Friday, March 27, 2015

Mkuu wa wilaya ya Ileje Rozimary Sinyamule awaasa Vijana kujikita katika shughuli za Maendeleo


 


Na;Daniel  Mwambene,Ileje      Vijana

Mkuu wa wilaya ya Ileje amewataka vijana wilayani humo kuondoa tofauti zao za kisiasa badala yake wajikite katika ujenzi wa misingi ya Ileje ijayo itakayokwenda sambasamba kimaendeleo na wilaya zingine hapa nchini.


Akizungumza na vijana wa mji wa Itumba na Isongole kwa nyakati tofauti Mkuu huyo wa Wilaya Bi; Rozimary Sinyamule amesema tofauti za kisiasa kamwe zisiwe chanzo cha kuwagawa vijana kwani mahitaji yao ni ya aina moja.


Alisema malalamiko kutoka kwa vijana wa vyama vyote vya siasa hapa wilayani hayatofautiani kati yachama kimoja na chama kingine,hivyo ujana huo hauna budi kuwaunganisha katikakuipigania wilaya hiyo kimaendeleo.


Alisema  vijana wanaweza kuchukua hatua za ukombozi ikiwa ni pamoja na kuunganisha nguvu  zao katika kupigania haki zao kwa kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa katika Uchaguzi Mkuuu ujao.


Bi;Sinyamule aliongeza kuwa vijana wamekuwa wakipinga kuitwa ni taifa la kesho wakitaka waitwe taifa la leo, uchuguzi wa mwaka huu iwe njia ya kuwaingiza katika nafasi za uongozi katika ngazi ya wilaya na taifa ili kupaza sauti zao.


Vijana kwa upande wao walimwomba Mkuu huyo wa Wilaya ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi   


na usalama wa wilaya kukemea vitendo vya ubaguzi vinavyofanywa na jeshi la polisi wakati wa sherehe za Krismas na mwaka mpya ambapo jeshi hilo linatuhumiwa kuvuruga sherehe hizi katika mij wa Isongole huku vijana wa mji wa Itumba wakiachwa kuserekea.


Hii ni mara ya pili kwa uongozi wa juu kupokea kero kama hiyo kwani siku kadhaa zilizopita wakazi wakiji hicho walimweleza  Mkuu wapolisi wa Wilaya hiyo Afande Fabin Masaka juu ya kero hiyo.


Mkuu huyo wa wilaya amekuwa akifanyaziara katika maeneo mbalimbali ya wilaya yake akipokea kero na matatizo mblimbali ya wananchi  huku akiwaimiza watumishi wa serikali kutokuwa vyanzo vya kero hizoIkumbukwe kuwa katika uchuguzi wa serikali za mitaa  uliopita vyama vya upinzani wilayani humo vilijiongezea viti vya uenyekiti wa vijiji kutokakiti kimoja na kupata viti zaidi ya 20.


No comments:

Post a Comment

ROSEMARY LUHAMO KUTOKA DODOMA AKABIDHIWA MAMILIONI YAKE NA UMOJA SPESHO

 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo akiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa pesa zake kupitia Benki ya CRDB na Kampun...