Tuesday, July 7, 2015

MSTAHKI MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI YUSUFU MWENDA AKABIDHI VIZIMMBA 512 KWA WAFANYABIASHARA

 Meya wa Manispaa ya Kinondoni , Yusufu Mwenda akikagua soko jipya la Mawasiliano Simu 2000 Sinza


Na Mwandishi wetu

MSTAHIKI  Meya wa manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda  amesema kuwa soko jipya la SIMU 2000 litaweza kuchukua wafanyabiashara 512 kutoka kila pembe ya manispaa ya kinondoni.

Mwenda amewatoa hofu wafanyabiashara wa soko jipya la kituo cha basi cha Simu2000 mawasiliano  kuwa watafanya biashara bila ya kuwa na matatizo yoyote kwa kuwa soko hilo lipo katika mfumo wa kisasa.

Mwenda alisema hayo alipokuwa akikabidhi vizimba vya soko hilo kwa wafanya biashara ndondogo waishio katika wilaya ya kinondoni na sio mtu kutoka eneo la nje ya manispaa hiyo hivyo kuwataka kulitunza soko hilo kama mali yao.
“tumeamua kulifanya soko hili hili liweze kuanza kazi kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanywa baadae hili kuweza  kuwapa fursa wafanya biashara kuliko kuacha jingo limeisha na kuonekana kama picha hivyo nawaomba mfanye biashara hili muweze kujiongeza kipato” alisema Mwenda.

Alitoa wito kwa wafanyabiashara hao kutokata tama kwani mwanzo ni mgumu kwnai eneo lenyewe ni jipya hivyo sio rahisi kuona biashara ikichanganya kwa haraka kama wanavyofikiri.

mwisho


 akiteta jambo na bahadi ya watumishi wa manispaa ya kinondoni

akziungumza na wafanyabiashara hao mara baada ya kukabidhi vizimba

No comments:

Post a Comment

ROSEMARY LUHAMO KUTOKA DODOMA AKABIDHIWA MAMILIONI YAKE NA UMOJA SPESHO

 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo akiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa pesa zake kupitia Benki ya CRDB na Kampun...