Warepublican wachukuwa udhibiti wa bunge la Marekani

Warepublican wameweza kunyakua kiti cha sita cha Baraza la Senet na hivyo kuchukua udhibiti wa bunge kamili baada ya kuongeza wingi wao katika Baraza la Wawakilishi.
Wademocrats walikuwa na viti 55 katika Baraza la Senet, lakini Warepublican waliwapokonya viti sita, kwa kushinda katika majimbo ya Arkansa, Colarado, Montana, Carolina ya Kaskazini, Dakota ya Kusini na Virginia ya Magharibi.
Wanachama wa chama hicho wanasherekea katika kila pembe ya nchi baada ya kupata ushindi mkubwa wa bunge pamoja na ushindi muhimu katika uchaguzi wa magavana, mabunge ya majimbo na serikali za mitaa.
Wachambuzi wengi wanasema wademocrats wameshindwa kutokana na kwamba Wamarekani hawaridhiki na sera za ndani na nje za Rais Barack Obama, na wagombea wake wengi hawakutaka kujihusisha na mafanikiyo yake.
Rais Obama hivi sasa hana budi bali kufanya kazi na chama cha upinzani kuweza kukamilisha sera zake za mwisho wa muhula, na wachambuzi wanasema hivi sasa anaweza kuonesha kwamba anaweza kuliongoza taifa hili baada ya kushambuliwa kutoonesha uwongozi ulohitajika.

Post a Comment

Previous Post Next Post