MSANII wa Kimarekani anayejulikana kwa jina la
Clifford Joseph ‘TI’, anatarajiwa kufanya shoo ya pamoja na wasanii 16 wa Tanzania
katika fainali za tamasha la Serengeti Fiesta zinazotarajiwa kufanyika Oktoba
18, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, meneja
masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), ambao ndiyo wadhamini wakuu, Ephrahim
Mafuru alisema ilichukua muda mrefu msanii huyo kukubali kuja nchini baada ya
kusikia kuwa Bara la Afrika limeandamwa na ugonjwa wa ebola.
Mafuru alisema wahusika waliotumwa kufuatilia ujio
wa msanii huyo, walilazimika kumuelewesha vizuri juu ya ugonjwa huo na kumtajia
baadhi ya nchi ambazo umefika.
“Tumeshukuru makubaliano na msanii huyu yalifanyika
vizuri na amekubali itakuwa mara yake ya kwanza kuja Afrika, matarajio yetu
wasanii wa Tanzania watajifunza vitu mbalimbali kutoka kwake, mbali na huyo
wapo wasanii wengine kutoka nchi za jirani
ambao watakuwepo,” alisema Mafuru.
Wakati huo huo msimamizi mkuu wa tamasha hilo, Ruge
Mutahaba alisema mwaka huu yamefanyika mabadiliko kwa kupunguza idadi ya
wasanii wa Tanzania, ambapo badala ya 40 kama mwaka jana watakuwa 16.