Friday, February 27, 2015

MABONDIA WAPIMA UZITO KUZIPIGA FEB 28 UWANJA WA NDANI WA TAIFA JUMAMOSI


Mabondia Mwinyi Mzengela kushoto na Shomari Milundi wakitunishiana misuri baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao jumamosi ya kesho feb 28 utakaofanyika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Fadhili Majiha akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Francis Miyeyusho utakaofanyika Feb 28 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Epson John wa Morogoro kushoto akitunishiana misuli na Vicent Mbilinyi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho utakaofanyika katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa katikati ni mratibu Antony Rutta Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Cosmas Cheka kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O Africa utakaofanyika jumamosi ya feb 28 uwanja wa ndani wa taifa picha na SUPER D BOXING NEWS
 BONDIA IBRAHIMU  CLASS 'KING CLASS MAWE' AKIPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WAKE WA UBINGWA WA U.B.O AFRICA
 BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO CHICHI MAWE AKIPIMA UZITO
Bondia Cosmas Cheka kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O Africa utakaofanyika jumamosi ya feb 28 uwanja wa ndani wa taifa picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Cosmas Cheka wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa raundi kumi kugombania ubingwa wa U.B.O Africa utakaofanyika jumamosi hii katika uwanja wa ndani wa taifa
mpambano huo mkali utatanguliwa na ngumi kali kutoka kwa bondia Fransic Miyeyusho atakaezipiga na Fadhili Majiha mpambano wa raundi nane mpambano mwingine wa ubingwa ni kati ya Alibaba Ramadhani na Jacobo Maganga na katika kusindikiza mapambano hayo makali bondia machachari na chipkizi Vicent Mbilinyi ataoneshana umwamba na Epson John wa Morogoro na Shomari Milundi atapambana na Mwinyi Mzengela huku Husein Mbonde atakabiliana na Shedrack Ignas katika kuhakikisha mpambano huo unakuwa wa kihistoria na kuacha gumzo nchini bondia Said Mundi wa Tanga atapambana na Ramadhani Shauli na mapambano mengine mbalimbali

mpambano huo unaosimamiwa na P.S.T chini ya rais wake Emanuel Mlundwa yamekuwa gumzo mjini na kusababisha taflani za mabondia kutaka kupigana kavukavu uku makocha wao pia wakikunjiana ngumi

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...