Monday, April 27, 2015

Rais Kikwete afika kutoa Salamu za Pole Nyumbani kwa Marehemu, Brigedia Jeneral Hashim Mbita

Kiongozi mkuu wa ACT zito kabwe akitoa pole kwa mke wa marehemu
 Rais Jakaya Kikwete akisaini katika kitabu cha salamu za Rambi rambi
 Rais Kikwete akimsalimia mke wa marehemu Hashim Mbita, Ngeme Shomari Mbita
Rais Kikwete akimuomba akae mke wa marehemu Hashim Mbita ,Ngeme Shomari Mbita
 Rais Kikwete akiapata maelezo kutoka kwa ndugu wa marehemu Hashim Mbita
 Rais kikwete akicheza na mmoja wa wajukuu Marehemu Brigedia Jeneral Hashim Mbita
 Waziri wa mabo ya nje Bernard Membe akitoa pole kwa mke wa marehemu brigedia Jenerali Hashim Mbita
 Katibu mkuu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam akitoa pole kwa watoto wa marehemu
 Balozi wa Afrika Kusini Nchini akitoa pole kwa mke wa marehemu Hashim Mbita na watoto
 Balozi wa Afrika Kusini akisaini kitabu cha wageni


. Nchi mbalimbali za Kusini mwa Afrika zimemlilia marehemu Brigedia Jenerali Hashim Mbita kutokana na mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi hizo ulioratibiwa na Serikali ya Tanzania.
Hashimu Mbita (82) alifariki siku ya Jumapili asubuhi katika hospitali ya Lugalo kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu uliomsumbua kwa miezi nane, huku muda mwingi akilazwa hospitali, na baada ya muda kurejeshwa nyumbani.
Mabalozi kutoka nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Angola na Zambia walifika nyumbani kwa marehemu kuwafariji wafiwa na kumzungumzia Mbita jinsi alivyokuwa na mchango mkubwa katika ukombozi wan chi zao.
Balozi wa Zimbabwe nchini, Edzai Chimonyo alisema marehemu Mbita alikuwa kiini katika mapambano dhidi ya wakoloni walioitawala Zimbabwe kwa muda mrefu na kuwanyonya wananchi wa nchi hiyo.
Chimonyo alisema Mbita alikuwa ni mtu wa kujitolea na alifanya kazi kubwa chini ya maelekezo ya Mwalimu Julius Nyerere. Aliongeza kuwa kumpoteza mtu kama yeye ni pigo kwa Afrika, na kuwa anastahili heshima kubwa.
“Tunafurahi kwa sababu Mbita aliweza kuandika vitabu 9 vyenye historia ya ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika. Tutamkumbuka daima kwa kutuachia historia ya ukombozi katika maandishi kwani vizazi vijavyo vitapata kufahamu historia hiyo,” alisema.
Chimonyo aliongeza kuwa unapozungumzia mchango wa Tanzania katika ukombozi wan chi za kusini mwa Afrika huwezi kuacha kumtaja Mbita kwa sababu alikuwa na mchango mkubwa katika kutekeleza maagizo ya Mwalimu Nyerere.
Ofisa kutoka Ubalozi wa Angola, Joel Cumbo alisema Mbita alikuwa kiungo muhimu katika kupigania uhuru wa Angola. Alisema mbinu na maarifa yake katika mapambano ndiyo yaliyopelekea ushindi dhidi ya mkoloni.
Alisema Angola ilikuwa ikipokea silaha kutoka Urusi kupitia Tanzania. Cumbo aliongeza kuwa mpaka silaha hizo zinaifikia Angola, Mbita ndiye aliyekuwa kiungo na kuwasaidia wanajeshi wa nchi yake mbinu za mapambano.
“Raia wa Angola wanamfahamu vizuri kwa kuwa alikuwa karibu nao katika mapambano dhidi ya mkoloni. Nipo hapa leo kwa niaba ya Serikali ya Angola kutoa pole kwa wanafamilia,” alisema ofisa huyo.

Rai Kikwete akiwa mwenye huzuni huku akipata maelezo kutoka kwa mke wa marehemu Brigedia Jenreali Hashim Mbita, Bi Ngeme Shomari Mbita

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...