Friday, April 3, 2015

Afya ya Gwajima ya waenyesha PolisiHALI ya afya ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, imebadilika ghafla baada ya kushindwa kupanda ngazi katika ofisi za Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam jana.
Askofu Gwajima alifika kituoni hapo saa 2 asubuhi akiwa ameongozana na maaskofu zaidi ya watano.
Katika hali ya kushangaza, wakati akipanda ngazi kuelekea kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, alifanikiwa kupanda mbili, lakini alipojaribu ya tatu alishindwa.
Baada ya kushindwa kuendelea kupanda ngazi, aliwaomba wasaidizi wake wamrudishe kwenye gari lake.
Alipandishwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T 631 AHD.
Akizungumzia tukio hilo, mwanasheria wake John Mallya alisema baada ya hali ya Askofu Gwajima kuonekana si shwari, alikwenda kuripoti kwa mkuu wa upelelezi.
Mallya alisema baada ya kutoa taarifa hiyo, aliruhusiwa kurudi nyumbani.
Alisema Askofu Gwajima anatakiwa kuripoti tena Aprili 20 kwa ajili ya kuhojiwa.
“Askofu Gwajima ameruhusiwa kurudi nyumbani kwa ajili ya mapumziko hadi afya yake itakapoimarika, tumeambiwa arudi kuripoti Aprili 20,” alisema Mallya.
Akizungumzia tukio la kuahirishwa kutoa maelezo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Constantine Massawe, alisema Askofu Gwajima alidai hali yake si nzuri, bado ni mgonjwa.
“Askofu Gwajima amesema anaumwa… kama anajisikia vibaya tunamwacha kwanza apate nafuu, baada ya Sikukuu ya Pasaka tumemtaka arudi kituoni hapa,” alisema.

KAMANDA KOVA
Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova, alisema hawakuweza kumhoji Askofu Gwajima ili kumpa fursa afya yake iimarike zaidi.
Alisema Askofu Gwajima alifika Kituo Kikuu cha Polisi akisindikizwa na wasaidizi wake, saa 2 asubuhi.
“Alifika kituoni akiwa bado anatumia kiti cha magurudumu matatu (wheel chair) na alikubaliana na wapelelezi akaendelee kwanza na matibabu.
“Gwajima anatakiwa kurudi kuripoti Aprili 20, mwaka huu ili aendelee na mahojiano juu ya tuhuma za kumkashifu na kumtukana Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo,” alisema Kova.
Askofu Gwajima alizimia wiki iliyopita wakati akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kisha kupelekwa Hospitali ya Polisi Kurasini ambako aligoma kutibiwa.
Baada ya hapo alihamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako pia hakukubaliana nako ndipo akahamishiwa Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni.
https://ssl.gstatic.com/ui/v1/icons/mail/images/cleardot.gif

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...