Friday, March 6, 2015

Mbunge wa Ileje Aliko Kibona asinzia wakati wa Kikao cha kamati ya Bunge ilipotembelea mamlaka ya hali ya hewaUshirikina chanzo cha mauaji ya watu wenye Albinism’ – Dk. Ally Possi


EXCLUSIVE INTERVIEW: ‘
Na Andrew Chale wa modewji blog
Dk. Ally Possi ambaye ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam. Akielezea na kuchambua kwa kina kuhusiana na wimbi la mateso na mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wenye albinism.
Mo dewjiblog, iliamua kufanya mahojiano maalum ilikukuletea wewe msomaji wetu unayeperuzi mtandao wako bora kabisa kujua na kuelewa na nini kifanyike ikiwemo mimi na wewe katika kuchukua hatua.
Suala la mauaji dhidi ya watu wenye albinism:
“JAMII yenye ushirikina ndio yenye kuamini suala la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambao wana albinism, hivyo ilikuondoa imani hii potofu ni kutoa elimu katika maeneo yote na kuwalinda popote pale, Jambo hili ni jukumu letu sote” anabainisha Dk. Ally Possi.
Dkt. Possi anabainisha kuwa, Serikali itaendelea kulaumiwa mpaka hapo juhudi za dhati za kukomesha mauaji na vitendo vya kikatili vitakavyochukuliwa na kutokomezwa kabisa.
Fuatilia hapa Mahojiano hayo maalum.
MO DEWJI BLOG : Karibu, mgeni wetu katika mtandao huu wa kijamii unaokuletea habari bora kabisa zilizochambuliwa kwa kina za ndani, nje na makala maalum za kina.
DK. POSSI: Asante, nashukuru sana…
MO DEWJI BLOG: Unadhani nini chanzo na hali ya ongezeko la vitendo hivi kwa sasa hapa Tanzania?
DK.POSSI: “Kwanza mauaji ni.. yanatokana na imani potofu. Imani potofu kwa jamii kuwa ukipata kiungo cha alibino unafanikiwa.
Hii ni imani potofu kwa jamii ya watu wenye kuamini ushirikina.
“Albino ni ulemavu ambao mtu anakosa aina ya vitamin inayoitwa melaniani…
Inakosekana ikiwemo katika ngozi, nywele na macho” anaendelea kubainisha kuwa: Kuwa albinism ni hali ya kurithi kutoka kwa wazazi wote wawili ama mmoja. Ni kwamba baba na mama wanakuwa na vinasaba vinavyokuwa na albinism na vinapokutana wakati wa kutunga mtoto ndipo mtoto mwenye albinism anazaliwa.
MO DEWJI BLOG: Vipi inahusishwa na suala la Imani?
DK. POSSI: “Imani sio dini, Ni imani ya kishirikina.
“Sijui kitu gani ambacho kimetokea kikaleta hiyo imani, kwa kifupi ipo kwenye jamii iliyoendelea na uwezo wake wa kiuchumi ni mdogo na elimu pia.
Pia tunaweza kusema: “Suala hili ni la imani, Imani si ya dini, bali ni ya kishirikina. Kwa sababu kuna mtu anasema yeye muislamu ama mkristo.
Au kuna mtu ana Phd/ Profesa, ama amesoma elimu nzuri tu ama ana pesa anafanya biashara au mfanyabishara au mwanasiasa mwenye elimu yake nzuri lakini ametumbukia kwenye imani hii ya kishirikina.
Kusoma zaidi ingia http://dewjiblog.com/…/exclusive-interview-ushirikina-chan…/

Wabunge wakamati ya miundo mbinu watembelea mamlaka ya hali ya hewa
Wasira aruhusu uagizaji sukari kutoka nje

Na Humphrey Shao, Dar es Salaam
WAZIRI wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira ameruhusu uagizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchini
Wasira alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Maji na Mifugo juu ya tatizo la kupanda ghafla kwa bei ya sukari tangu kusitishwa kwa uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi.
Waziri huyo alisema wenye viwanda vya sukari pekee hawawezi kupewa kibali cha kuagiza sukari bali ni kwa mfanyabiashara yoyote yule ambaye atakidhi vigezo vitakavyowekwa.
“Nimegundua kuna siasa za sukari ambazo zinaendelea hivyo siwezi kukubali kuona wananchi wanaumia kwa ajili ya kundi la watu wachache ambao walisema wanayo sukari ya kutosha lakini tulipowaita waje kujieleza juu ya kiasi walichonacho wanasema hawana sukari hivyo kwangu naona hizi ni siasa kuliko uhalisia wa soko la sukari lililopo” alisema Wasira.
Katika ufafanuzi huo, Wasira alisema ameiagiza Bodi ya sukari kuweka vigezo vya watu watakaoweza kununu sukari kutoka popote pale duniani wafanye hivyo.
“Baada ya kuzuia kuingia kwa sukari ya nje wauzaji wa ndani waliweza kupandisha sukari ikawa bei juu kwa muda mfupi na tulivyo wauliza walisema sukari imewaishia hawana kabisa katika maghala yao” alisema.
Wasira alisisitiza msimamo wa serikali kuwa ni  kuhakikisha sukari inapatikana nchini kwa bei nzuri na kutoa mifano kuwa mtu aliyepo Mwanza hawezi kununu sukari kutoka Kagera kwa bei ya juu wala mtu wa Morogoro hapashwi kununua sukari kwa bei ya Sh. 2,200 kama ilivyo sasa.

Aliongeza kuwa serikali imekwishafanya mazungumzo na Kamishna wa TRA kuhakikisha sukari iliyozuiwa kwenye maghala inalipiwa kodi na kufika kwa wananchi ili kupunguza tatizo la sukari nchini.


Wanafunzi St Glory wafanya usafai eneo la michungwani Kimara
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA PILI WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Kamishina Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya, wakati walipokutana baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Burn Ltd, Malaczynski Burn, baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia alipokuwa akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia alipokuwa akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia alipokuwa akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.

Muonekano wa Daraja la Kimara mwisho ambapo mradi wa mabasi ya mwendo kasi yatakapokuwa yanishia
Makonda watwangana makonde kariakooJoti amtolea macho Rachel wa kizunguzungu

 Joti akimsalimia rachel
 Joti akimtizama rachel kwa jicho la mahaba
akitaka kuchukua simu hili aandike namba yake ya simu hili apigiwe

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...