Wednesday, October 8, 2014

FINCA Tanzania M.F.C Limited yazindua ‘Fika na FINCA’FINCA Tanzania imezindua ‘Fika na FINCA’, kampeni inayolenga kuwafikia Watanzania wote kupitia huduma za kibenki na kuwasaidia kutimiza malengo ya kimaendeleo waliyojiwekea. Mnamo Januari 2013 FINCA ilikuwa microfinance ya kwanza kupata leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania inayoiruhusu kupokea na kutunza akiba, na tangu hapo, mbali na mikopo ya aina mbalimbali, FINCA imekuwa ikitoa huduma ya akaunti za akiba kwa wateja wake.
Faida za akaunti za akiba za FINCA ni nyingi, ikiwa ni pamoja na urahisi wa kufungua na kuendesha akaunti, taratibu za kufungua akaunti zina mahitaji madogo, kutoa na kuweka pesa ni bure kwenye matawi yote nchini, na usalama wa fedha za mteja kupitia mfumo wa bayometriki unaotumiwa na benki hiyo. Vilevile kupitia akaunti ya muda maalum (Mipango), FINCA inampatia mteja faida kubwa zaidi ya 14%.Mteja wa mara ya kwanza sasa anaweza kupata mkopo wa hadi Tshs. milioni 150 ndani ya siku 5 tu. FINCA inatoa pia Mkopo wa Kilimo kwa wakulima hasa wale walio katika maeneo ya vijijini na Mkopo wa Elimu kusaidia wamiliki wa taasisi za elimu na wale wanaohitaji kulipia ada za watoto na ndugu zao.
Kupitia njia mbalimbali za kutoa huduma, FINCA inaendelea kurahisisha maisha ya mteja na kutoa kipaumbele kwa mahitaji ya mteja. Kwa kutumia huduma za kibenki kupitia simu za mkononi na huduma ya wakala wa FINCA Express iliyoanzishwa hivi karibuni, wateja wanaweza kupata huduma wakati wowote, popote walipo.
Kwa zaidi ya miaka 16 FINCA imeaminiwa na wananchi katika kuwapatia huduma za kifedha na inapanga kuendeleza viwango vyake kama benki inayowajibika kuhudumia na kuwawezesha Watanzania kwa ujumla.Kuhusu FINCA Tanzania:
FINCA Tanzania ni moja kati ya taasisi 23 za FINCA Microfinance Holding Company (FMH), yenye makao yake makuu Washington DC nchini Marekani na kuendesha shughuli zake katika bara za Latin America, Eurasia, Mashariki ya Kati, na Afrika. FMH inahudumia karibu wateja 2,000,000. Wanahisa wa FINCA ni pamoja na The International Finance Corporation (IFC) – ambayo ni sehemu ya World Bank, The German Development Bank - KfW, The Dutch Development Bank - FMO, ResponsAbility (kampuni ya Uwisi inayowajibika katika jamii kwenye uwekezaji), TripleJump (kampuni ya Uholanzi inayowajibika katika jamii kwenye uwekezaji), Nederlandse Financierings- Maatschappij voor Ontwikkelingslanden, Credit Suisse Microfinance Fund Management Company, ASB-Novib Microkredietfonds, FINCA International Inc.

No comments:

Post a Comment

MWENGE WA UHURU WAINGIA GAIRO NA KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA MILIONI MIASABA NA ZAIDI

 Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Morogoro Regina Chonjo mara ulipofika katika eneo la Ma...