Eric Baume, head of cooperation to European Union,Tanzania
Na Humphrey Shao , Dar es Salaam
Na Humphrey Shao , Dar es Salaam
SERIKALI imetangaza kuendelea kudhibiti baadhi ya watu wasio
waadilifu ambao wamekuwa na tabia ya kusafirisha watoto ndani na nje ya nchi
kwa ajili ya kwenda kuwatumikisha kazi za majumbani.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia
na Watoto Pindi Chana kwenye mkutano wa kujadili miaka 25 ya mkataba wa Haki za
Watoto Duniani.
Alisema ili kudhibitisha hilo katiba mpya inayotarajiwa
kupigiwa kura ya maoni ya kuikubali au kuitakaa kuna ibara ya 53 inayozungumzia
haki ya watoto ikiwamo ya kupata elimu, kupinga ukatili na kupata huduma za
afya.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia
na Watoto Pindi Chana kwenye mkutano wa kujadili miaka 25 ya mkataba wa Haki za
Watoto Duniani.
“Serikali iliungana na mataifa mbalimbali Duniani ili
kuridhia haki ya mtoto kulindwa, kupata elimu, afya na kuondoa ukatili wa
jinsia.
“Ili kutekeleza hilo, katiba mpya ibara ya 53 inazungumzia
haki ya watoto kwa ujumla, hivyo basi mtu atakayebainika anakwenda kinyume na
haki hizo serikali itamchukulia hatua za kisheria,”alisema Chana.
Aliongeza kutokana na hali hiyo serikali imejipanga
kuhakikisha kuwa inazuia biashara haramu ya watoto pamoja na kudhibiti vitendo vya ukatili vinavyofanywa
na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakisafirisha binadamu wenzao kama wanyama
katika nchi za Magharibi.
“ mkakati wa serikali ni kuhakikisha kuwa inashirikiana na wadau
mbalimbali ili kufanikisha mipango na kuhakikisha kuwa haki ya mtoto inalindwa
kuanzia nyumbani hadi katika jamii hili kupata kizazi ambacho kitakuwa na
uadilifu na weredi”.