Friday, March 6, 2015

Ushirikina chanzo cha mauaji ya watu wenye Albinism’ – Dk. Ally Possi


EXCLUSIVE INTERVIEW: ‘
Na Andrew Chale wa modewji blog
Dk. Ally Possi ambaye ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam. Akielezea na kuchambua kwa kina kuhusiana na wimbi la mateso na mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wenye albinism.
Mo dewjiblog, iliamua kufanya mahojiano maalum ilikukuletea wewe msomaji wetu unayeperuzi mtandao wako bora kabisa kujua na kuelewa na nini kifanyike ikiwemo mimi na wewe katika kuchukua hatua.
Suala la mauaji dhidi ya watu wenye albinism:
“JAMII yenye ushirikina ndio yenye kuamini suala la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambao wana albinism, hivyo ilikuondoa imani hii potofu ni kutoa elimu katika maeneo yote na kuwalinda popote pale, Jambo hili ni jukumu letu sote” anabainisha Dk. Ally Possi.
Dkt. Possi anabainisha kuwa, Serikali itaendelea kulaumiwa mpaka hapo juhudi za dhati za kukomesha mauaji na vitendo vya kikatili vitakavyochukuliwa na kutokomezwa kabisa.
Fuatilia hapa Mahojiano hayo maalum.
MO DEWJI BLOG : Karibu, mgeni wetu katika mtandao huu wa kijamii unaokuletea habari bora kabisa zilizochambuliwa kwa kina za ndani, nje na makala maalum za kina.
DK. POSSI: Asante, nashukuru sana…
MO DEWJI BLOG: Unadhani nini chanzo na hali ya ongezeko la vitendo hivi kwa sasa hapa Tanzania?
DK.POSSI: “Kwanza mauaji ni.. yanatokana na imani potofu. Imani potofu kwa jamii kuwa ukipata kiungo cha alibino unafanikiwa.
Hii ni imani potofu kwa jamii ya watu wenye kuamini ushirikina.
“Albino ni ulemavu ambao mtu anakosa aina ya vitamin inayoitwa melaniani…
Inakosekana ikiwemo katika ngozi, nywele na macho” anaendelea kubainisha kuwa: Kuwa albinism ni hali ya kurithi kutoka kwa wazazi wote wawili ama mmoja. Ni kwamba baba na mama wanakuwa na vinasaba vinavyokuwa na albinism na vinapokutana wakati wa kutunga mtoto ndipo mtoto mwenye albinism anazaliwa.
MO DEWJI BLOG: Vipi inahusishwa na suala la Imani?
DK. POSSI: “Imani sio dini, Ni imani ya kishirikina.
“Sijui kitu gani ambacho kimetokea kikaleta hiyo imani, kwa kifupi ipo kwenye jamii iliyoendelea na uwezo wake wa kiuchumi ni mdogo na elimu pia.
Pia tunaweza kusema: “Suala hili ni la imani, Imani si ya dini, bali ni ya kishirikina. Kwa sababu kuna mtu anasema yeye muislamu ama mkristo.
Au kuna mtu ana Phd/ Profesa, ama amesoma elimu nzuri tu ama ana pesa anafanya biashara au mfanyabishara au mwanasiasa mwenye elimu yake nzuri lakini ametumbukia kwenye imani hii ya kishirikina.
Kusoma zaidi ingia http://dewjiblog.com/…/exclusive-interview-ushirikina-chan…/

No comments:

Post a Comment

Dk 30 ZA ASLAY ALIVYOWALIZA WATU ESCAPE ONE

Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii Ilikuwa siku ya feb 17 ambapo Msanii wa Muziki wa BONGO Fleva Aslay Isihaka alivyoweza kubadilisha H...