Thursday, April 16, 2015

Wema: Kumuimba msichana uliyeachana nae ni ushamba


NA RHOBI CHACHA
STAA wa filamu za kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amesema ni ushamba kwa wasanii wa muziki kuwatungia nyimbo za majungu wasichana wanaoachana nao kimapenzi.
Wema wasanii wengi wa muziki wamekuwa na tabia ya kishamba ya kutunga nyimbo zenye maneno ya kuudhi wakiwalenga waliokuwa wapenzi wao.
“Ni ushamba wa mapenzi, haiwezekana mlikuwa mnafurahia wote mapenzi yenu lakini mkiachana anakutungia wimbo za kukuponda hakuna neo la kuzungumzia hilo zaidi ya kuita ushamba kwa wasanii wa aina hiyo,’’ alisema Wema
Hata hivyo kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani kutoka studio moja kubwa ya kurekodi muziki nchini kuna wimbo wa wasanii wawili waliowahi kuimba pamoja na wimbo wao ukawa gumzo kwa mashabiki wa muziki huo wanamalizia kurekodi wimbo unaodaiwa unamzungumzia mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment

MWENGE WA UHURU WAINGIA GAIRO NA KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA MILIONI MIASABA NA ZAIDI

 Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Morogoro Regina Chonjo mara ulipofika katika eneo la Ma...