Wednesday, November 19, 2014

Binti ajinasua na ndoa ya wana mgambo

Mwanamke mmoja raia wa Uholanzi amewasili nchini Uturuki baada ya safari iliyojaa hatari nchini Syria kwa ajili ya kumchukua binti yake aliyekua mjini Raqqa, mji unaokaliwa na waasi wa Islamic State.
Monique alikwenda Uturuki mara ya kwanza baada ya binti yake aitwae Aicha kusafiri kwenda Syria kuoana na mmoja wa wanamgambo wa kundi hilo mwenye asili ya Uholanzi na Uturuki.
Mamia ya Wanamgambo wenye asili ya Ulaya wamekua wakienda Syria kupigana ndani ya kundi la IS.
Aicha ,19 ni miongoni mwa Wasichana ambao walisafiri kujiunga na IS.Raia wawili wa Austria wenye umri wa miaka 15 na 17 walikwenda Syria Mwezi Aprili na mmoja wao aliripotiwa kuuawa.
Aicha aliondoka Uholanzi mwezi Februari, akaolewa na Omar Yilmaz, mwanamgambo mwenye asili ya Uturuki na Uholanzi ambaye alishawahi kuwa mwanajeshi nchini Uholanzi,alitumia mbinu alizopatiwa akiwa mwanajeshi na kuwafunza wapiganaji wenzake.
Monique amesema mwanae alibadilika ghafla kutoka binti aliyefahamika vyema na kuwa Msichana mwenye msimamo mkali.
Wapiganaji wa Islamic State wakifanya mashambulizi
Baada ya Polisi kumuonya Aicha kutosafiri kwenda Syria walikamata Pasi yake ya kusafiria, Aicha hakuvunjika moyo alitumia kitambulisho chake.
Aicha alikuwa akiwasiliana na Yilmaz kwa njia ya mtandao wa kijamii kisha wakapendana.
Monique alisafiri mpaka Uturuki mwezi Oktoba ili kumchukua mtoto wake lakini alishindwa kuvuka mpaka.
Lakini wiki iliyopita, baada ya Aicha kuomba msaada alirudi tena nchini Syria ingawa Polisi walimkataza kufanya hivyo.Monique alifika Raqqa nchini humo na kumchukua bintiye kisha kurejea Uturuki
Yilmaz, Mume wa Aicha anamtaja mkewe kuwa mtalaka wake kwenye anuani yake ya Tweeter.
Hivi sasa Mama na mwana wanashikiliwa mpakani mwa Uturuki, wakisubiri ruhusa ya kurudi Uholanzi.
Serikali ya Uholanzi imeiambia BBC kuwa inawasiliana na Monique lakini haijatoa ufafanuzi zaidi, tatizo ni kuwa Aicha hana Pasi ya kusafiria ingawa mwanasheria wake anasema huenda wakarejea Uholanzi ndani ya wiki moja.

No comments:

Post a Comment

TFS NA WADAU WAANZA SAFARI YA KUELEKEA MISITU YA AMANI

 Meneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS),Mariam Kobelo akigawa Vipeperushi kwa Wakazi wa Dar es Salaam amb...