Monday, March 23, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA ENEO LA BUGURUNI KWA MNYAMANI LILILOATHIRIKA NA MAFURIKO

 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza mkandalasi wa ujenzi wa mtaro wa kupitishia maji machafu wakati alipotembelea eneo la Buguruni kwa Mnyamani leo Machi 23, 2015 kwa ajili ya kukagua maeneo yaliyoathirika kutokana na mafuriko ya mvua zinazoendele kunyesha jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo juu ya hatua zilizokwishachukuliwa na Serikali, kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, wakati Makamu alipotembelea eneo la Buguruni Kwa Mnyamani lililoathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo hilo baada ya kujionea athari zilizotokana na mafuriko hayo kwa wakati wa Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam, leo machi 23, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiangalia mtaro wa maji machafu ambao utaunganishwa na mabomba yatakayonyonya maji yaliyotuama katika eneo hilo lililoathirika kwa mafuriko ya mvua. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

MWIJAGE MGENI RASMI KONGAMANO LA VIWANDA MNMA

Na Humphrey Shao, Globu Ya jamii Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage anataraji kufungua kongamano kuhusu Maende...