Nape ashusha Pumzi kwa Lowasa



KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amempongeza Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa
Monduli Edward Lowassa kwa kukubali kuyasitisha makundi ya Watanzania wanaokwenda nyumbani kwake kumshawishi agombee
urais Oktoba 31, mwaka huu.
Lowassa anayetajwa kugombea urais mwaka huu amekuwa akipokea makundi tofauti ya wananchi nyumbani kwake Dodoma yanayokwnda kumshawishi atangaze nia pindi muda utakapowadia.
Juzi Lowassa akipokea kundi jongine LA vijana waendesha pikipiki bodaboda kutoka wilayani Mbarari mkoan Mbeya   fananisha makundi yanayokwenda kumshawishi sawa na mafuriko hivyo hawezi kuyazuia kwa mkono.
Akizungumzia uamuzi huo wa Lowassa wa kusitisha kuyapokea makundi hayo wilayani hapa Nape alimpongeza kwa kukubali kutii maagizo ya Chama pamoja na kanuni zinazokiongoza Chama hicho.
"Nampongeza Lowassa kwa kukubali kuheshimu kanuni, taratibu na Katiba ya chama ambayo ndio inatakiwa kufuatwa na kila mmoja ndani ya chama.
"Alichokuwa anafanya lowassa ni kufanya kuanza kampeni kabla ya wakati
na kwa mujibu wa chama chetu ni makosa maana anakiuka taratibu na
kanuni za chama.Hatuwezi kukaa kimya wakati kanuni zinavunjwa.hivyo
nimpongeze lowassa kwa kutii agizo la chama,"alisema nape.
Akizungumzia kuhusu wapambe wa makada wa wanaotaka urais, aliwataka  makada wote wanataka kugombea urais kupitia chama hicho wawe makini na
wapambe wao.
Nape alifafanua kuwa ni vyema makada wanaotaka kugombea urais wakawa makini na ushauri unaotolewa na washauri au wapambe wao kwani unaweza kuwasababisha kupoteza sifa ndani ya CCM.
"Nawashauri wote wanaotaka kugombea urais wasiwasikilize wapambe
kwani ushauri mwingine unaweza
kuwakosesha sifa za kugombea  nafasi ya urais,"alisema Nape na kuongeza:
"Na hili si kwa wapambe wa Lowassa tu, bali ni kwa wapambe wa makada wore ndani ya CCM,"alisema.
Akisisitiza kuhusu CCM kutenda haki Nape alisema kwamba Chama hicho kitahakikisha kinatenda haki kwa  kila anayeomba nafasi na hakuna ambaye
atanyimwa haki yake.
Alisema kwa wote ambao watakuwa makini katika kuzingatia kanuni na
taratibu za chama haki zao zitalindwa lakini wale ambao watakiuka kwa
maksudi hao hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
"Tunaendelea kuwakumbusha makada wote kuzingatia kanuni na
Katiba ya chama.Kinyume cha hapo watakuwa wanajinyima haki ya
kuomba ridhaa ya kugombea kupitia Chama cha Mapinduzi,"alisema Nape.

Post a Comment

Previous Post Next Post