Saturday, February 21, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUZALIWA MWANZILISHI WA USKAUTI DUNIANI, LORD ROBERT STEVENSON SMYTH BADEN-POWELL, JIJINI DAR.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha Nishani ya Juu, Skauti Barnaba Abel, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mwanzilishi wa Uskauti Duniani, Lord Rebert Stevenson Smyth Baden-Powell, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Feb 21, 2015. Kulia ni Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania,  Abdulkarim Shah na (kulia kwa Makamu) ni Rais wa Skauti Tanzania, Dkt. Shukuru Kawambwa. Picha na OMR
 na Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania,  Abdulkarim Shah (kulia) na Kiongozi wa Skauti, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Feb 21, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mwanzilishi wa Uskauti Duniani, Lord Rebert Stevenson Smyth Baden-Powell. Picha na OMR
 Vijana wa Skauti wakipita mbele ya jukwaa kuu kwa maandamano wakati wa sherehe hizo za maadhimisho hayo. Picha na OMR

Vijana wa Skauti wakionyesha michezo ya ukakamavu wakati wa sherehe hizo. Picha na OMR

Vijana wa Skauti wakionyesha michezo ya ukakamavu wakati wa sherehe hizo. Picha na OMR

Friday, February 20, 2015

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHA RA JANETH MBENE AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI BURUNDI


MELI NYINGINE KUBWA YENYE UREFU WA MITA 209 YATIA NANGA BANDARI YA MTWARA
Mabadiliko ya teknolojia pamoja na kuboreshwa kwa bandari zilizo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) zimeanza kuzaa matunda baada ya meli nyingine kubwa yenye urefu wa mita 209 kutia nanga Bandari ya Mtwara.


Ujio wa meli hiyo iliyotia nanga katika Bandari ya Mtwara ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nchini baada ya Bandari ya Dar es Salaam na Tanga umefanya jumla ya meli kubwa na za kisasa zilizotia nanga katika bandari zetu nchini kufikia tatu.


Meli nyingine kubwa na ya kisasa kuja nchini kwa mara ya kwanza ilikuwa ni Maersk Cubango mali ya Maersk Line iliyokuwa na urefu wa mita 250 na upana wa mita 38 ikiwa na uwezo wa kubeba kontena 4,500.


Kabla ya ujio wa meli hiyo, Meli kubwa nyingine ni MSC Martina yenye urefu wa mita 244 na upana wa mita 32.2 ikiwa na uwezo wa kubeba makontena 2,411 pia ilifanikiwa kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.


Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Bandari ya Mtwara kupokea meli kubwa yenye urefu wa mita 209 ikilinganishwa na meli ambayo iliwahi kutia nanga katika Bandari ya Mtwara ambayo ilikuwa na urefu wa mita 205. 


Meli hii kubwa iliingia Bandarini Mtwara tarehe Februari 04, 2015 ikiwa na jumla ya Makontena 1,240 ambayo yalishushwa na kupakia Makontena 1,027 yaliyosheheni Korosho. 


Kitu pekee kilichokuwa kivutio wakati wa kuingia kwa meli hiyo ni umaridadi wa Kapteni wa Bandari ya Mtwara Kapteni Hussein Kasugulu kuingiza meli kwa kutumia ‘Tug’ moja tu ambapo ni vitu adimu kwa Bandari nyingine kufanyika. Kwa kawaida meli huingizwa katika bandari kwa kutumia ‘Tug’ mbili.


Meli hiyo inatarajiwa kuondoka Bandarini hapa baada ya siku tano, ikishasheheni shehena ya mzigo wa korosho ambalo ni zao kuu la biashara katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania, haswa Mtwara.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA BARABARA YA KM 10 YA MSOGA-MSOLWA NA KAGUA MZANI MPYA WA KISASA WA VIGWAZA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi. Evarist Ndikilo, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuzindua rasmi Barabara ya Kilometa 10 ya lami ya Msoga-Msolwa, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika jana Feb 17, 2015 Msoga. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli na Mbunge wa Chalinze kwa pamoja wakikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Barabara ya Msoga- msolwa wakati wa hafla ya uszinduzi huo iliyofanyika jana Feb 17, 2015 Msoga. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli, wakati akimpa maelezo kuhusu Mzani mpya wa kisasa uliokamilika kujengwa eneo la Vigwaza Mkoani Pwani, ambao umeanza kutoa huduma, wakati alipotembelea mzani huo akiwa katika Ziara yake ya Mkoa wa Pwani jana Feb 17, 2015. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAJULIA HALI WANANCHI WALIOANGUKIWA NA NYUMBA ZAO KWA UPEPO NA MVUA KUBWA MSOGA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia), wakati alipowasili Kitongoji cha Mnazi Mmoja, Msoga jana kwa ajili ya kuwafariji wananchi waliokubwa na maafa kwa kuangukiwa na nyumba zao kutokana na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi. Katika tukio hilo jumla ya watu 12 walijeruhiwa na jumla ya nyumba 128 kubomoka. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji Bi.Fatuma Janga na baadhi ya majeruhi wakati alipowatembelea jana Feb 17, 2014 baada ya kuangukiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi kijijini  hapo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli na baadhi ya Viongozi, wakati alipowasili Kitongoji cha Mnazi Mmoja, Msoga jana kwa ajili ya kuwafariji wananchi waliokubwa na maafa kwa kuangukiwa na nyumba zao kutokana na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi. Katika tukio hilo jumla ya watu 12 walijeruhiwa na jumla ya nyumba 128 kubomoka. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KITAIFA KUHUSU WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed  Gharib Bilal, akizungumza wakati akifungua rasmi Kongamano la Kitaifa kuhusu Watoto walio katika mazingira hatarishi, lililofanyika leo Feb. 18, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akimkabidhi Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, Vitabu vya Miongozi kuhusu huduma za Watoto walio katika Mazingira Hatarishi na Sheria ya Mtoto No, 21 ya mwaka 2009, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa kuhusu Watoto walio katika mazingira hatarishi, lililofanyika leo Feb. 18, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa dare s Salaam, Said Meck Sadik na Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akimkabidhi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Ummy Mwalimu, Vitabu vya Miongozi kuhusu huduma za Watoto walio katika Mazingira Hatarishi na Sheria ya Mtoto No, 21 ya mwaka 2009, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa kuhusu Watoto walio katika mazingira hatarishi, lililofanyika leo Feb. 18, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa dare s Salaam, Said Meck Sadik na Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mwanafunzi, Zulfa Said, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa kuhusu Watoto walio katika mazingira hatarishi, lililofanyika leo Feb. 18, 2015 kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Banana Zorro (kulia) na msanii wa maigizo, Angelina Leonard, na baadhi ya washiriki katika Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akihutubia.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...