Saturday, March 28, 2015

cbe yawakutanisha walimu juu ya mtaa wa biashara

 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema akizungumza  wakati  wa mkutano wa wadau na wataalam wa elimu kutoka Taasisi za Elimu, vyuo, walimu wa masomo ya Biashara wa shule za Sekondari  waliokutana kupitia Mtaala wa kufundishia mafunzo ya taaluma ya Ualimu katika Biashara leo jijini Dar es salaam.

 Menejimenti na watendaji wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa wadau na wataalam wa elimu kutoka Taasisi za Elimu, vyuo, walimu wa masomo ya Biashara wa shule za Sekondari na vyuo na  wadau mbalimbali wa Elimu leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Mafunzo ya awali wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Esther Mbise akitoa ufafanuzi kwa wadau wa Elimu kuhusu uandaaji wa mtaala wa kufundishia walimu wa masomo ya Biashara leo jijini Dar es salaam.

Gwajima alivyojisalimisha kituo cha Polisi

 Askofu gwajima akishuka ndani ya gari
 Askofu gwajima akiongozana na wanasheria wake kuelekea Polisi akitokea mtaa wa Samora

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, jana alijisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam na kuhojiwa kwa zaidi ya saa tano kuhusu kauli kali alizozitoa dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Askofu Gwajima alifika kituo cha polisi majira ya saa 8:22 mchana akitembea kwa miguu na kueleza kuwa amechelewa kwa sababu ya foleni kali iliyokuwepo barabarani.
Wakati akiingia kituoni hapo, Askofu Gwajima alikuwa ameongozana na Mwanasheria wake, John Malya pamoja na baadhi ya waumini wa kanisa analoliongoza.

Kabla ya kuingia ndani kwa ajili ya mahojiano, Askofu Gwajima alizungumza na waandishi na habari na kueleza kuwa ameshangazwa na wito alioupata kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alimtuhumu kumtukana na kumkashafu Kardinali Pengo wakati alikuwa akitekeleza kazi ya kitume.

Askofu Gwajima aliwaambia waandishi wa habari kuwa kauli yake ambayo imesambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii aliitoa baada ya Kardinali Pengo kuwageuka wenzake katika Baraza la Maaskofu Tanzania linalounganisha maaskofu wa Kanisa Katoliki, Pentekoste na Jumuiya ya Kikristo Tanzania.

“Maaskofu wote kwa pamoja tulikubaliana kuwa hawataki Mahakama ya Kadhi na tulisaini tamko na alikubali lakini nashangaa alitugeuka.

“Mimi kama kiongozi wa kiroho nikaona nimkemee kiongozi mwenzangu wa kiroho aache mambo ambayo si mazuri. Hakuna maneno ya kashfa ambayo nimeyatoa. Niliyoyatoa ni maneno ya Mungu yanayotumiwa kumwongoza mtumishi wa Mungu,” alisema Gwajima.

Baada ya Askofu Gwajima kuingia polisi, Kamanda Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa ametii amri ya jeshi hilo kama alivyotakiwa.

Kamanda Kova alitafanyiwa mahojiano katika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam SACP, Costantine Massawe.

Alizitaja tuhuma zinazomkabili Askofu Gwajima kuwa ni kumkashfu na kumtukana hadharani kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Kardinali Pengo.

“Taratibu za kuhojiwa zinafanyika kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa atapewa haki zote anazostahili ikiwemo kuwa na ndugu yake wa karibu, rafiki anayemwamini au wakili wake.

“Kama ilivyo kawaida utakusanywa ushahidi kutoka pande zote za shauri hilo ili kubaini ukweli wa jinsi tukio hilo lilivyotokea,” alisema Kova.

Kova alisema baada ya kukamilika taratibu za awali, zitafuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kupata maoni ya kitaalamu na ya kisheria ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka.

“Ili ufanisi upatikane katika upelelezi wa shauri hili ni muhimu kupata ushirikiano kutoka kwa kila atakayetakiwa kulisaidia Jeshi la Polisi kukamilisha haraka upelelezi wa shauri hili ambalo limepata mvuto mkubwa kwenye jamii,” alisema Kova.

Kwa takribani wiki moja sasa Askofu Gwajima amekuwa akisikika katika mitandao mbalimbali ya kijamii akitoa lugha kali dhidi ya Kardinali Pengo anayemtuhumu kuwasaliti maaskofu wenzake dhidi ya msimamo walioufukia kwa pamoja kuhusu upigaji kura ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa.

Askofu Gwajima katika matamshi yake anamtuhumu Kardinali Pengo kusaliti Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kuwataka waumini waisome Katiba Inayopendekezwa kisha wapewe uhuru wa kupiga kura ya ndiyo au hapana tofauti na azimio la pamoja la maaskofu hao. waandishi mbalimbali wa habari wakijaribu kutafuta picha za tukio hilo

 Gwajima akihojiwa na vyombo mbalimbali vya habari kabla ya kuingia ukumbini

 wafuasi wake waliokuwa nje

Friday, March 27, 2015

Nape ashusha Pumzi kwa LowasaKATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amempongeza Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa
Monduli Edward Lowassa kwa kukubali kuyasitisha makundi ya Watanzania wanaokwenda nyumbani kwake kumshawishi agombee
urais Oktoba 31, mwaka huu.
Lowassa anayetajwa kugombea urais mwaka huu amekuwa akipokea makundi tofauti ya wananchi nyumbani kwake Dodoma yanayokwnda kumshawishi atangaze nia pindi muda utakapowadia.
Juzi Lowassa akipokea kundi jongine LA vijana waendesha pikipiki bodaboda kutoka wilayani Mbarari mkoan Mbeya   fananisha makundi yanayokwenda kumshawishi sawa na mafuriko hivyo hawezi kuyazuia kwa mkono.
Akizungumzia uamuzi huo wa Lowassa wa kusitisha kuyapokea makundi hayo wilayani hapa Nape alimpongeza kwa kukubali kutii maagizo ya Chama pamoja na kanuni zinazokiongoza Chama hicho.
"Nampongeza Lowassa kwa kukubali kuheshimu kanuni, taratibu na Katiba ya chama ambayo ndio inatakiwa kufuatwa na kila mmoja ndani ya chama.
"Alichokuwa anafanya lowassa ni kufanya kuanza kampeni kabla ya wakati
na kwa mujibu wa chama chetu ni makosa maana anakiuka taratibu na
kanuni za chama.Hatuwezi kukaa kimya wakati kanuni zinavunjwa.hivyo
nimpongeze lowassa kwa kutii agizo la chama,"alisema nape.
Akizungumzia kuhusu wapambe wa makada wa wanaotaka urais, aliwataka  makada wote wanataka kugombea urais kupitia chama hicho wawe makini na
wapambe wao.
Nape alifafanua kuwa ni vyema makada wanaotaka kugombea urais wakawa makini na ushauri unaotolewa na washauri au wapambe wao kwani unaweza kuwasababisha kupoteza sifa ndani ya CCM.
"Nawashauri wote wanaotaka kugombea urais wasiwasikilize wapambe
kwani ushauri mwingine unaweza
kuwakosesha sifa za kugombea  nafasi ya urais,"alisema Nape na kuongeza:
"Na hili si kwa wapambe wa Lowassa tu, bali ni kwa wapambe wa makada wore ndani ya CCM,"alisema.
Akisisitiza kuhusu CCM kutenda haki Nape alisema kwamba Chama hicho kitahakikisha kinatenda haki kwa  kila anayeomba nafasi na hakuna ambaye
atanyimwa haki yake.
Alisema kwa wote ambao watakuwa makini katika kuzingatia kanuni na
taratibu za chama haki zao zitalindwa lakini wale ambao watakiuka kwa
maksudi hao hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
"Tunaendelea kuwakumbusha makada wote kuzingatia kanuni na
Katiba ya chama.Kinyume cha hapo watakuwa wanajinyima haki ya
kuomba ridhaa ya kugombea kupitia Chama cha Mapinduzi,"alisema Nape.

Mkuu wa wilaya ya Ileje Rozimary Sinyamule awaasa Vijana kujikita katika shughuli za Maendeleo


 


Na;Daniel  Mwambene,Ileje      Vijana

Mkuu wa wilaya ya Ileje amewataka vijana wilayani humo kuondoa tofauti zao za kisiasa badala yake wajikite katika ujenzi wa misingi ya Ileje ijayo itakayokwenda sambasamba kimaendeleo na wilaya zingine hapa nchini.


Akizungumza na vijana wa mji wa Itumba na Isongole kwa nyakati tofauti Mkuu huyo wa Wilaya Bi; Rozimary Sinyamule amesema tofauti za kisiasa kamwe zisiwe chanzo cha kuwagawa vijana kwani mahitaji yao ni ya aina moja.


Alisema malalamiko kutoka kwa vijana wa vyama vyote vya siasa hapa wilayani hayatofautiani kati yachama kimoja na chama kingine,hivyo ujana huo hauna budi kuwaunganisha katikakuipigania wilaya hiyo kimaendeleo.


Alisema  vijana wanaweza kuchukua hatua za ukombozi ikiwa ni pamoja na kuunganisha nguvu  zao katika kupigania haki zao kwa kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa katika Uchaguzi Mkuuu ujao.


Bi;Sinyamule aliongeza kuwa vijana wamekuwa wakipinga kuitwa ni taifa la kesho wakitaka waitwe taifa la leo, uchuguzi wa mwaka huu iwe njia ya kuwaingiza katika nafasi za uongozi katika ngazi ya wilaya na taifa ili kupaza sauti zao.


Vijana kwa upande wao walimwomba Mkuu huyo wa Wilaya ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi   


na usalama wa wilaya kukemea vitendo vya ubaguzi vinavyofanywa na jeshi la polisi wakati wa sherehe za Krismas na mwaka mpya ambapo jeshi hilo linatuhumiwa kuvuruga sherehe hizi katika mij wa Isongole huku vijana wa mji wa Itumba wakiachwa kuserekea.


Hii ni mara ya pili kwa uongozi wa juu kupokea kero kama hiyo kwani siku kadhaa zilizopita wakazi wakiji hicho walimweleza  Mkuu wapolisi wa Wilaya hiyo Afande Fabin Masaka juu ya kero hiyo.


Mkuu huyo wa wilaya amekuwa akifanyaziara katika maeneo mbalimbali ya wilaya yake akipokea kero na matatizo mblimbali ya wananchi  huku akiwaimiza watumishi wa serikali kutokuwa vyanzo vya kero hizoIkumbukwe kuwa katika uchuguzi wa serikali za mitaa  uliopita vyama vya upinzani wilayani humo vilijiongezea viti vya uenyekiti wa vijiji kutokakiti kimoja na kupata viti zaidi ya 20.


Wachezaji wa kigeni wanaosumbuliwa na Imani za kishirikina VPLNa Humphrey Shao, Dar es Salaam
LiGI kuu wa Soka Tanzania bara ni moja kati ya ligi inayovutia wachezaji wengi wa kigeni hapa nchini hasa wachezaji kutoka nchi za afrika mashariki na kati.

Ligi hii imekuwa kivutio kikubwa kutokana na malipo wanayopata wachezaji wa kigeni ambao wanachezea timu hizi kulinganisha na nchio wanazotoka.
Licha yakuwa na uwezo wachezaji hawa wamekuwa na mtihani mkubwa wa kukumbana na utamdauni usioshikika kutoka kwa wachezaji wanao wakuta hama uongozi wa timu hali inayofanya washindwe kuonesha kipaji chao kama ipasavyo.

Hivyo leo hii najaribu kukuchambulia wachezaji wachache kutoka nje ya Tanzania ambao wamekutana na kigingi hichi cha imani ya kishirikina katika timu zao.

Daniel Serunkuma -Simba
Huyu ni moja wachezaji ambao walinunuliwa kwa fedha nyingi kutoka klabu ya Golmahia ya Kenya akiwa mfungaji bora nakujiunga na Simba katika mzunguko wa pili waligi kuu ya Tanzania bara.

Licha ya watu kuwa na imani na mchezaji huyo bado ameshindw akuonyesha kile ambacho watu walitegemea kukipata kutoka kwake hilikusadia timu hiyo kufanya vyema kwenye ligi

Serunkuma ambaye hivikaribuni alipata ofa ya mapumziko ya siku chache kwenda kwao aliweza kuandikwa katika vyombo vya habari kuwa ameishutumu klabu yake ya Simba kuwa kuna ushirikina unaomfanya ashindwe kufanya vizuri uwanjani.
Per Sherman- Yanga
Mchezaji huyu mwenye umbo zuri na la kuvutia na madaa ya kumiliki mpira alisajiliwa na klabu ya Yanga akitokea nchini Liberia ameshindwa kufurukuta katika ligi kuu.
Shermana ambaye anasema kuwa amini juu ya kiwango anachokionyesha katika klabu ya Yanga hivyo yeye anamuachia mungu na ipo siku akiondoka watamuelewa tu.
Anasema kuwa huko alikokuwa akicheza alikuwa ni mchezaji mzuri sana lakini cha ajabu kila anapokuwa uwanjani na timu ya Yanga uw anajiona tofauti na kushindw kufanya vile vitu vinavyotakiwa hivyo kusema kuwa yeye katika hilo anamuachia mungu atalimaliza.

Andrew Countinho-Yanga
Huyu ni winga wa timu ya Yanga ambaye aliweza kujiunga na klabu hiyo akitokea nchini brazil mara baada ya kuletwa na kocha kutoka Brazil Marcio Maximo.
Countinho licha ya kufanya vizuri katika michezo yake ya awali  lakini ameshindwa kufurukuta katika mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara mara baada ya kuandamwana magonjw ayasiyoamazika.
Mchezaji huyu mwenye uwezo wa hali ya juu anasema kwa staili hiyo ya kuumwa umwa yuko tayari kucheza hata JKT Ruvu kuliko alipo hapo sasa kikubwa kwake ni kuchez anje ya Brazil.

Emmanuel Okwi-Simba
Licha ya mchezaji huyu kuwa tegemeo kubwakatika klabu yake bado anatajwa kuwa si mchezaji aliyeweza kuipatia goli timu yake nje ya uwanja wa Taifa Dar es Salaam tangu kuanza kwa ligi kuu ya Vodacom.

Okwi ambaye alijiunga na Simba akitokea Yanga huku wazee wa klabu hiyo kuapa kuwa atofanya vizuri huko anakokwenda mpaka pale atakporejesha fedaha na kuwaomba msamaha mashabiki na wapenzi wa klbau hiyo.
Didier Kavumbagu-Azam
Huyu ni mshambuliaji wa Azam Fc ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Yanga mara baada ya kusitishiwa mkataba wake .

Kavumbagu amekuwa akifanya vizuri na klabu ya Azam aliwahi kukariri wana chombo kimoja cha habari kuwa kilichokuwa kinafanyika yanga yeye alewi lakini yeye anamini kuwa kuna mchezo mchafu ulikuwa unafanyika juu yake .
MWISHOTAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...