Monday, October 6, 2014

MTOTO AMUOA MAMA YAKE WA KAMBO


Bwana mmoja nchini Ufaransa amemuoa mke wa zamani wa baba yake (mama yake wa kambo) baada ya kushinda kesi iliyodumu kwa miezi kadhaa.
Harusi ya Eric Holder, 45, na aliyekuwa mama yake wa kambo Elisabeth Lorentz, 48, ilifanyika katika kijiji cha Dabo, karibu na mji wa Metz.
Imeripotiwa kuwa mume wa zamani wa bi harusi, ambaye ni baba wa Bwana Holder, alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.
Sheria za Ufaransa zinapiga marufuku ndoa kati ya watoto wa kambo na wazazi wa kambo, lakini mahakama ilitoa uamuzi wa ndoa hiyo kufanyika.
Ofisi ya mwendesha mashtaka ilipinga uamuzi huo wa mahakama katika eneo la Lorraine, lakini ikaamua kutokata rufaa.
Awali, wawili hao walipeleka malalamiko yao hadi katika ofisi ya Rais Francois Hollande - lakini walipata barua kuthibitisha kuwa ndoa za aina hiyo ni marufuku.
Baada ya uamuzi wa mahakama, bi harusi alisema: "Hatimaye, ile siku kuu imewadia!"
"Kwa kweli nina imani kuwa habari yetu itasaidia wapenzi wengine waliopo kwenye hali kama hii, kwa sababu najua wapo kadhaa," ameliambia shirika la habari la AFP.
Bi harusi huyo ameongeza kusema kuwa mume wake wa zamani amekuwa "akiwaunga mkono" katika mapambano ya kisheria.

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...