Saturday, July 11, 2015

Mashindano ya wana Sayansi vijana kufanyika Agosti 5 mwaka huu (YST)

 Mkurugenzi wa tasisi ya Youn Scientist Dr Gozibert Kamugisha  akizungumza na waandishi wa habri juuu yaashindano ya wanasayansi vijana


Description: Macintosh HD:Users:josephclowry:Desktop:12_01_02_Yst Logos:Platinum Sponsors:yst logo without sponsors.psd 
        Concern Tanzania, Plot 169 Regent Estate, P.O. Box 61429, Dar es Salaam, Tanzania.
                                                   
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Young Scientists Tanzania (YST) inayo furaha kuwafahamisha wanafunzi, walimu na watu wote kwa ujumla kuwa onesho lilikuwa likisubiriwa kwa hamu la YST 2015 litafanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia tarehe 5 hadi 7 August 2015. Hili ni onesho na hitimisho la tafiti za sayansi na tekinologia zilifanywa na wanafunzi wa sekondari kwa takribani mwaka mmoja. Kwa mara nyingine tena, wadhamini wakuu wa maonesho haya BG Tanzania na Irish Aid wamewezesha mafanikio haya.
Ni mafankio makubwa kwa YST kuweza kuifikia mikoa yote kwa kipindi cha miaka mine. Maonesho ya YST 2015 yajumisha wanafunzi 240 na walimu 120 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar. Kwa siku tatu za maonesho, wanafunzi wataonyesha kazi zao za ugunduzi na utafiti wa kisayansi kama vile kemia, fizikia na hesabu, biologia na ekologia, teknologia na sayansi ya jamii. Ingawa kazi hizi zinajumuisha maeneo mapana ya kisayansi, kazi nyingi zimejikita katika kutafuta ufumbuzi kwa masuala kama afya, kilimo na usalama wa chakula, usalama, mawasiliano na uchukuzi, nishati na mazingira, elimu, mahusiano na matatizo ya kijamii.
Bado tuna changamoto katika kuinua kiwango cha sayansi kwa shule za sekondari hasa ukizingatia uchache wa wanafunzi wanaosoma sayansi na ufaulu usioridhisha. Ingawa ufaulu umeanza kuimarika kidogo miaka ya karibuni tatizo kubwa limebaki kuwa ukosefu wa sayansi kwa vitendo na matumizi ya sayansi katika kuboresha maisha ya watu....sayansi haiwezi kufanywa kwa kutumia chaki na ubao tu. Maonesho ya YST 2015 yanajaribu kuonyesha kuwa kufanya sayansi ni raha inayotakiwa kufanyika kwa vitendo kumaliza matatizo mbalimbali na inaweza kufanyika popote kwa kutumia vifaa vyovyote. Washiriki wa maonesho ya YST 2015 wataonyesha kupitia kazi zao kuwa kuna namna ya Tanzania kuondokana na umasikini.
Kama njia ya kuwashukuru vijana wabunifu, zawadi zitatolewa kwa wanafunzi wenye kazi nzuri za kisayansi. Takribani wanafunzi 60 watazawadiwa zawadi mbalimbali kama pesa saslimu, medali, vikombe, vifaa vya maabara, na matengenezo ya library na vitabu. Wanafunzi 6 watazawadiwa udhamini wa kusoma vyuo vikuu kusoma shahada za sayansi na teknologia na kuendelea kufanya kazi za kisayansi katika maisha yao. Washindi wa jumla wa maonesho ya YST 2015, pamoja na kupewa pesa na udhamini wa masoma ya chuo kikuu, pia watashinda zawadi ya kwenda Ireland na USA mapema 2016 kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
YST 2015 ni onesho la wanafunzi wenye vipaji katika sayansi. Pia ni ushahidi katika kuimalika kwa ujuzi wa walimu ambao ni walezi wa wanafunzi hao. Haya yote ni matokeo ya mafunzo kwa walimu ambayo yamekuwa yakitolewa na YST kwa miaka mine iliyopita. Wanafunzi wapatao 2,000 kutoka sekondari za Dar es Salaam wamealikwa kutembelea maonesho na kuja kujionea ubunifu wa vijana wenzao. Wananchi wote wanaalikwa kutembelea maonesho tarehe 6 na 7 August 2015.

Young Scientists Tanzania(YST) is happy to inform students, teachers and the general public that the long awaited YST 2015 exhibition will run for three days at Diamond Jubilee Hall in Dar es Salaam from 5th – 7th August 2015. This exhibition will be a showcase and culmination of year-long innovative and scientific investigations done by secondary school students. Once again, the main sponsors, Irish Aid and BG Tanzania, are the driving force behind this success.
It is a great achievement that over the period of four years YST has covered every region.  YST 2015 exhibition will involve 240 students and 120 teachers from all 30 regions of Tanzania Mainland and Zanzibar. Over three days of the exhibition, students will showcase projects in various areas of science such as chemical, physical and mathematical sciences; biological and ecological sciences; social and behavioural sciences; and technology. Although the projects are covering wide areas of science, most projects are addressing issues such as health, agriculture and food security, communications and transportation safety, energy and environment, education, social relations and social problems.
We still have major problems in improving the level of sciences in secondary schools leading to low subscription and unconvincing pass rates. While pass rates are gradually improving, the major problem remain to be the lack of practicals and application of sciencies in improving people’s life...sciences can never be done by using chalk and blackboard. YST 2015 exhibition tries to demonstrate that science is fun, practical and problem solving, and can be done both inside and outside the classroom. Participants of YST 2015 exhibition will show through their projects that there is a way out of poverty in Tanzania.  
As a way of acknowledging the great work done by the young and innovative minds, prizes will be awarded to students with bests projects. About 60 students will win prizes in form of cash, medals, trophies, lab equipment and library refurbishment. University scholarships will be awarded to six students to help them to pursue scientific and technological studies in universities and ultimately take up scientific carriers. Overall winners of YST 2015 exhibition will also win  all expenses paid trip to Ireland and USA in 2016 to represent Tanzania in international scientific and technological competitions for young scientists.
YST 2015 exhibition is a showcase of scientific talents of secondary school students. It is also a testimony of improvement of skills of teachers of who are the mentors of the students. This is the result of trainings provided to science teachers by YST over the periods of four years. About 2,000 students from secondary schools in Dar es Salaam have been invited to visit the exhibition and experience the ingenuity of their fellow young people. All people are invited to visit the exhibition on the 6th and 7th August 2015.
  Contact: Dr. Gosbert Kamugisha, YST Executive Director & Co-Founder, +255767708579.

No comments:

Post a Comment

Waziri Dk Kigwangalla ataka wavamizi maeneo yaliyohifadhiwa kuondoka

Mwandishi wetu,Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewataka wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi nchini,...