Saturday, August 16, 2014

PICHA MBALIMBALI UN TANZANIA ILIVYOAZIMISHA WIKI YA VIJANA VIWANJA VYA CHUO KIKUU

 Naibu katibu mkuu wizara ya habari vijana utamaduni na michezo akitembelea mabanda
 kiongozi wa makangarawe Youth akitoa somo kwa wanafunzi waliofika hapo

 mechi ikiendelea kati ya Don bosco lady Lions na magereza
Tuesday, August 12, 2014

Tanzania yaandaa mkutano wa Magavana        
   


        
   
 
Tanzania yaandaa mkutano wa Magavana
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 30 wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki (BOG) utakaofanyikia jijini Dar es salaam tarehe 22 mwezi huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile na Rais wa Benki ya PTA kwa vyombo vya habari, mkutano huo utakuwa wa siku moja.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa lengo la mkutano huo ni  kujadili masuala mbalimbali ya kibenki ikiwemo mpango mkakati wa benki hizo na masuala ya fedha na uchumi kwa nchi washirika.

Wajumbe wa mkutano huo ni Mawaziri wa Fedha na uchumi wa nchi washirika ambao ndio chombo cha juu cha ngazi ya maamuzi ya benki katika nchi zao.

Aidha, taarifa hiyo imeongeza  kuwa mkutano huo utatanguliwa na semina ya wafanyabiashara itakayofanyika Agosti 21 siku moja kabla ya mkutano mkuu wa Magavana hao.

Benki ya PTA ilianzishwa mwaka 1985 ikiwa na jumla ya washirika 22 ikiwemo nchi 18 ambazo ni Burundi, Comoros, Djibouti na Congo.

Nchi nyinine ni Misri, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Malawi, Mauritius, Rwanda, Seychelles, Somalia, Sudan, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania.

Aidha, PTA inashirikiana na nchi nyingine nje ya bara la Afrika ambazo ni Belarus na China.
Washirika wengine Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Kampuni ya Bima ya Mauritia iitwayo Eagle na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Mauritius.

 
   

 
   

Matukio katika picha Uzinduzi wa studio za BBC Swahili Dar es Salaam

 Dk Salim Hamed Salim, akiwa na Prof Lipumba wakipata maelekezo kutoka kwa mtangazaji mkongwe Aly Salehe jinsi Studio hizo zinavyofanya kazi kisasa
 Abdul Mohamed mtangazaji wa Michezo akitoa maelekezo  kwa D.k Helen Kijo Bisimba
 CEO wa Jiji letu blog Humphrey Shao akiwa na mtangazaji mahiri Salim Kikeke
 picha ya pamoja ya wageni maharufu na mkurugenzi wa habari barani afrika Nikki Clarke
 Mrisho mpoto akiwa na wadau mbali mbaliSunday, August 10, 2014

Dimond ala bata na wema Ziwa VictoriaDEMU WA BONGO MOVIE AMFUKUZISHA LOGA KAZI SIMBA

 Mmoja wa wasanii maharufu wa tasni aya filamu amabye jina lake lina fanana na moja ya sofa maharufu Duniani ametajw akuwa ni chanzo cha kufukuzwa kwa kocha wa simba Zdravko Logarusic mara baada ya kumfungia mpaka saa saba za usiku mara baada ya kumalizika kwa mechi ya simba day.

Msanii huyo ambaye alishatajw amara kwa mara katika baadhi ay mitandao ya kijamii kuwa namhusiano na loga na ni mmoja kati ya wasanii wajane ambao wapo katika tasnia ya filamu hpa nchini ameweza kumduwaza kocha huyo kiasi cha kusahau majukumu yake.


Kocha wa Simba, Zdravko  Logarusic, akitoka nje ya hoteli ya serena jijini Dar es Salaam huku akisindikizwa na mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo,Colin Frisch, tayarai kwa safari ay kwenda kwao.Picha na Humphrey Shao. 


 Rasi wa simba evance aveva akizungumza na waandishi wa haabri katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam , pembeni yake ni Said Tully na Colin Fish

UJENZI WA NJIA NNE MOROGORO ROAD ENEO LA MBEZI WASHIKA KASI

Wakandarasi wakiendelea na ujenzi wa Roound about ya Msigani kama inavyoonekana katika picha Barabara ya Morogoro Road katika Mfumo wa nj...