Tuesday, November 4, 2014

wamarekani-wapiga-kura-uchaguzi-wa-kati-kati-ya-awamu

Wapiga kura kote Marekani wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa kati kati ya awamu ambao utaamua kama wa-Democrat au wa-Republican wanadhibiti baraza la seneti katika muda wa miaka miwili uliobaki madarakani kwa Rais Barack Obama.
Viti vyote 435 katika baraza la wawakilishi na theluthi moja ya viti 100 vya baraza la seneti  vinagombaniwa. Lengo kuu ni baraza la seneti,  ambapo wachambuzi wengi wa kisiasa wanasema wa-Republican wanaelekea kushinda viti sita muhimu ili kuweza kudhibiti baraza hilo kutoka chama cha Democrat cha bwana Obama ambacho kinashikilia wingi wa viti 55.
Huku kiwango cha utendaji kazi cha rais kikiwa kimeshuka mpaka asilimia 40 fursa nzuri  ya chama cha Republican ni viti kadhaa ambavyo bwana Obama alivipoteza miaka miwili iliyopita wakati wa kampeni yake ya kuchaguliwa tena.
Wa-Republican wanatarajia kuendelea kushikilia na pengine  kujiongezea viti zaidi katika bunge.
Ukusanyaji  maoni wa hivi karibuni unaonyesha kwamba wagombea wa chama cha Republican watashinda kirahisi katika kinyang’anyiro cha seneti huko West Virginia, South Dakota na Montana majimbo ambayo hivi sasa yanashikiliwa na wa-Democrat.  Maoni hayo  pia yanaonyesha kuwa wa-Republican pia wanatarajiwa  kushinda kinyang’anyiro cha seneti katika majimbo ya Iowa, Colorado na Alaska japokuwa huenda ikachukua saa kadhaa au hata siku kabla ya matokeo rasmi kujulikana.
Vinyang’anyiro viwili huko kusini, Georgia na Louisiana wamefungana na watahitajika kufanya uchaguzi wa marudio.

    No comments:

    Post a Comment

    MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                             Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...