Wednesday, October 8, 2014

RAIS KENYATTA NDANI YA ICC

Rais Kenyatta wakati akiwasili katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huko The Hague.

Rais Kenyatta wakati akielekea The Hague jana. 

Rais Kenyatta ni kiongozi wa kwanza wa taifa kuwasili mbele ya mahakama hiyo.
Kenyatta amefika mbele ya mahakama hiyo baada ya waendesha mashtaka kuishutumu serikali ya Kenya kukataa kuwasilisha ushahidi muhimu.
Kenyatta amekanusha madai ya kupanga na kufadhili ghasia za kikabila nchini Kenya baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mwaka 2007/2008.
Kikao cha leo kitatathmini ombi la upande wa mashitaka la kutaka kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi pale serikali ya Kenya itakapoikabidhi mahakama hiyo ushahidi unaohitajika kuhusiana na mali ya Rais Kenyatta.
Upande wa utetezi nao unataka kesi hiyo ifutiliwe mbali ukisema kuwa upande wa mashitaka hauna ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea.
Kiongozi wa mashitaka, Fatou Bensouda, amewasili mahakamani akisema kesi hiyo iko katika awamu muhimu sana.
Kenyatta ameamua kukaa kimya akimtaka wakili wake kuongea kwa niaba yake.

No comments:

Post a Comment

M-KOPA YAFUNGA UMEME JUA WENYE THAMANI YA Tshs 4,959,000. KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWINYI MKURANGA PWANI

 Meneja Msaidizi wa M-Kopa nchini , June Muli akikabidhi boksi la Vifaa vya umeme wa jua kma ishara ya makabidhiano ya mradi wa umeme uli...