Tuesday, March 31, 2015

Ukosefu wa TBS Mpaka wa Kasumulu ni tatizo kwa Walaji
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara , Janeth Mbene, akizungumza na Meneja wa Mamlaka ya mapato mkoa wa Mbeya, Joseph Ruge, katika ofis za TRA Kasumulu. Picha na Humphrey ShaoNa Humphrey Shao, Kyela
MPAKA wa Kasumulu ni  moja ya mipaka ambayo inaingiza fedha nyingi katika serikali kupitia kodi ya mapato na tozo mbalimbali, mpaka huu una urefu wa kilometa 32 kutoka wilaya ya Ileje upande magharibi hadi ziwa Nyasa upande wa mashariki katika wilaya ya Kyela.
Mpaka huu ambao una vivuko visivyo rasmi vipatavyo 32 ambavyo hutumika  kuvusha bidhaa za magendo ambazo uchangia kwa kiasi kikubwa kupotea kwa mapato na bidhaa ambazo azina viwango kwa matumizi hapa nchini
Hivi karibuni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, akiwa na maofisa waandamizi wa shirika la Viwango nchini(TBS),walitembelea mpaka huo hili kujionea namna shughuli zinavyofanyika katika mpka huo.
Akiwa katika mpaka huo Waziri mbene aliweza kujionea na namna tasisi mbalimbali zinavyofanya kazi na kupata ripoti ya tasisi mama katika eneo hilo mamlaka ya mapato nchini(TRA).
Waziri Mbene alibaini kuwa licha ya kuwepo tasisi kadhaa za serikali katika eneo hilo lakini bado kuna upungufu wa kutokuwepo kwa shirika la viwango nchini(TBS) Katika eneo hilo hali inayo hatarisha maisha ya walaji wa bidhaa zianazopita katika mpaka huo licha ya kulipiwa ushuru.
Waziri mbene amelitaka shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kuakikisha kuwa wanaweka kituo cha ukaguzi katika mpaka wa Kasumulu kwa haraka katika eneo hilo kutokana na mahitaji ya mpaka huo ambao upitisha bidha akutoka nchi za Malawi na Afrika Kusini.
Mbene anasema kuwa kumekuwa na tatizo la kusambaa kwa bidhaa katika masoko ya nyanda za juu kusini ambayo yanapitishwa katika mpaka wa Kasumulu hali inayochangia kwa bidhaa za ndani kukosa masoko .
“Serikali yote iko hapa hivyo ni aibu kuona kuwa atuna kituo cha tbs katika mpaka huu kwani hii ni moja ya lango kuu la uingizaji bidhaa kwa ajili ya mikoa ya nyanda za juu kusini kutokea nchi jirani ya Malawi na Afrika kusini kama nilivyoelezwa kwenye ripoti ya TRA” alisema Waziri Mbene.
Akieleza mbele  ya naibu waziri Afisa habari wa TBS, Roida Andusamile, alisema kuwa shirika hilo lipo katika mchakato wa kuweka kituo katika kituo hicho hili kupunguza tatizo la uingizwaji wa bidhaa ambazo azikidhi viwango.
Roida anasema kuwa wao kama maofisa wa TBS wameona namna mpka huo ulivyokuwa na umuhimu wa kuwekewa kituo cha ukaguzi kama ilivyo katika bandari na vituo vingine kwani biashara ya bidhaa na vyakula ni kubwa kuliko kawaida.
Kwa upande wake Kaimu afisa mfawidhi forodha Kasumulu Delya Yohana anasema katika kipindi chote wamekuwa katika mapambano makali juu ya uingizwaji wa pombe za viroba kutoka nchini Malawi.

Anasema kuna kila sababu ya TBS kuwepo kwani bidhaa za vilelevi zimekuwa zikiingia na kulipiwa ushuru licha ya baadhi kupigwa marufuku kutokana na uwepo tasisi ya chakula na lishe ya TFDA kubaini kuwa vina kemikali mbaya.

Alitaja kuwa idadi ya magari yanayoingia katika kituo hicho kuanzia mwezi Desemba ni magari yaliyoingia ni 1389 na yaliyotoka ni 592 na thamni ya mizigo iliyokwenda nje kama export ilikuwa sh11,833,414,899.
Alitaja kuwa kudorola kwa uchumi wa Malawi kumechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa baishara katika mpaka huo ambao unategemewa kama lango kwa nchi jirani.
Alitaja kuwa mizigo inayotoka nje ya nchi na bidhaa zinazouzwa nchini Malawi ni Saruji kutoka mbeya , Sabuni,bidhaa za majumbani,Mafuta ya kupaka, Mafuta ya kupikia na Juice za Azam.

Mizigo inayoingia nchini kwa wingi ni vipuri vya Viwandani hasa vile vya kiwanda cha Sukari cha Kilombero, bidhaa zingine ni mbao kutoka nchini Malawi, Mashudu ya kulishia wanyama na Vipodozi.
Anasema kuna mpango wa kujenga kituo kimoja cha Forodha kijulikanacho kama OSBP(One stop Border Post) Katika mpaka wa Kasumulu Faida ya mradi huu ni pamoja na kupunguza muda wa kuingiza na kutoa mizigo na kudhibiti magendo ulinzi na usalama mpakani.

mwisho

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...