Saturday, June 20, 2015

Diwani wa Kibada na mtia nia wa Ubunge,Juma Nkumbi akabidhi vifaa kwa ajili ya ligi ya Jimbo la Kigamboni

 Diwani wa Kibada Juma Nkumbi akikabidhi mipira
 Diwani wa Kibada Juma Nkumbi akikabidhi jezi kwa timu ya Kibada Kombaini


MASHINDANO ya Kombe la Kigamboni yamezinduliwa rasmi na  yanatarajiwa kuanza leo katika viwanja mbalimbali vya Kata ya Kigamboni.
Diwani wa Kata ya Kibada, Juma Nkumbi, ambaye ndiye mwandaaji wa mashindano hayo, jana aligawa vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 4 kwa timu 20 zinazoshiriki mashindano hayo, ambapo kila timu imepata mipira miwili pamoja na jezi seti moja.
Akizungumza wakati wa uzinduzi na ugawaji wa vifaa hivyo kwa timu shiriki, Nkumbi alisema lengo la mashindano hayo ni kutoa fursa kwa vijana kushiriki kwenye michezo, lakini pia kuendeleza vipaji vyao vya soka, ikiwa ni moja ya ajira yao.
“Kama ilivyo Ilani ya Chama cha Wananchi (CUF), tutakapofanikiwa kuchukua nchi tutahakikisha timu yetu ya Taifa inashiriki mashindano ya Kombe la Dunia, hivyo katika kuelekea huko tumeona ni bora kuanzia chini kwa kuwaendeleza vijana katika soka,” alisema Nkumbi.
Nkumbi alisema mshindi wa kwanza katika mashindano hayo yatakayokuwa yanachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini atajinyakulia Sh 1,000,000 huku mshindi wa pili akijipatia Sh 700,000 na mshindi wa tatu akiondoka na Sh 500,000.

 vijana wa Sarakasi wakitoa burudani kabla ya mchezo
 vijana wa sarakasi wakitoa burudani kabla ya mchezo
 Juma Nkumbi akizungumza na wakazi wa mbagala  Zakhem
Juma Nkumbi akipiga mpira kuashiria kuzinduliwa kwa mashindano hayo katika uwanja wa Zakhem

No comments:

Post a Comment

Waziri Dk Kigwangalla ataka wavamizi maeneo yaliyohifadhiwa kuondoka

Mwandishi wetu,Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewataka wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi nchini,...