Wednesday, February 25, 2015

AMIN SALMINI AAHIDI KUIBORESHA OFISI YA SERIKALI YA MTAA KATA YA TABATA, WAKIFANYA SHEREHE YA KUWASHUKURU WAPIGA KURA WAO

 Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akimkabidhi Cheti, Mwenyekiti wa UWT ambaye pia ni Kaimu Katibu wa CCM wa Tabata Relini, Shahani Mtwawa, wakati wa Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake mgeni rasmi huyo, aliahidi kuiboresha Ofisi hiyo ya Serikali ya Mtaa wa Tabata kwa kununua Fenicha za ofisi zisizopungua gharama ya Sh. M 1.5.
 Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akimkabidhi Vifaa vya michezo (Jezi na Mpira)  Katibu Mwenezi wa Kata ya Tabata Relini, Ramadhan Mazongera,  wakati wa Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam.
Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya tano Zanzibar, Amin Salmin, akikabidhi Meza na Viti, kwa  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tabata, Elisante Msangi (kulia)  wakati wa Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam.

 Wasanii wa kundi la Segere wakiimba wakati wakitoa burudani katika Sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru Wapiga Kura wa CCM, waliofanikisha kuchaguliwa kwa Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wa Kata ya Tabata. Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Serikali ya Mtaa Kata ya Tabata, jijini Dar es Salaam
Sehemu ya Kinamama waliojitokeza kwenye sherehe hiyo

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...