Friday, November 21, 2014

Pindi chana asema serikali itapigania haki za watoto

 Eric Baume, head of cooperation to European Union,TanzaniaNa Humphrey Shao , Dar es Salaam
SERIKALI imetangaza kuendelea kudhibiti baadhi ya watu wasio waadilifu ambao wamekuwa na tabia ya kusafirisha watoto ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kuwatumikisha kazi za majumbani.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Pindi Chana kwenye mkutano wa kujadili miaka 25 ya mkataba wa Haki za Watoto  Duniani.


Alisema ili kudhibitisha hilo katiba mpya inayotarajiwa kupigiwa kura ya maoni ya kuikubali au kuitakaa kuna ibara ya 53 inayozungumzia haki ya watoto ikiwamo ya kupata elimu, kupinga ukatili na kupata huduma za afya. Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Pindi Chana kwenye mkutano wa kujadili miaka 25 ya mkataba wa Haki za Watoto  Duniani.


“Serikali iliungana na mataifa mbalimbali Duniani ili kuridhia haki ya mtoto kulindwa, kupata elimu, afya na kuondoa ukatili wa jinsia.

“Ili kutekeleza hilo, katiba mpya ibara ya 53 inazungumzia haki ya watoto kwa ujumla, hivyo basi mtu atakayebainika anakwenda kinyume na haki hizo serikali itamchukulia hatua za kisheria,”alisema Chana.
Aliongeza kutokana na hali hiyo serikali imejipanga kuhakikisha kuwa inazuia biashara haramu ya watoto  pamoja na kudhibiti vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakisafirisha binadamu wenzao kama wanyama katika nchi za Magharibi.
“ mkakati wa serikali ni kuhakikisha kuwa inashirikiana na wadau mbalimbali ili kufanikisha mipango na kuhakikisha kuwa haki ya mtoto inalindwa kuanzia nyumbani hadi katika jamii hili kupata kizazi ambacho kitakuwa na uadilifu na weredi”.

Wednesday, November 19, 2014

Binti ajinasua na ndoa ya wana mgambo

Mwanamke mmoja raia wa Uholanzi amewasili nchini Uturuki baada ya safari iliyojaa hatari nchini Syria kwa ajili ya kumchukua binti yake aliyekua mjini Raqqa, mji unaokaliwa na waasi wa Islamic State.
Monique alikwenda Uturuki mara ya kwanza baada ya binti yake aitwae Aicha kusafiri kwenda Syria kuoana na mmoja wa wanamgambo wa kundi hilo mwenye asili ya Uholanzi na Uturuki.
Mamia ya Wanamgambo wenye asili ya Ulaya wamekua wakienda Syria kupigana ndani ya kundi la IS.
Aicha ,19 ni miongoni mwa Wasichana ambao walisafiri kujiunga na IS.Raia wawili wa Austria wenye umri wa miaka 15 na 17 walikwenda Syria Mwezi Aprili na mmoja wao aliripotiwa kuuawa.
Aicha aliondoka Uholanzi mwezi Februari, akaolewa na Omar Yilmaz, mwanamgambo mwenye asili ya Uturuki na Uholanzi ambaye alishawahi kuwa mwanajeshi nchini Uholanzi,alitumia mbinu alizopatiwa akiwa mwanajeshi na kuwafunza wapiganaji wenzake.
Monique amesema mwanae alibadilika ghafla kutoka binti aliyefahamika vyema na kuwa Msichana mwenye msimamo mkali.
Wapiganaji wa Islamic State wakifanya mashambulizi
Baada ya Polisi kumuonya Aicha kutosafiri kwenda Syria walikamata Pasi yake ya kusafiria, Aicha hakuvunjika moyo alitumia kitambulisho chake.
Aicha alikuwa akiwasiliana na Yilmaz kwa njia ya mtandao wa kijamii kisha wakapendana.
Monique alisafiri mpaka Uturuki mwezi Oktoba ili kumchukua mtoto wake lakini alishindwa kuvuka mpaka.
Lakini wiki iliyopita, baada ya Aicha kuomba msaada alirudi tena nchini Syria ingawa Polisi walimkataza kufanya hivyo.Monique alifika Raqqa nchini humo na kumchukua bintiye kisha kurejea Uturuki
Yilmaz, Mume wa Aicha anamtaja mkewe kuwa mtalaka wake kwenye anuani yake ya Tweeter.
Hivi sasa Mama na mwana wanashikiliwa mpakani mwa Uturuki, wakisubiri ruhusa ya kurudi Uholanzi.
Serikali ya Uholanzi imeiambia BBC kuwa inawasiliana na Monique lakini haijatoa ufafanuzi zaidi, tatizo ni kuwa Aicha hana Pasi ya kusafiria ingawa mwanasheria wake anasema huenda wakarejea Uholanzi ndani ya wiki moja.

Innocent Mnyuku kuagwa ijumaa Hospitali ya Lugalo


Aliyekuwa mhariri mkuu wa jarida la umoja linalochapishwa na kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Innocent Mnyuku ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo anataraji kusafrshwa siku ya ijumaa na kupelekwa kijini kwao amzimbu Morogoro kw ajaili ya Maziko.

Kwa mujibu taharifa alizopata bloger wetu kutoka chanzo kinachoaminika ndani ya New Habari zinasema kuwa taratibu zote za mazishi zinafanywa katika ofisi ya New Habari na mpango wa kumsafirisha kwenda morogoro na kusema kuwa  mwili huo wa marehemu ambao uemhifandhiwa katika hospitali ya lugalo ambako heshima za mwisho zitafanyika katika hospitali hiyo siku ya ijumaa

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...