Friday, March 20, 2015

Rose Mhando amzimia H Baba

Mwanamuziki wa Injili kutoka Tanzania Rose Muhando ameleta utata mtandaoni baada ya kutoa sifa za kuonyesha kumkubali Mwanamuziki wa Bongo Fleva H-Baba kwa kazi yake mpya Show Time,Rose Mhando alitoa sifa hizo baada

Msanii wa Bongo Fleva H Baba akiwa na Mwibaji wa nyimbo za injili Tanzania Rose Mhando.
ya kushuhudia show aliofanya H Baba na wimbo wake mpya wa Show Time.
Rose Mhando alinukuliwa akisema kuwa show aliyoiona kwa H Baba na huo wimbo wake mpya ni matata sana na kama akiendelea kutoa nyimbo kama hiyo hakika wasanii wenzake
wanatashidana sana lakini hawataweza kumfikia,lakini pia aliongeza kuwa H Baba ni msanii ambae anakuwa toka alipoanza kutoka na Mpenzi Bubu amekuwa anazidi kupanda
hata show zake ni matata sana ukilinganisha na show zingine za wasanii wa bongo fleva.
Baada ya watu kuonyesha hawajapendezwa na kitendo alichokifanya mwanamuziki huyo wa Injili kukubali nyimbo za kidunia H baba alisema kuwa Rose Mhando ni mwanamuziki
mwenzake hivyo haoni kama kuna ubaya yeye kumsifia kwani alichosifia amesifia sanaa yake na si kitu kingine hivyo hakuna tatizo lolote.

"Namkubali sana Mwanamuziki wa injili Rose Mhando kwakuongea ukweli kutoka moyoni.Naomba niulize Kwakuwa amesifiwa H.baba ndio kakosea mlitamani asifiwe nani sasa apo
ukweli utabakia Kuwa ukweli siku zote toka Mpenzi bubu,mpaka Leo nipo nijambo lakumshukuru muumba.sasa Rose ni mwanamuziki mwenzangu kunisifia nisawa tuu mbona disco
wanapiga nyimbo za Makoma kwani wale wanaimba mziki wakidunia?" Alihoji H-Baba.
"Hebu punguzeni kelele Rose Mhando amenisifia baada yakuona Show yangu wimbo nilioimba ukamvutia ni Show Time na upande wa Show pia jukwanii hilo linafahamika ila
linachengeshwa kila siku ila Mungu ananisimamia nipo mpaka leo,Mbona Alli Kiba amesifia show zangu hamjaongea kitu,hii imeingia kwenye historia ya nchi tayari.Ahsante
dada angu Rose Mhando nakukubali sanaa." Aliongeza H-Baba.

Kutokana na hili mwanamuziki wa Rap kutoka mwanza Fid Q kwa upande wake aliibuka na kusema kuwa hata yeye anaungana na mwanadada Rose Mhando kwani anamkubali sana H
Baba kwa show zake na nyimbo zake pia hali ambayo ilimfanya Fid aanze kutoa mwongozo kwa mashabiki wake ambao nao walionekana kupokea tofauti ujumbe wa Rose Mhando juu
ya kumkubali H baba na kuanza kumuhukumu kwa mambo mbalimbali na ufuatao ulikuwa ufafanuzi wa Fid Q kwa watu ambao wameweza kumjudge Rose Mhando juu ya kauli yake ya
kumkubali H baba.

"Nashukuru tumekubaliana katika suala la mwenye mamlaka ya hukumu..Joa lyimo sasa tubaki katika tafsiri ya UPENDO.. Sasa kama dada hatompenda ndugu yake anayemuona..
Atawezaje kumpenda Mungu asiyemuona? Ni ukweli tumeonywa kuhusu anasa za kidunia lakini pia tusisahau kama tunauhitaji msaada wa mwenye dhambi ili kumfukuza
shetani.Eliud Nyaulingo Lakini Kaisali ni kiumbe wa Mungu pia.. Huenda UPENDO huu alioonyeshwa ukamvutia kiasi cha yeye kurudi kundini.. Haudhani?"

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...