Tuesday, March 10, 2015

Barthez aiangukia Yanga
Na Humphrey Shao, Dar es Salaam
KIPA wa Yanga, Ally Mustapher ‘Barthez’ amewaomba radhi mashabiki, wapenzi na viongozi wa timu hiyo kutokana na kipigo cha bao 1-0 walichokipata Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya mahasimu wao Simba.

mara baada ya mchezo huo Barthez alisema hakutarajia kupata matokeo hayo na kitendo cha kutangulia kufungwa kulionekana kuwaondoa mchezoni karibu wachezaji wote na kuanza kucheza kwa kukamiana.
“Binafasi nawaomba radhi mashabiki, viongozi na wapenzi wa Yanga kwa kufungwa bao hilo kwani hayakuwa matarajio yetu kupoteza mchezo ukizingatia kwa sasa tupo katika kiwango kizuri hivyo kila mmoja alikuja uwanjani akitarajia kuona tunawafunga watani zetu lakini hali imekuwa tofauti, alisema Barthe huku akitokwa na machozi.

Katika mchezo wa Jumapili Simba iliendeleza ubabe kwa mahasimu wao Yanga ambao ndiyo vinara wa Ligi Kuu Tanzania bara wakiwa wamecheza michezo 16 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi na wana pointi 31 wakifuatiwa na mabingwa watetezi Azam FC wenye pointi 30.No comments:

Post a Comment

MWAKIBINGA AONGOZA WAISLAMU KAWE KUPELEKA KILIO CHAO KWA RAIS MAGUFULI

 Mwanaharakati na Mzawa Kawe James Mwakibinga akizungumza na wakazi wa Kawe wakati walipokuwa wakitoa ombi lao kwa Rais Magufuli kupitia ...