Tuesday, November 4, 2014

Warepublican wachukuwa udhibiti wa bunge la Marekani

Warepublican wameweza kunyakua kiti cha sita cha Baraza la Senet na hivyo kuchukua udhibiti wa bunge kamili baada ya kuongeza wingi wao katika Baraza la Wawakilishi.
Wademocrats walikuwa na viti 55 katika Baraza la Senet, lakini Warepublican waliwapokonya viti sita, kwa kushinda katika majimbo ya Arkansa, Colarado, Montana, Carolina ya Kaskazini, Dakota ya Kusini na Virginia ya Magharibi.
Wanachama wa chama hicho wanasherekea katika kila pembe ya nchi baada ya kupata ushindi mkubwa wa bunge pamoja na ushindi muhimu katika uchaguzi wa magavana, mabunge ya majimbo na serikali za mitaa.
Wachambuzi wengi wanasema wademocrats wameshindwa kutokana na kwamba Wamarekani hawaridhiki na sera za ndani na nje za Rais Barack Obama, na wagombea wake wengi hawakutaka kujihusisha na mafanikiyo yake.
Rais Obama hivi sasa hana budi bali kufanya kazi na chama cha upinzani kuweza kukamilisha sera zake za mwisho wa muhula, na wachambuzi wanasema hivi sasa anaweza kuonesha kwamba anaweza kuliongoza taifa hili baada ya kushambuliwa kutoonesha uwongozi ulohitajika.

Ukawa wanasa Waraka wa ikulu Juu ya Kampeni kupitisha katiba inayopendekezwa
UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umeweka wazi kuwa imenasa waraka wa Ofisi ya Rais Ikulu unaoonyesha Serikali imetenga Sh bilioni 2.5 kwa ajili ya kampeni za vyombo vya habari kuwashawishi wananchi kupigia kura katiba nayopendekezwa.
   
Akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa Ukawa ambaye pia ni Katibu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alidai Dar es Salaam jana  kuwa kampeni hiyo itafanywa kupitia vyombo vya habari  kuwahamasisha wananchi waweze kupiga kura ya ndiyo na kuipitisha kwa urahisi Katiba inayopendekezwa.
Waraka huo alidai kwamba unatoka Ikulu kwenda kwa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo na kuelekeza kazi hiyo inatakiwa kuanza wiki hii zikipatikana Sh milioni 50 za kuanzia.
“Ofisi ya Rais Ikulu imetenga Sh bilioni 2.5 kwa ajili ya kuhamasisha wananchi waweze kuipigia kura ya ndiyo Katiba pendekezwa.
“Lengo ni kutaka kuipitisha Katiba hiyo bila ya kuwaelimisha wananchi jambo ambalo ni kinyume na sheria,” alisema Dk. Slaa.
Alisema suala hilo ni kinyume na sheria kwa sababu  wanaohusika na utangazaji au uhamasishaji wa Katiba mpya ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na siyo Ofisi ya Rais Ikulu.
Alidai ofisi hiyo imeandaa Kamati ya Kudumu ya Habari ya kusimamia mpango wa kuelimisha umma hadi muda wa kura ya maoni.

VYOMBO VYA HABARI
Dk. Slaa alidai baadhi ya vyombo vya habari vimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo zikiwamo redio,   magazeti, mitandao ya jamii na televisheni mbalimbali   kuhakikisha mpango huo unafanikiwa.
Alidai wahariri wa vyombo hivyo wametengewa fedha kuhakikisha wanatumia vyombo vyao kutenga vipindi vya kutoa elimu kwa wananchi juu ya suala hilo.
Dk. Slaa alidai vipindi hivyo vitaongozwa na baadhi ya watu walioandaliwa kufanya kazi hiyo wakiwamo wasomi kutoka vyuo vikuu nchini; baadhi yao ni wale waliokuwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.

WASOMI
Dk. Slaa alidai  wasomi hao watalipwa Sh 500,000 kwa kila kipindi watakachoshiriki katika muda wa wiki 22  kuhakikisha suala hilo linafanikiwa.
“Wameamua kuwachukua baadhi ya wasomi kutoka vyuo vikuu, tena baadhi yao walikuwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuendesha vipindi hivyo  kwenye media mbalimbali nchini,” alisema.

NGOMA, VIKUNDI VYA UTAMADUNI  
Dk. Slaa alidai katika kampeni hiyo pia zitatumiwa    ngoma na vikundi vya utamaduni vya asili wakiwamo   maofisa utamaduni wa maeneo mbalimbalia kwa ajili ya kuvikusanya pamoja vikundi hivyo.  
Njia nyingine alizitaja kuwa ni kubandika mabango katika miji mikuu ya mikoa kuongeza uelewa wa Katiba inayopendekezwa ili wananchi waipigie kura ya ndiyo.
 Alipotafutwa kwa simu kuzungumzia madai hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu, Salva  Rweyemamu alisema; “nitakupigia baadaye”.
Hata hivyo hakuweza kupiga na alipotafutwa mara kadhaa baadaye simu yake haikupatikana hadi tunakwenda mtamboni.
Mwisho


wamarekani-wapiga-kura-uchaguzi-wa-kati-kati-ya-awamu

Wapiga kura kote Marekani wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa kati kati ya awamu ambao utaamua kama wa-Democrat au wa-Republican wanadhibiti baraza la seneti katika muda wa miaka miwili uliobaki madarakani kwa Rais Barack Obama.
Viti vyote 435 katika baraza la wawakilishi na theluthi moja ya viti 100 vya baraza la seneti  vinagombaniwa. Lengo kuu ni baraza la seneti,  ambapo wachambuzi wengi wa kisiasa wanasema wa-Republican wanaelekea kushinda viti sita muhimu ili kuweza kudhibiti baraza hilo kutoka chama cha Democrat cha bwana Obama ambacho kinashikilia wingi wa viti 55.
Huku kiwango cha utendaji kazi cha rais kikiwa kimeshuka mpaka asilimia 40 fursa nzuri  ya chama cha Republican ni viti kadhaa ambavyo bwana Obama alivipoteza miaka miwili iliyopita wakati wa kampeni yake ya kuchaguliwa tena.
Wa-Republican wanatarajia kuendelea kushikilia na pengine  kujiongezea viti zaidi katika bunge.
Ukusanyaji  maoni wa hivi karibuni unaonyesha kwamba wagombea wa chama cha Republican watashinda kirahisi katika kinyang’anyiro cha seneti huko West Virginia, South Dakota na Montana majimbo ambayo hivi sasa yanashikiliwa na wa-Democrat.  Maoni hayo  pia yanaonyesha kuwa wa-Republican pia wanatarajiwa  kushinda kinyang’anyiro cha seneti katika majimbo ya Iowa, Colorado na Alaska japokuwa huenda ikachukua saa kadhaa au hata siku kabla ya matokeo rasmi kujulikana.
Vinyang’anyiro viwili huko kusini, Georgia na Louisiana wamefungana na watahitajika kufanya uchaguzi wa marudio.

  Milka Kakete Mtanzania aliyetwaa tuzo katika mashindano ya muziki wa Injili

  Muziki ni moja ya sehemu kubwa ya maisha ya vijana duniani ukiwa ni wa kidini au wa kidunia katika jukwaa la Vijana tumezungumza na mwanamzuiki wa Injili Milka Kakete ambaye alijipatia ushindi katika mashindano ya kimataifa ya muziki wa Injili yaliofanyika katika jiji la Maryland na  Milka Kakete  ambaye ni Mtanzania anayeishi Canada aliibuka mshindi katika mashindno yaliojumuisha wanamuziki wa Injili kutoka nchi mbali mbali za Afrika.

  Al- Shabab yatishia Burundi

  Marekani imewaonya raia wake wasiende Burundi na kuwashauri wafanyakazi wa serikali ya Marekani walioko nchini humo kuchukua tahadhari haswa nyakati za usiku.
  Wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia imewaonya raia wote wa Marekani wasiende Burundi, ila kwa shughuli muhimu sana, ikisema kuwa kuna vitisho vya mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Somalia-al Shabab, pamoja na uhalifu wa hali ya juu ndani ya taifa hilo maskini.
  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kundi la al-Shabab limetishia kufanya mashambulizi ya kigaidi ndani ya Burundi na huenda likalenga maslahi ya Marekani.
  Onyo hilo linaonya Wamarekani walioko Burundi wasitumie barabara kuu kuanzia jioni hadi alfajiri. Inasema magenge yenye silaha huvizia magari kwenye barabara kuu zinazoingia mji mkuu Bujumbura.

  Mtu wa nne Marekani kuambukizwa Ebola

  Daktari wa new York ambaye amekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola nchini Guinea amekuwa wa mtu wa kwanza kupatikana na ugonjwa wa Ebola katika mji huo.
  Mayor wa mji Bill de Blasio alithibitisha jana huku akisema kwamba daktari Craig Spencer  ametengwa  na hakuna haja ya kuwa na wasi wasi.
   Spencer siku ya alhamisi alilijulisha shirika la hisani la madaktari wasio na  mipaka  ambako alikuwa akifanya kazi kwamba  ana homa kali  na alikuwa akijisikia kichefuchefu ikiwa ni dalili mbili za  Ebola.
  Maafisa wanatafuta yeyote  ambaye huenda alikuwa na mawasiliano  na Spencer,  ambaye amekuwa mtu wa nne kugundulika  na Ebola  katika ardhi ya Marekani na wa kwanza  huko  New York .

  AU yataka jeshi la Burkina faso kukabidihi madaraka kwa raia.


  Luteni Kanali Isaac Zida, kiongozi wa muda wa Burkina Faso akisalimiana na mabalozi, Nov. 3, 2014 huko Ouagadougou.
  Luteni Kanali Isaac Zida, kiongozi wa muda wa Burkina Faso akisalimiana na mabalozi, Nov. 3, 2014 huko Ouagadougou
  Umoja wa Afrika umeipa jeshi la  Burkina Faso muda wa wiki mbili kurudisha madaraka kwa serikali ya mpito ya kiraia.
  Baraza la usalama na Amani la Umoja wa Afrika lilieleza jana kwamba halitaiwekea vikwazo Burkina Faso kwa sasa lakini imesema jeshi lazima likibadhi madaraka kwa serikali ya kiraia au la sivyo kukiona.
  Rais wa muda mrefu wa Burkina Faso Blaise Compaore alijiuzulu Ijumaa baada ya maandamano ya ghasia kupinga juhudi zake za   kujaribu kuongeza  muda wa utawala wake uliodumu kwa miaka 27 kwa kubadili katiba.
  Jeshi lilichukua udhibiti wa nchi na kumteuwa Luteni kanali Isaac Zida kama rais wa muda. Vyombo vya habari vinamnukuu kwamba atakabidhi madaraka kwa baraza la mpito litakaloongozwa na kiongozi atakayeteuliwa kwa maridhiano, lakini hakusema lini hilo litafanyika.

  Pauni Mil12 zachangwa UK dhidi ya Ebola

  Kiasi cha pauni milioni 12 kimechangishwa nchini Uingereza ikiwa ni ombi kutoka kamati ya kupambana na maafa kuwasaidia watu waliokumbwa na Ebola Afrika Magharibi, michango hiyo ilichangwa kwa njia ya mitandao, simu na mchango wa serikali ya Uingereza.
  Kiasi hiki cha fedha kimechangwa baada ya siku sita tangu ombi lilipotolewa na Idara hiyo,taarifa ya idara hiyo imeeleza hii leo.
  Mkuu wa idara hiyo Saleh Saeed amesema wametiwa moyo mno na namna ambavyo Uma wa Uingereza ulivyojitolea kwa nia ya kuwezesha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi na kuwashukuru kila mmoja aliyejitolea.
  Idara za kupambana na maafa zinatoa mchango mkubwa Afrika Magharibi, ambapo mpaka sasa zimeshawasaidia watu milioni mbili na nusu walioathiriwa na Ebola ikiwemo kuwapa taarifa kupitia Kampeni za kutoa taarifa kuhusu ugonjwa huu.
  idara za kupambana na maafa zimekua zikifika katika baadhi ya nchi zilizoathiriwa zaidi na Ebola na pia katika maeneo ya ndani yasiyofikiwa kwa urahisi ya nchini Sierra Leone na Liberia.
  Mpaka sasa takriban watu 5,000 wamepoteza maisha na zaidi ya Watu 13,000 wanaugua ugonjwa huu, lakini wataalam wanasema takwimu hizi huenda zikawa kubwa zaidi kutokana kutotolewa taarifa za mara kwa mara.
  Pauni milioni 12 zilizochangwa zinajumuisha Pauni milioni 5 zilizotolewa na Serikali ya Uingereza

  Chanzo BBC SWAHILI

  UNHCR yahamasisha wakimbizi kutambuliwa

  Shirika la Wakimbizi duniani linaanzisha kampeni ya kumaliza hali ya kuwepo kwa watu wasio na makazi yani wasio na uraia na pasi za kusafiria.
  Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kuna takriban watu milioni kumi duniani ambao hawapati huduma za afya, elimu na hata haki za kisiasa wakiwemo watoto wanaozaliwa kwenye kambi za wakimbizi na hata makundi ya watu wanaonyanyaswa.
  Kamishna Mkuu wa Shirika hilo Antonio Guterres ametoa wito kwa Serikali mbalimbali duniani kutoa uraia kwa Watoto wasio na makazi wanaozaliwa katika maeneo ya mipaka yao.

  Chanzo BBC

  Sunday, November 2, 2014

  Warioba adhalilishwa mdahalo wa Katiba

  Warioba adhalilishwa mdahalo wa Katiba

  Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba akisaidiwa kutolewa katika vurugu
  Katika mazingira ya kutatanisha, siku ya Jumapili vurugu zimekatisha mdahalo uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa.
  Mdahalo huo uliokuwa ukitangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni ulivurugika kutokana na kundi la vijana wapatao 20 kuanza kumzomea aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha mada yake.
  Vijana hao ambao haijajulikana walitokea wapi au walikuwa na ajenda gani waliinua mabango ya kupinga msimamo wa waliokuwa wakiendesha mdahalo na kusema rasimu ya katiba iliyopendekezwa inakidhi mahitaji yote na kusema hakuna haja ya mdahalo.
  Jaji Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania alifanikiwa kutoka nje ya ukumbi ulipokuwa ukifanyika mdahalo huo mjini Dar Es Salaam, lakini wapo watu waliojeruhiwa kutokana na kurushwa viti na vitu vingine.
  BBC iliwasiliana na Jaji Warioba apate kueleza yaliyotokea na kama yuko salama baada ya vurugu hizo, lakini aliomba radhi kwa kusema hayupo tayari kulizungumzia swala hilo.
  Kiongozi wa kitengo cha hamasa umoja wa vijana CCM (UVCCM), Paul Makonda, aliyekuwepo ukumbini alidaiwa kuhusika na vurugu. Lakini alipoulizwa na BBC kujibu tuhuma hizo Bw Makonda amekanusha kuhusika nazo huku akisema kwamba alihudhuria mdahalo kwasababu ulikuwa wazi kwa kila mtu.
  Wakati wa vikao vya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, Makonda aliwahi kutoa kauli za kumkebehi Jaji Warioba ambaye tume yake iliandaa rasimu ya iliyokuwa ikijadiliwa na bunge hilo.
  Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, aliieleza BBC kuwa hana maelezo ya kutosha na kwamba atalizungumzia akipata taarifa rasmi ya kiofisi.
  Tanzania ipo katika mchakato wa kupata katiba mpya. Rasimu iliyodaliwa na kupitishwa na bunge lililosusiwa na vyama vya upinzani inatarajiwa kupigiwa kura na wananchi mwezi Aprili, 2015.
  Wachambuzi wa maswala ya kisiasa wameeleza wasi wasi kuwa endapo hakutakuwa na kuvumiliana hali ya kisiasa nchini humo inaweza kubadilika na kuleta ghasia ambazo zinaweza kuepukika.

  TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

  CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...