Thursday, April 9, 2015

UTT-PID yashiriki katika mkutano mkuu wa 30 wa ALAT Jijini Dar es Salaam

 Naibu waziri wa TAMISEMI,Khasim Majaliwa,akipata maelezo na kusaini kitabu cha wageni kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Tasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu chini ya Wizara ya Fedha, Bw, Uli Mtebe
 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa, Mh Hawa Ghasia, akisaini kitabu na kupata maelezo kutoka Afisa Uhusiano Mkuu wa Tasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID), Uli Mtebe, akiambatana na Afisa Masoko, Bi, Kilave Atenaka
Na Humphrey Shao
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID) inayoshiriki  mkutano  mkuu wa miaka wa 30 wa jumuia za  Serikali za Mitaa Nchini (ALAT), unaofanyika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.Mkutano huo ulioanza Aprili 8 na kutarajiwa kumalizika Aprili 11,  UTT-PID imeendelea kutoa elimu na huduma za taasisi hiyo.
UTT-PID  ambayo imejikita hususani katika upimaji wa viwaja  na upangaji wa  miji katika maeneo mbalimbali ya Nchi  ikiwemo  Halimashahuri ya Lindi, Bukoba, Sengerema, Bagamoyo, Chalinze, Morogoro na Halimashahuri nyingine mbalimbali za hapa Nchini.
Aidha, katika  maonyesho hayo, banda la UTT-PID  limeendelea kutoa elimu na huduma kwa watu mbalimbali kuhusiana na kazi zao  zinazofanywa na taasisi hiyo kwa wajumbe wa ALAT na wananchi wanaotembelea banda hilo.
Pia viongozi mbalimbali wa kiserikali  akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  Hawa Ghasia.
 Kazi  za UTT-PID ni pamoja na Utoaji huduma za  ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
END.

 g
Naibu Waziri wanchi Tawala za Mikoa Agrey Mwanri akisaini kitabu cha wageni na kupata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mkuu wa Tasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID), Uli Mtebe, akiambatana na Afisa Masoko, Bi, Kilave Atenaka

No comments:

Post a Comment

MWENGE WA UHURU WAINGIA GAIRO NA KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA MILIONI MIASABA NA ZAIDI

 Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Morogoro Regina Chonjo mara ulipofika katika eneo la Ma...