Tuesday, March 10, 2015

Okwi amtia ukiziwi Niyonzima

 Emmanuel okwi akimsii niyonzima atoke uwanjani
 Niyonzima akimwambia meneja wa timu hiyo kuwa asikii


Na Humphrey Shao, Dar es Salaam

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda anayekipiga katika klabu ya Simba, Emmanuel Okwi, amemsababishia kiungo wa Yanga,Haruna Niyonzima kupata tatizo la kutosikia Filimbi ya mwamuzi  kutokana na kelele za Mashabiki.
Niyonzima ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kupiga mpira wavuni  kisha kumlalamikia mwamuzikuwa alikuwa sikii nini kinaendelea akiwa mchezo kutokana Mashabiki wa Simba walikuwa wanashangilia sana.
“kiukweli nilikuwa sisikii hiyo filimbi ya mwamuzi kwani awa mashabiki wa Simba wana kelele sana kiasi cha kunichanganya sasa sioni sababu ya mwamuzi kunipa kadi nyekundu wakati nimemweleza sikusikia kutokana na kelele za mashabiki” alisema Niyonzima.
Niyonzima altoka uwanja huku akiongea maneno ya kejeli huku akitukana matusi kwa waamuzi juu ya kile alichotendewa na mwamuzi wa kati wa mchezo huo.

mwisho


No comments:

Post a Comment

ROSEMARY LUHAMO KUTOKA DODOMA AKABIDHIWA MAMILIONI YAKE NA UMOJA SPESHO

 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo akiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa pesa zake kupitia Benki ya CRDB na Kampun...