Wednesday, March 18, 2015

Japan waitabiria makubwa Tanzania


Na ;Daniel Mwambene;Ileje              JapanBalozi wa Japan nchini Tanzania Mh;Kazuyoshi Matsunaga ameitabiria makubwa Tanzania iwapo wasomi wa  nchi hii watachukua hatua mathubuti za kitaaluma na kizalendo katika kulitoa taifa hili kwenye umaskini na kulipeleka mbele kimaendeleo.
Alitoa rai hiyo wilayani Ileje wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya  mkataba wa ujenzi wa chuo  cha VETA kati ya kaimu balozi wa Japan hapa nchini na viongozi wa serikali wilayani humo ambapo Japan itachangia  fedha za Kiatanzania  milioni 160.
Alisema kuwa Tanzania ina rasilimali nyingi ambazo wasomi wakitumia vizuri fani zao nchi hii itakwenda mbele na kuwa taifa lenye uwezo mkubwa wa kiuchumi .
Akitumia picha za mji mkuu wa Japan Tokyo alionyesha mwonekano ulivyokuwa mara baada ya vita  vya pili vya Dunia ukionekana kuharibiwa vibaya huku kukiwa hakuna miundombinu yoyote kama ville majengo na umeme.


Aliongeza kuwa walioifikisha Japan ilipo sasa kimaendeleo ni wasomi ambao walitanguliza uzalendo kwa taifa lao huku nchi hiyo ikiwa haina rasilimali kama ilivyo kwa Tanzania ambayo ina utajiri mkubwa wa madini kama vile dhahabu na almasi lakini iko nyuma kimaendeleo.

Matsunaga aliongeza kuwa,vyuo vinvyoanzishwa wahitimu wake wawe chachu ya maendeleo katika maeneo yao na taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Mh; Janet Mbene alitoa wito kwa wasomi waishio nje  ya Ileje kuwekeza wilayani  kwao kama ilivyo kwa wilaya zao.
Amesema,wilaya zingine zimesonga mbele kwasababu wasomi huwekeza makwao balala ya kukimbia na kusahau kuwa kukumbuka nyumbaniu ni uzalendo pia.
Mpaka sasa wilaya ya Ileje ina chuo cha ufundi  kimoja   tu kinachomilikiwa na kanisa la Moraviani Jimbo la Kusini.

No comments:

Post a Comment

MWENGE WA UHURU WAINGIA GAIRO NA KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA MILIONI MIASABA NA ZAIDI

 Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Morogoro Regina Chonjo mara ulipofika katika eneo la Ma...