Wednesday, April 8, 2015

bao la Samata laokoa mamilioni

BAO la straika wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika kikosi cha TP Mazembe ya Kongo (DRC), Mbwana Samatta dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, limeokoa mabilioni ya fedha za klabu hiyo.
Samatta wikiendi iliyopita ameiwezesha timu hiyo kutinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kufunga bao katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Ushindi huo umewezesha Mazembe kuokoa zaidi ya Sh bilioni tatu ambazo ni sawa na thamani ya kikosi  chote cha timu hiyo na kama wangepoteza ingekuwa hasara kubwa kwao na mmiliki wa timu hiyo.
Mchezo huo wa marudiano wa raundi ya kwanza, ulifanyika jijini Kinshasa juzi Jumapili, ikiwa ni baada ya wageni kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza nchini Afrika Kusini.
Mabao mengine ya TP Mazembe ambao ni mabingwa mara nne wa michuano hiyo, yalifungwa na Rainford Kalaba na Roger Assale, wakati lile la Mamelodi Sundowns liliwekwa kimiani na Percy Tau.

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...