Sunday, August 24, 2014

MKURUGENZI WA CLOUDS MEDIA GROUP RUGE MUTAHABA AKIMKARIBISHA MKUU WA WILAYA YA MKOA WA TANGA KUSHUHUDIA SHOO YA SERENGETI FIESTA


SOMO LALEO KATIKA IBADA YA JIJI LETU BLOG

Mathayo 5, 7 & 16, Yohana 17)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Sehemu kubwa ya kazi yangu kwa miaka mingi imejihusisha na kushughulikia kesi zinazohusu uhuru wa dini. Huwa ninawawakilisha “watu wadogo” pekee nikimanisha waajiriwa, katika nyanja za uhuru wa dini mahala pa kazi. Hata hivyo, swali la msingi sana katika kesi ya aina hii ni endapo mwajiriwa ana imani ya dhati katika dini. Nimejifunza kuepuka kuwawakilisha waajiriwa wasio na mafungamano ya dhati na kanisa mahalia. Watu ambao mara kwa mara wanaabudu katika kundi la waumini wana nafasi kubwa ya kuwa na imani za dhati katika dini. Kwa nini hivyo? Hebu tujifunze Biblia inachofundisha kuhusu muumini na kanisa!
I.                   Mwamba
A.                Soma Mathayo 16:13. Unadhani kwa nini Yesu aliwauliza wanafunzi wake swali hili?
B.                 Soma Mathayo 16:14. Unafikiria nini kuhusu majibu haya? (Hii ni orodha ya kufurahisha kuhusu uwezekano wa kwamba Yesu ni nani. Hata hivyo, kwa hakika majibu haya sio sahihi.)
C.                 Soma Mathayo 16:15-17. Petro analo jibu sahihi! Nani aliyempa msukumo wa jibu hilo? (Mungu.)
D.                Soma Mathayo 16:18. Je, palikuwepo na utatanishi kuhusu jina la Petro? Kwa nini Yesu anamwambia Petro, “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro?” (Kiyunani ni cha msingi hapa. Kwa Kiyunani Petro maana yake ni mwamba mdogo, au kipande cha mwamba. Yesu anacheza na maneno, “Nakuambia ewe kipande cha mwamba kwamba nitalijenga kanisa langu juu ya mwamba mkubwa.”)
1.                  Unadhani nini maana ya jambo hilo? (Soma kile anachokisema Petro kuhusu jambo hili katika 1 Petro 2:4-6. Petro anasema kwamba Wakristo ni “mawe yaliyo hai” yanayojengwa kwenye “nyumba ya Roho.” Yesu ndiye jiwe kuu la pembeni la nyumba hiyo.)
2.                  Hebu turejee kwenye mwamba mkubwa katika Mathayo 16:18. Unapotafakari mazungumzo ya wanafunzi na Yesu, unadhani “mwamba” (mwamba mkubwa) unawakilisha nini? (Nadhani mwamba ambao Kanisa linajengwa juu yake ni kauli ya Petro kwamba Yesu ni “Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” Yesu ndiye jiwe kuu la pembeni na uungu wake ni imani kuu.)
3.                  Hebu turejee nyuma kidogo. Unadhani maana kamili ya Mathayo 16:18 ni ipi? (Kwamba Kanisa linajengwa juu ya “mwamba” wa ufahamu kwamba  Yesu ni Mungu, na Kanisa linajumuisha miamba midogo midogo inayofahamu jambo hili, miamba kama vile Petro na wewe na mimi, na milango ya kuzimu haitatushinda.)


E.                 Soma Mathayo 16:19. Nani anayepewa “funguo” hapa? (Inaonekana kama vile ni Kanisa – au angalao washiriki wa Kanisa. Inaweza iwe vigumu sana funguo hizo kumaanisaha kuwa ni Yesu kwa kuwa Yesu hawezi kujipatia funguo yeye mwenyewe.)
1.                  Hii ni kauli madhubuti sana. Unadhani Yesu anamaanisha nini anaposema kuwa Kanisa linapewa “funguo za ufalme wa mbinbguni,” au angalao washiriki wa Kanisa wanatenda kazi pamoja kama Kanisa? (Nina uhakika sielewi kikamilifu muktadha wa kauli hii, lakini angalao kauli hiyo inasema kuwa Kanisa hufunua njia ya kwenda mbinguni. Kuwa katika kundi la waumini hutusaidia kuielewa neema na mwenendo wa Kikristo.)
F.                  Soma Mathayo 16:20. Ikiwa ukweli kwamba Yesu ni Mungu ni mwamba ambao Kanisa linajengwa juu yake, kwa nini jambo hilo liwe siri? (Mungu ana muda wake kwa ajili ya kila jambo. Huu ndio ukweli tunaopaswa kuwa nao mawazoni mwetu tunapokatishwa tamaa na kutokutenda kwa watu wengine.)
II.                Mtazamo
A.                Soma Yohana 17:20-23. Tuna dhana nyingi sana zilizopo kwenye haya mafungu. Kuna sababu gani ya kuwa na mtazamo wa umoja miongoni mwa waumini? (“Ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.” Umoja ndani ya kanisa hutoa ujumbe chanya kwa walimwengu wasioamini.)
1.                  Kiini cha ujumbe ni kipi? (Umoja hutokana na upendo. Mungu anatupenda nasi tunapendana.)
2.                  Je, kanisa lina hali gani katika kipengele hiki? (Unaweza kuwa umegundua kwamba tulipokuwa tukijadili Mathayo 16:19 niliruka lugha inayohusu Kanisa kufunga na kufungua masuala mbinguni na duniani. Ni vigumu sana kwangu kuelewa jinsi jambo hili linavyohusika sasa hivi wakati kuna makanisa mengi sana tena yenye viwango tofauti.)
3.                  Kauli nyingine ya kupendeza katika Yohana 17:22 ni kwamba Yesu “[ametupatia] utukufu ambao [Mungu Baba alimpa Yesu].” Je, huu utukufu wa Kiungu ambao wewe na mimi tunao ni upi? (Nadhani ni utukufu wa kushirikishwa na Mungu. Je, una ushirika fulani maishani unaokufanya upendeze? Hivi sasa nina gari jipya ambalo watu huwa wananisimamisha na kulizungumzia. Ikiwa una mwenzi mwenye mafanikio, watoto wenye mafanikio, kampuni yenye mafanikio, mashirikiano yote haya yanakupatia “utukufu.” Kuwa mshirika wa karibu wa Muumba wa Ulimwengu hutupatia utukufu.)
III.             Umoja Unapopata Pancha
A.                Soma Mathayo 7:1-2. Hili linaonekana kama jambo la kujifunza kivitendo. Kuna tatizo gani katika kuwahukumu watu wengine? (Nawe unahukumiwa kwa kiwango hicho hicho unachokitumia.)
1.                  Je, tunazungumzia hukumu ya mwisho? Je, hukumu hiyo ina kipimo kikubwa? Je, wale wasiojali chochote wanapata kiwango cha chini kabisa? (Kwa mara nyingine, hili linaonekana kama jambo la kujifunza kivitendo, badala ya kauli inayohusu hukumu ya mwisho.)


B.                 Soma Mathayo 7:3-4. Unadhani kwa nini mifano yote miwili, kibanzi na boriti, vinatengenezwa kwa mbao? (Nadhani huwa tunajielekeza kuangalia dhambi zetu ndani ya watu wengine. Ni dhambi ile ile, isipokuwa tu mtu mwingine anayo dhambi hiyo. Kimsingi, fungu linaashiria kwamba mtu anayehukumu ana tatizo kubwa zaidi.)
C.                 Soma Mathayo 7:5. Je, tunapaswa kuwa kwenye kazi ya kuondoa boriti? Jambo hili linalenga kujua kama tumejiandaa kikamilifu?
1.                  Je, ungependelea kuwa na kibanzi jichoni mwako? (Maatizo ya dhambi maishani mwetu yanatukera. Yanatufanya tusiwe na raha. Mtu mwenye tatizo hilo hilo anapoanza kutukosoa, tunakasirika – ingawa tungekuwa bora zaidi pasipo uwepo wa tatizo la dhambi.)
a.                   Mara zote nimekuwa nikidhani kwamba mtu mwenye uzoefu na dhambi fulani yuko kwenye nafasi nzuri zaidi kuwashauri watu wengine kuhusu dhambi hiyo. Je, hiyo ni kweli? (Nadhani hiki ndicho kinachomaanishwa na kauli ya “ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi.” Ikiwa, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, umeshinda tatizo kubwa la dhambi, unaweza kuona suluhisho “kwa wazi zaidi.”)
2.                  Je, mambo yote haya yanahusianaje na umoja? (Kuwakosoa watu wengine juu ya dhambi zile zile maishani mwako husababisha ugomvi/migongano na mgawanyiko. Kumsaidia mtu ili ashinde dhambi uliyoishinda huleta mbaraka.)
a.                   Je, hiyo inapaswa kuwa kanuni kanisani – wale tu waliotaabika na kupambana na dhambi ndio wanaoweza kutoa maoni kwenye dhambi hiyo kwa watu wengine?
D.                Soma Mathayo 7:6. Je, Yesu amebadili mada?
1.                  Ikiwa tupo kwenye mada hiyo hiyo, je, lulu za dhati ni zipi? (Ushauri wako uliojengwa kwenye uzoefu wako mwenyewe. Mjadala wako kuhusu jinsi ulivyotawaliwa na dhambi katika eneo hilo. Mbwa na nguruwe hawatanufaika na ufunuo wako wa dhati wa matatizo ya zamani, matatizo hayo “yatakugeuza na kukuvunja vipandevipande.”)
IV.             Kuziba Pancha
A.                Soma Mathayo 5:23-24. Je, watu hawa wanafanya nini mara wanapokumbuka kutokuelewana na mtu fulani? (Wapo madhabahuni – ikimaanisha kwamba wana mwenendo mzuri na Mungu. Mara kwa mara, kuenenda vizuri na Mungu huhusisha dhambi inayoleta athari chanya kwa watu wengine. Katika hali ya kawaida utakuwa ukimfikiria mtu huyu wakati ulipokuwa ukitubu dhambi yako kwa Mungu.)
1.                  Je, tunamzungumzia mtu ambaye amekukosea? (Hapana. “Ndugu yako ana neno juu yako.”)
2.                  Je, tunazungumzia halia ambayo wewe binafsi huna makosa? (Fungu halizungumzii chochote juu ya nani mwenye makosa. Linasema tu kwamba mtu fulani hana amani na wewe.)
3.                  Je, tunatakiwa kuwafanyia nini watu wenye kinyongo dhidi yetu? (Tunaendele na kutafuta suluhu.)


4.                  Nimegundua Yesu anatumia neno “ndugu.” Je, hilo ni la muhimu sana? (Soma Luka 6:22-23. Watu hawa wana jambo dhidi yako, na mara hii huu ni mbaraka. Nadhani jambo hili linarejea kwenye mjadala wa mbwa na kondoo uliopo katika Mathayo 7:6. Tatizo linapokuwa miongoni mwa washiriki unatakiwa kulifanyia kati kulitatua. Tatizo linapoibuka kwa wapagani kwa sababu wewe ni mwaminifu kwa Mungu, basi haiwezekani kujaribu kutafuta sukuhu. Nguruwe wa kipagani watakugeukia na kukuganyagia chini.)
B.                 Rafiki, je, upo kanisani na kanisa lako lina umoja? Kanisa ni chombo muhimu cha Mungu cha kuiendeleza injili. Endapo wewe au kanisa lako mnapitia uzoefu wa gurudumu lenye pancha inapokuja kwenye suala la umoja, je, utajitoa leo kujaribu kurejesha umoja?

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...