Wednesday, July 8, 2015

KINONDONI WAVUNJA BARAZA LA MADIWANI WAKITAMBA KWA MAFANIKIO MAKUBWA



Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni , Yusuph Mwenda akimkabidhi jezi ya timu ya soka ya Kinondoni Municipal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi kama ishara ya kuwa mlezi wa timu hiyo




Na Mwandishi wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeliahirisha rasmi Baraza la Madiwani ambapo mgeni rasmi katika kuahirisha Baraza hilo alikuwa mheshimiwa Rais mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi.
Shughuli hizo zilianza kwa kikao cha baraza cha kawaida cha kupokea taarifa ya utekelezaji ambapo baada ya hapo aliwasili mgeni rasmi Mheshimiwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na kufuatiwa na tukio la kupita katika mabanda maalum yaliyoandaliwa yakionyesha shughuli za kila idara na kupata maelezo ya shughuli zinazofanywa na idara hizo pasitisha moja na mafanikio mbalimbali katika idara hizo.Baada ya mgeni rasmi kupita katika mabanda hayo na kupata maelezo ndi[po kilianza kikao rasmi cha baraza cha kusitisha rasmi baraza hilo ambapo lilianza kwa ufunguzi wa sala na kisha utambulisho uliofanywa na Mstahiki Meya Yusuphu Mwenda kabla ya wawakilishi mbalimbali wa vyama vya siasa kutoa neno.
Akiongea mkurugenzi wa jiji alilipongeza baraza la Madiwani na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondonikwa kazi nzito waliyoifanya ambayo Tanzania nzima wanaikubali ikiwepo ukusanyaji mzuri wa mapato na kumalizia kuwa Manispaa hii ni mfano mzuri wa kuigwa na Mstahiki Meya ni Meya wamfano kwa Tanzania nzima.Akiongea katika kikao hicho mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni alilishukuru Baraza la madiwani kwa ushirikiano wao katika kutekeleza shughuli za maendeleo kwa Manispaa hii ambapo ni mengi sana yaliyotekelezwa na mengine kutokana na muda bado hayakuweza kutekelezeka,lakini ameahidi kuyatimiza yale ambayo wameyabariki yafanyike likiwepo la kujengwa kwa mtambo wa kuchakata taka huko mabwepande ambapo tayari na mkataba umeshasainiwa wa kuanza kujengwa kwa mtambo huo kwa msaada wa Humburg city.
Mgeni rasmi alitoa medani na vyeti kwa madiwani na kwa baadhi ya watendaji akiwepo Mkurugenzi.Katika kuitambulisha timu ya KMC-FC ambayo ni timu ya Manispaa ya Kinondoni mgeni rasmi alikabidhiwa jezi ya timu hiyo yenye jina lake Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ,hali kadhalika madiwani pia walipewa jezi hizo kila mmoja zenye majina ya kila mmoja na mkurugenzi aliwaomba kuitangaza timu hiyo na kuisaidia kwa hali na mali .
Akiongea katika hafla hiyo Mstahiki Meya aliwashukuru wakazi wa kinondoni kwa ushirikano.kuhusiana na suala la maendeleo Meya alisema kumekuwa na ushiriki mpana wa wananchi katika maendeleo na pia uboreshwaji wa fedha za matumizi ya umma kwa kujenga mashule,barabara,mahospitali ambapo aliiongelea pia hospitali ya Mabwepande ambayo itakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi,akiongelea upande wa mapato alisema pato limeongezeka sana kutoka bil.11 kutoka kipindi cha nyuma hadi kufikia bil.35 hivi sasa.Akiongelea suala la vibali vya ujenzi kwa sasa vimekuwa vikitolewa na kupunguza msongamano na nia ni kuhakikisha vibali vya ujenzi vinapatikana ndani ya wiki moja,kuhusu usafi.
alisema Manispaa imekuwa ikishinda mfululizo katika mashindano ya usafi yanayosimamiwa na wizara ya afya pamoja na hilo aliongelea pia mpango kabambe wa alioucha katika mchakato wa utunzaji wa coco beach ili kuiboresha na kubadilishwa sura yake licha ya hayo manispaa hii pia imekuwa ikipata tuzo ya kutunza mahesabu vizuri,.Pia alimshukuru Naibu Meya Songoro Mnyonge kwa ushirikiano na ushauri mzuri ambao amekuwa akimpa na mkurugenzi kwa ubunifu na ushirikiano wake pamoja na watendaji wote kwa ujumla.Kaimu mkuu wa mkoa akiongea alipopewa nafasi alisema haihitaji hata maelezo kuelezea Manispaa ya Kinondoni kwani juhudi zao zinaonekana kwa macho.Mgeni rasmi akiongea katika hafla hiyo aliwashukuru kwa heshima hiyo waliyompa kwani alikuwa ana hamu kubwa ya kuja kuonana na watendaji wa Manispaa hii ,alisifia kazi nzuri ya kuboresha maendeleo katika Manispaa hii na kuongeza kuwa Kinondoni ina uwezo wa kuendesha mambo vizuri kwa kuja kwake katika hafla hii amefundishika haswa.Hongera Manispaa ya Kinondoni.

 Meya akiahutubia wananchi


Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Alli Hassan Mwinyi, akikagua maonyesho ya kazi zinazofanywa na manispaa ya Kinondoni.




Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Alli Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti na na nishani ya utumishi uliotukuka Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni, Yusuph Mwenda wakati wa sherehe zakufunga barza la manispaa hiyo



Rais Mstaafu wa awamu ya pili , Alhaji Ally Hassan Mwinyi, akimkabidhi cheti cha utumishi uliotukuka katika baraza la madiwani Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, wakati wa hafla ya kuvunja baraza la madiwani la Manispaa ya Kinondoni




No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...