Monday, August 4, 2014

WASIWASI UMEIGHARIMU TAIFA STARS- NOOIJ

WASIWASI UMEIGHARIMU TAIFA STARS- NOOIJ
Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema moja ya sababu za kikosi chake kupoteza mechi dhidi ya Msumbiji (Mambas) ni wachezaji wake kucheza kwa wasiwasi katika kipindi cha kwanza.

Taifa Stars iliruhusu bao la kwanza sekunde chache kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kucheza hatua ya makundi iliyochezwa leo (Agosti 3 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimpeto hapa Maputo.

Bao hilo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3 lilifungwa kwa kichwa na mshambuliaji Josemar Machaisse.

Nooij alisema wasiwasi katika kipindi cha kwanza ndio ulioipa Msumbiji fursa ya kutawala mechi hiyo katika kipindi hicho na kukimalizia ikiwa mbele kwa bao hilo la mshambuliaji huyo wa klabu ya Bravos de Maquis ya Angola.

Alisema timu yake ilitulia kipindi cha pili baada ya kumuingiza Amri Kiemba badala ya Khamis Mcha. Pia alilalamikia bao ambalo Taifa Stars ilifunga dakika ya 16 kupitia kwa John Bocco lakini likakataliwa na mwamuzi Dennis Bate kutoka Uganda.

Aliongeza kuwa mchezaji Elias Pelembe aliyeifungia Msumbiji bao la pili dakika ya 83 kwa mpira wa adhabu nje ya eneo la hatari ndiye aliyemaliza mchezo huo. Pia ni mchezaji huyo aliyebadili matokeo ya mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam ambapo Msumbiji ilisawazisha dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na ambayo ilicheza vizuri kipindi cha pili ilipata bao lake dakika ya 78 na Mbwana Samata kwa shuti la pembeni akiwa nje ya eneo la hatari na kumshinda kipa Ricardo Campos.
Matokeo hayo yameipeleka Msumbiji katika kundi C lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia. Mechi za hatua ya makundi kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco zitaanza kuchezwa mwezi ujao.

Mechi hiyo ndiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya Tanzania na Msumbiji itakayoingia hatua ya makundi ya michuano ya Afrika kwa ajili ya kutafuta tiketi za Fainali itakayofanyika mwakani nchini Morocco.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Timu itakayosonga mbele itaingia kwenye kundi lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia.

Taifa Stars inarejea Dar es Salaam kesho (Agosti 4 mwaka huu) saa 8 mchana kwa ndege ya Air Tanzania.

Kikosi cha Stars kilipangwa hivi; Deogratias Munishi, Said Moradi, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Erasto Nyoni, Mwinyi Kazimoto, Mcha Khamis/Amri Kiemba, John Bocco/Simon Msuva, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu/Mrisho Ngasa.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
MAPUTO

Kamanda Kova amuanika askari bandia wa usalama barabarani

 Kova akionyesha mguu bandia unaotumika kuficha dawa za kulevya

 Kamisna kova akinyehs meno ya tembo kwa waandishi

Pepsi yazindua Soda mpya inayojulikana kwa jina Mirinda Green apleSales Manager of  Pepsi Tanzaia,Godlistern Mende(Right), and  area Sales Manager , Omary Madaya, Show to journalist a new bland of Mirinda green aple to journalist recently in Dar es Salaam. Photo by Humphrey Shao.


 waandishi wa habari wakionja soda hiyo kwa mara ya kwanza

 Ceo  wa JIJI letu blog Humphrey Shao akiwa na afisa mauzo wa pepsi Zainabu mchovu

Sheikh Issa Ponda akipandishw akizimbani katika mahkama kuu jijini Dar es SalaamSunday, August 3, 2014

Simba yawafukuza wanachama 72

 Rais wa Simba evance aveva
Safari ya Bitchuka na muziki wa Tanzania-2

Safari ya Bitchuka na muziki wa Tanzania-2
**Aliajiriwa Msondo akiwa ziarani

NA JIMMY CHIKA
WASTAHIKI wasomaji wa makala haya, wiki iliyopita tulianza kuona safari ya mwimbaji nguli wa muziki wa dansi Hassan Rehani Bitchuka.
Kwa uchache tuligusia safari yake iliyomtoa Arusha na kuja jijini Dar na kujiunga na bendi ya NUTA.
Tumepata maoni mengi kutoka kwa wasomaji, hasa wale waliotujulisha safari nyingine ya mwimbaji huyo, hususan alipowahi kufanya muziki kabla ya kuwepo Arusha na NUTA Jazz.
Kwetu tunaamini kwamba mwimbaji huyo, kwa hakika ameitumia nafasi yake kwa weledi na muda mrefu, na kwamba si rahisi kupagusa kila alipopita.
Kwa uchache huu tutaangalia yale tuliyobahatika kuyagusa, na pia tutaendelea kupokea ushauri, maoni na hata pongezi kama zipo.


Naam, usiku wa takriban saa nne hivi ikiwa bendi ya NUTA imeshatumbuiza nyimbo kama tatu hivi, hatimaye mwimbaji wake (Marehemu) Muhidin Gurumo anatangaza ujio wa mwanamuziki chipukizi, Hassan Bitchuka, hiyo ilikuwa mwaka 1973.
Hatimaye Bitchika anakabidhiwa kopaza sauti na kuimba wimbo ninaoukumbuka kwa mameno.
"Ukiwa kama hunitaki dada"
Ukumbi ulitamalaki, watu wakapagawa, na mifuko yake ikafurika tuzo, kwa ujumla aliimba kwa ufasaha mkiubwa na sauti ya kughani.
Viongozi wa NUTA Jazz kwa umoja wao wakiwa na wanamuziki kama Kiiza Hussein, Ahmad Omar, Mabruk Khalfan, Joseph Lusungu, Mnenge Ramadhani, Abel Baltaza na Muhidin Gurumo wakafurahi kuliko ilivyokuwa kwa mashabiki.
Hapo ndipo ilipopigwa simu jijini Dar es Salaam katika ofisi za Jumuia ya Wafanyazi enzi hizo NUTA kutaja kijana huyo afungulie ajira mara moja.
Bitchuka aliporea jijini alikuwa na kazi moja tu ya kutia saini faili lake na ndipo maisha mapya na matamu ndani ya NUTA jazz yalipoanza.

AIBUKA NA MSONDO WA NUTA
Siku chache baada ya kuzoeana na wanamuziki, hasa Ahmed Omar anayemsifu kwamba alikuwa akifahamu vizuri lugha ya Kishwahili, Bitchuka akaibuka na wimbo uitwao Msondo wa NUTA.
Kati ya nyimbo zilizolete mabadiliko makubwa katika bendi hiyo ni pamoja na huo, ambao ni utunzi wake wa kwanza Hassan Bitchuka kabla ya Mpenzi Zalina na Aziza.

Katika hali nyingine ujio wake ulimuunganisha vizuri na mkongwe Gurumo ambaye aliridhia kuacha kuimba sauti ya kwanza na kumuachia rasmi kijana huyo enzi hizo huku yeye akihamia rasmi sauti za chini, yani ya pili na ya tatu.

Ukipata nafasi ya kusikiliza wimbo uitwao Mume wangu, utaona jinsi magwiji hawa kwa pamoja walivyoziichea sauti zao kwa ujuzi wa hali ya juu.

Habu ukumuke kidogo wimbo huu.
Mume wangu nirudishe kwetu kwa baba na mama.
Sababu watoto wako sielewani nao, kila nisemaloo wasema mimi mama wa kambo.
Kumbuka nilikueleza usimuache mama wato wako, watoto wengi mmekwisha zaa naye mrudie mama wato wako...

Hayo ni baadhi ya maneno yaliyomo kwenye wimbo huo ambao ndani yake una sauti mbili yani ya Bitchuka na Gurumo.

Umaarufu wa Bitchuka sasa ulianza kusambaa na hadi kutoka nje ya jukwaa.
Kwani marafiki waliongezeka na hasa wafanyakazi wa ngazi mbalimbali katika jumuia ya wafanyakazi nao walijisogeza karibu yake.
Mialiko mbalimbali iliyoambatana na posho za hapa na pale havikukauka kwa mwanamuziki huyo.
Vilevile ndani ya bendi walijikuta wakiunda 'upacha' wa sauti kati yake na Gurumo, pia wapiga magitaa wakahusudu sana kuikia sauti yake kila wanapotengeneza wimbo mpya.
Kuanzia hapo Bitchuka alikuwa ni yeye na Msondo.
Lakini kila panano mazuri na mabaya yapo, ukaribu wa yeye na Gurumo hatimaye ulifikia tamani, wakaachana, hawakuwa pamoja tena, ule uipacha ukapotelea gizani, unajua ni kwa nini..Fuatilia makala hii Jumapili ijayo.
&&&&

WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WATAKIWA KUWA WAADILIFU

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,Amina Khamis Shaban amesema hakuna sababu yoyote ya T...