MOURINHO ATUPIWA VIRAGO RASMI CHELSEA



Mourinho atupiwa virago Chelsea
LONDON England
CHELSEA hatimaye imefikia uamuzi mgumu kabisa wa kumtimua kocha wao kipenzi, Jose Mourinho ikiwa ni miezi saba tu tangu kocha huyo aimbiwe wimbo wa kishujaa baada ya kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa England.
Uamuzi wa Bodi ya Chelsea umetangazwa jana jioni na umeelezwa kuchangiwa na matokeo mabaya ya timu hiyo katika Ligi Kuu ya England (EPL) msimu huu, ambapo timu hiyo inashika nafasi ya 16 ikiwa na pointi 15 kutokana na michezo 16 iliyocheza.
Kufungwa na vinara wa ligi hiyo Leicester City mabao 2-1 na kuwafanya wawe nyuma kwa pointi 20 nyuma ya timu hiyo, kulimfanya mmiliki wa  Chelsea, Roman Abromovic kuitisha kikao cha bodi ambacho kwa pamoja kilifikia uamuzi mgumu licha ya malalamiko ya kocha huyo aliyoyatoa kwamba anahujumiwa na wachezaji wake.
 

Post a Comment

Previous Post Next Post