Saturday, December 20, 2014

Jerry Muro awa bosi wa kizuguto YangaYANGA imefumua benchi lake la ufundi na kumtupa chini kumpa ulaji mnono mmoja wa waandishi wa habari mahiri hapa nchini Jerry Muro kuwa afisa habri mkuu badala ya aliyekuwa mkuu na mkuu wa kitengo hicho  Baraka kizuguto kuweka kand.

kwa mujibu wa taharifa zilizotufikia zinasema kuwa Mabadiliko hayo yalitangazwa jana na klabu hiyo ambapo Mholanzi Hans van der Pluijm ndiye aliyebebeshwa mikoba ya benchi hilo, akisaidiwa na mzawa Charles Boniface Mkwasa, huku Mbrazil Marcio Maximo na msaidizi wake, Leonardo Neiva wakipewa mkono wa kwaheri. 

Kiziguto amabye alikuwa analalamikiwa na waandishi w ahabari wengi kutokana na tabia yake ya kudharau wanahabari na kusahau majukumu yake anasubiri kupangiw akazi nyingine ya kufanya.
  
Mbali ya mabadiliko hayo ya benchi la ufundi, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, pia amefanya mabadiliko katika sekretarieti ya klabu hiyo ambayo sasa itaongozwa na Katibu Mkuu Dk. Jonas Tiboroha ambaye atafanya kazi na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Jerry Muro, Mkuu wa Idara ya Masoko, Omar Kaya, Mkuu wa Idara ya Sheria, Frank Chacha na Mkuu wa Idara ya Fedha, Baraka Deusdedit.  

  kuteua mabosi wapya watakaoiongoza timu hiyo kuanzia leo, huku kibarua chao cha kwanza kikiwa ni mchezo wa raundi ya nane ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Desemba 28, mwaka huu dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Akisoma taarifa hiyo ya Manji iliyosainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, Muro alisema kuwa klabu hiyo imeamua kujipanga upya kwa kuteua watendaji kadhaa, wengi wakiwa ni vijana ili kujiimarisha zaidi.
   kwa pamoja waliwahi kukinoa kikosi cha timu hiyo mwaka huu kabla ya kutimkia katika nchi za Falme ya Kiarabu kwenda kufundisha soka.
Rekodi ya Pluijm alipokuwa akiifundisha Yanga kwa mara ya kwanza inaonyesha kwamba, aliiongoza katika mechi 18 zikiwemo za Ligi Kuu Klabu Bingwa Afrika na za kirafiki ambapo kati ya hizo, alishinda 11 akatoka sare sita na kupoteza mbili.
Kabla ya kujiunga na Yanga kwa mara ya kwanza, Pluijm alishafanya kazi katika klabu mbalimbali za Afrika, ikiwemo Belkum Chelsea ya Ghana pamoja na Saint Georges ya Ethiopia.
Yanga imeamua kuvunja benchi la ufundi baada ya timu hiyo kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya mahasimu wao Simba katika pambano la kirafiki, lililopewa jina la Nani Mtani Jembe lililochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Waziri Dk Kigwangalla ataka wavamizi maeneo yaliyohifadhiwa kuondoka

Mwandishi wetu,Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewataka wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi nchini,...