

Mtibwa Sugar: Said Mohammed, Hassan Ramadhan, David

Luhende/Majaliwa Hassan 64, Salim Mbonde, Andrew Vicent, Shaaban

Nditi, Ally Shomari, Mzamiru Yassin, Ame Ali, Mussa Mgosi/Vicent

Barbanas dk 50, Mussa Nampaka.

No comments:

Post a Comment

ROSEMARY LUHAMO KUTOKA DODOMA AKABIDHIWA MAMILIONI YAKE NA UMOJA SPESHO

 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo akiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa pesa zake kupitia Benki ya CRDB na Kampun...