Saturday, September 20, 2014

Yanga yashikwa shati na mtibwa leo
TIMU ya Yanga jana ilishindwa kufurukuta mbele ya Mtibwa Sugar

baada ya kuchapwa mabao 2-0, katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi

Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini

hapa.

Mpira ulianza kwa timu zote kushambuliana, ambapo Yanga ndio

waliokuwa wa kwanza kufika katika lango la Mtibwa dakika ya

kwanza kabisa baada ya Genilson Santana Santos ‘Jaja’ kupiga

shuti kali nje ya 18 lakini mpira ukapaa juu.

Dakika ya tisa Mtibwa Sugar walifanya shambulizi la kustukiza,

ambapo beiki wao Andrew Vicent alipiga shuti lakini kipa wa

Yanga aliliona na kudaka.

Dakika ya 16 Mtibwa walipata bao la kwanza kupitia kwa

mshambuliaji wa zamani wa Simba Mussa Hassan 'Mgosi' baada ya

kupigwa pasi ndefu na Ali Shomari, baada ya bao hilo nyuki

wakavamia uwanjani hali iliyowalazimu wachezaji pande zote mbili

kulala uwanjani kwa sekunde kadhaa.

Dakika ya 31 Yanga wanakosa bao la wazi kupitia kwa Jaja baada

ya Haruna Niyonzima kupiga mpira wa kona na kumkuta Jaja ambaye

alipiga mpira wa kichwa lakini kipa wa Mtibwa akaokoa.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Mtibwa walikuwa wakiongoza

bao 1-0, katika kipindi hiki timu zote zilikuwa zikishambuliana

kwa zamu na kosa kosa za hapa na pale.

Kipindi cha pili kilianza, huku kila timu ikitafuta bao la

ushindi.Dakika ya 46 Yanga wanakosa bao baada ya Shaaban Nditi

kunawa mpira eneo la hatari, lakini Jaja akakosa penalti hiyo.

Baada ya mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Yanga Marcio Maximo

kumtoa Kiiza na kumwingiza Simon Msuva mpira ulibadilika sana,

dakika 51 Yanga walikosa bao la wazi kupitia Nadir Haroub

Cannavaro aliyewahi mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna

Niyonzima.

Dakika ya 61 Yanga walikosa bao tena kupitia kwa Jaja akiwa

ndani ya 18 huku kipa akiwa anaufuata mpira, alipiga mpira nje.

Dakika ya 82 Mtibwa walipata bao la pili kupitia kwa Ame Ally

baada ya mabeki wa Yanga kujua aliotea, mpira ulipigwa wa pasi

ndefu.

Dakika 15 za mwisho Yanga walishambulia sana lakini bahati

haikuwa yao.

Kikosi cha Yanga: Deogratius Mushi, Juma Abdul, Oscar

Joshua/Omega Seme dk 31, Nadir Haroub 'Cannavaro, Mbuyu Twite,

Kelvin Yondan, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Khamis

Kiiza/Simon Msuva 46, Genlson Santos 'Jaja' na Mrisho Ngassa.

Mtibwa Sugar: Said Mohammed, Hassan Ramadhan, David

Luhende/Majaliwa Hassan 64, Salim Mbonde, Andrew Vicent, Shaaban

Nditi, Ally Shomari, Mzamiru Yassin, Ame Ali, Mussa Mgosi/Vicent

Barbanas dk 50, Mussa Nampaka.

Friday, September 19, 2014

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AOMBA SAPOTI YA KUANDALIWA MECHI YA KUTETEA MKANDA WAKE WA WPBF AFRICA

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AOMBA SAPOTI YA KUANDALIWA MECHI YA KUTETEA MKANDA WAKE WA WPBF AFRICA
Na Mwandishi Wetu BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' won 11 (KO 4) + lost 1 (KO 0) + drawn 0 = 12  anaeshikilia mkanda wa WPBF Africa katika uzito wa light welterweight amejitokeza hadharani na kusema kwamba mchezo wa ngumi nchini Tanzania aulipi kutokana na malipo yake ni madogo bondia huyo aliyefanikuwa kuwa bingwa baada ya kumpiga Mwansa Kabinga
 mpambano ulio fanyika  june 8 mwaka huu huko  Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia na kuibuka mshindi katika raundi ya tisa bondia huyo mwenye ndoto ya kuwa bingwa wa dunia katika miaka ya hivi karibuni


 amesema mabondia wa hapa nchini bado awajajielewa kutokana na kuto kuwepo na wafadhili wa kutosha katika mchezo wa masumbwi ila ufadhili mwingi unapelekwa katika mambo ya soka uku wakiuwacha mchezo wa masumbwi auna mwelekeo na sapoti yoyote bondia huyo alijitamba  kwa kujinasibu kuwa kwa hapa nchini akuna bondia ambaye anaweza kumbabaisha katika kipindi hiki kwani yeye kwa sasa yupo matawi ya juu bondia huyo anaefanya mazoezi katika kambi ya Ilala ananolewa na jopo la makocha likiongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'

 ameomba watu mbalimbali kujitokeza kumsaidia ili atetee mkata wake wa WPBF Africa alioupata Zambia ili awadhilishie watu kuwa uwezo alionao ni mkubwa sana katika masumbwi kingine ni wadhamini wajitokeze kumpa sapoti kwani ana uwezo wa kuwatangazia biashara mbalimbali ukizingatia yeye ni bingwa na bado kijana mdogo mwenye nia ya kufika mbali katika mchezo wa masumbwi nchini

Halamashauri kuu ya Ccmmkoa wa Dar es saklaam yatembelea daraja la kigamboni
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karrim (kushoto), wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), akitoa maelezo ya ujenzi wa mradi wa daraja la kisasa la Kigamboni kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick (wa tatu kulia), aliyefuatana na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi kutembelea mradi huo, Dar es Salaam jana. Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Bw.  Ramadhani Madabida.
Pix No. 8
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick (wa pili kushoto), akimsikiliza kwa makini Meneja Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (wa tatu kushoto), wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Ramadhani Madabida  (wa tatu kulia), akimsikiliza Mhandisi Karrim Mataka wa NSSF (wa pili kulia), wakati Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM walipotembelea mradi wa daraja la Kigamboni, Dar es Salaam jana. Meneja Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick (wa pilia kulia) aliyefuatana na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), walifika kukagua maendeleo ya mradi wa daraja la kisasa la Kigamboni, Dar es Salaam jana. Wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa, Bw. Ramadhani Madabida.

Halmashauri kuu ya ccm Dar es Salaam yatembelea mradi wa gesi wa kinyereziKatibu mkuu wa wa Wizara ya Nishati na Madini , Eliakim Maswi, akiwaonyesha wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi na Kamati ya ulinzi na usalama namna mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi jinsi itakavyofanya  kazi Pembeni ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam. Picha na Humphrey Shao.
njiani kuelekea moro wadau

Tuesday, September 16, 2014

OPENING OF THE EU INFO POINT

 Mnufaika na na mfuko wa kusomeshwa na umoja wa ula Geline Fuko, akizungumza  na watanzania wakati wa uzinduzi wa kituo cha habari na maktaba kwa wanfunzi mbalimbali katika kituo cha Aliance,Francai's. Picha na Humphrey Shao


 Head of Cooperate Eu Tanzania  , Eric Beaume
 mnufaika na na mfuko wa kusomeshwa na umoja wa ula Geline Fuko, akizungumza  na watanzania wakati wa uzinduzi wa kituo cha habari na maktaba kwa wanfunzi mbalimbali katika kituo cha Aliance,Francai's. Picha na Humphrey Shao

  
afisa mipango, maendeleo ya miradi ya mawasiliano, Kulthum Maabad akiwa na mmoja wa watu waliotembela kituo hicho
The Delegation of the European Union (EU) to Tanzania and the EDF National Authorising Office (NAO) have launched EU Info Point with a focus on development cooperation. This will serve notably to showcase EU funded programmes, including those supported by EU Member States. Partners such as Government agencies, Non-Governmental Organisations or Decentralised Authorities will be put forward.  

Voda com Tanzania yaanzisha huduma mpya ya lipa kwanza

 zaidi ya wafanya biashara na mawakala 24 000 wamejiunga na huduma hiyo ya lipa na M-Pesa kama Chaibora na Serengeti Breweries hivyo sasa wafanya biashara wataweza kuweka fedha kiasi cha Sh 50 milioni kwenye akaunti zao za M-PesaMonday, September 15, 2014

Jaja alivyoitesa Azam Fc ngao ya hisani
KAMATI YA SHERIA YAPITISHA USAJILI

Release No. 149
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 15, 2014


KAMATI YA SHERIA YAPITISHA USAJILI
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imepitisha usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza huku wenye kasoro ndogondogo klabu zao zikitakiwa kuziondoa ili waweze kupatia leseni za kucheza ligi msimu huu wa 2014/2015.

Kasoro hizo ni kufikia makubaliano na klabu ambazo wachezaji husika wametoka, kuwafanyia uhamisho (transfer) na kulipa ada za uhamisho. Kamati vilevile ilibaini wachezaji wengi hawakufanyiwa uhamisho kama kanuni za ligi hizo zinavyoelekeza.

Hivyo, klabu ambazo hazitakuwa zimeondoa kasoro hizo kwa wachezaji wao leseni zao zitazuiliwa mpaka watakapokuwa wamekamilisha kila kitu. Ni wachezaji wenye leseni tu ndiyo watakaoruhusiwa kucheza mechi za ligi.

Klabu za African Lyon, African Sports, Ashanti United, Coastal Union, Kiluvya United, Majimaji, Mji Mkuu, Polisi Dodoma, Polisi Morogoro, Red Coast na Stand United ziliwawekea pingamizi wachezaji mbalimbali kwa kutofanyiwa uhamisho.

Kuhusu Ike Bright Obina wa Nigeria aliyewekewa pingamizi na African Lyon dhidi ya Coastal Union, Kamati imezitaka klabu hizo kufikia makubaliano, na zikishindwa mchezaji huyo atabaki African Lyon.

Kamati vilevile ilijadili malalamiko ya Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic dhidi ya klabu hiyo, na kuzipa pande hizo mbili siku 14 kufikia muafaka juu ya malalamiko hayo, na zikishindwa ndipo zirejee tena mbele ya Kamati.

Logarusic aliyewakilishwa na mwanasheria wake Dickson Sanga anailalamikia klabu hiyo kwa kuvunja mkataba kinyume cha taratibu, hivyo kutaka Simba imlipe dola 6,000 kwa kuvunja mkataba, na pia kulipa dola 50,000 ikiwa ni fidia maalumu ya madhara yaliyotokana na uvunjwaji huo.

BONIFACE WAMBURA
KNY KATIBU MKUU
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

TASISI YA HUMANITY ACTION FOR CHILDREN FOUNDATION YATOA VIFAA KWA WALEMAVU

 Mwanzilishi wa Tasisi ya Humanity  Action For Children Foundation , Rahma Mohamed Abdalah akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa ...