Saturday, April 11, 2015

Mtoto Irene aliyefariki KIbamba mwaka jana aletwa akiwa hai na mganga kutoka Dodoma

 Mtoto Irene baada ya kufufuliwana mganga huyo
 mtoto Irene enzi za uhai wake kabla ya kufa


 watu wakiwa wengi wakitoa fedha na kumshangaa mtoto huyo

 Mganga aliyemfufua mtoto huyo kushoto aliyevaa flana ya kijani na mapete mkononi huku mama mzazi wa mto huyo akiwa amemshikilia mtoto Irene


Na Humphrey Shao, Dar es Salaam
MGANGA wa Jadi aliyejitambulisha kwa jina la, Juma Mohamed (Bino) Amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa eneo la Kibamba Mloganzila mara baada ya Kudai kuwa ameweza kumrejesha mtoto wa Mwaka mmoja na nusu aliyefariki mwaka jana na kuzikwa katika makaburi ya mloganzila pamoja na dada mmoja aliyefariki mkoani njombe mwaka jana.
Akizungumza na gaezti hili Juma Mohamed alisema kuwa mwishoni mwa mwaka jana wazazi wa mtoto huyo waliweza kumpigia simukuwa awana imani kuwa binti yao amefariki kifo cha kawaida hivyo wakata awapigie ramli kujua kama yupo ama amefariki ndipo alipwaambiwa kuwa mtoto wenu akufariki bali mlizika mbwa .
“mara baada ya kuwa mbia hivyo nikawambia wanitumie shilingi 50,000 wakatuma ndipo nilipanza kazi yao nilipoona inamafanikio nikawambia wanitumie tena shilingi 300,000 ndipo baadae nikawambia wapande gari kwa ajili yakuja kumalizia kazi lakini lazima waje na shilingi laki moja ya kumalizia kazi ndipo wakafanya hivyo nakufika kwa ajili ya kuweza kumuona mtoto wao”alisema Bino
Alisema kuwa wakati wa kuanza kazi hiyo niliwaagiza waje na wazazi wao ndipo wakafanya hivyo na tukaanza kazi ya kumvuta mtoto huko aliko kwa kutumia jina lake la Irene na la mama yake hili nyota ziweze kuendena kazi ifanikiwe.
Muda mchache tu ndipo nikafanikwa kumrejesha mtoto huyo ambaye alionekana kuwa yupo katika hali mbaya ya kiafya na kuwaomba nikae nae kwa miezi miwilina nusu kwa jili ya tiba zingine za kumuweka sawa kumtoa katika undondocha nakuwa katika hali ya kawaida.
Baba asimulia
Akisimulia tukio hilo baba mzazi wa mtoto Irene anasema kuwa na huakika kabisa huyo ndio mtoto wake kwani tangu siku yakuaga maiti alikuwa ana imani na yule marehemu aliyekuwa kwenye jeneza kwa kuona sura ikiwa na kovu la kimasai wakati mwanwe akuwa hivyo.
Alisema kuwa mtoto wake ambaye alifariki mwezi wa nane mwaka jana kw akifi cha ghafla ni huyo ambaye mganga huyo aliweza kumleta mnamomiezi miwili iliyopita hivyo wao kama wao wakasubiri amalize tiba ndio hiyo juzi wameamua kumrudisha katika makazi yao.
“kabla ya kwenda huku nilikwenda sehemu nyingi na nikaambiwa kuwa mtoto wangu ajafariki moja ya sehemu niliyoenda ni kwa nabii flora kule tegeta kwa jaili ya maombi nako nikaambiwa niombe mungu mtoto wangu akapatikana hivyo mmoja ya watu wakanipa namba ya simu ya huyu mganga name nikampigia na akaniambia kuwa kweli mwanangu namuona yupo sehemu hivyo siku niliyoenda alingia mahali na kushika mwiko kisha akarudi na mtoto tulivyomtazama tukaona ni yeye hivyo sisi tuna mshukuru mungu”alisema Raphael Mtoro

Mama Ashuhudia
Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto huyo Helena Raphael aliseama kuwa ana uhakika kuw ahuyo ni mwanawe na ana alama zote ambazo anazitambua kwa mtoto huyo tangu afaraiki mwaka jana hivyo sio jambo la kuzungukazunguka juu ya kupatikana kwa mtoto wake.
“mimi sina mengi ya kueleza huyu ni mwanangu na namtambua kw akila kitu licha ya kuwa mwaka jana kulikuwa na msiba na tukazika hpa hivyo mi sijui nini kilitendeka nashukuru mungu mwanangu karudi hapa hivyo hapa sisi ni sherehe tu na kufuta ule msiba uliotekea hapo awali kw akuwa mungu amejibu maombi yetu”alisema mama wa mtoto huyo.


Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa
Kwa upande wake mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mloganzila, Leila Mabewa aliseam kuwa yeye kama yeye amepta taharifa kutoka kwa wajumbe wake wa nyumba kumina kumuhakikishi akuwa tukio hilo la msiba lilitokea katika nyumba hiyo mwaka jana na mtoto aliyezikwa ni huyo huyo hivyo na leo ameonekana  na kila mtu anamshangaa mtoto huyo jambo ambalo yeye linamtia utata wa kuthibitisha.
“mimikama mwenyekiti wajumb wangu wansema huyo mtoto ndo aliyefariki na sasa mzima hivyo nimeona jambo hili nilipeleke Polisi hili wafanye uchunguzi wa kina ju yamtoto huyu hili kuepusha mambo mengine ambayo sio ya uhakika moja kwa moja kwnai kilichopo hapa ni swala la imani”alisema Mwenyekiti huyo.

Mpaka mwandishi wa gazeti hili anaondoka kituo cha Polisi cha Mbezi kwa Yusufu kulikuw ahakuna taharifa zinginine juu ya tukio hili kutoka eneo hilo zaidi ya watu kuendelea kumiminika nyumbani kwa wazazi wa mto huyo kutka kumshuhudia mtoto.
Mwisho. mama mzazi wa mtoto Helena Raphael Mtaroakiwana mtoto wakielekea kituo cha Polisi
 Jenifer Mwenda ambaye amefufuliwa akiwa na mimba

No comments:

Post a Comment

Waziri Dk Kigwangalla ataka wavamizi maeneo yaliyohifadhiwa kuondoka

Mwandishi wetu,Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewataka wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi nchini,...