Thursday, April 16, 2015

Wema: Kumuimba msichana uliyeachana nae ni ushamba


NA RHOBI CHACHA
STAA wa filamu za kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amesema ni ushamba kwa wasanii wa muziki kuwatungia nyimbo za majungu wasichana wanaoachana nao kimapenzi.
Wema wasanii wengi wa muziki wamekuwa na tabia ya kishamba ya kutunga nyimbo zenye maneno ya kuudhi wakiwalenga waliokuwa wapenzi wao.
“Ni ushamba wa mapenzi, haiwezekana mlikuwa mnafurahia wote mapenzi yenu lakini mkiachana anakutungia wimbo za kukuponda hakuna neo la kuzungumzia hilo zaidi ya kuita ushamba kwa wasanii wa aina hiyo,’’ alisema Wema
Hata hivyo kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani kutoka studio moja kubwa ya kurekodi muziki nchini kuna wimbo wa wasanii wawili waliowahi kuimba pamoja na wimbo wao ukawa gumzo kwa mashabiki wa muziki huo wanamalizia kurekodi wimbo unaodaiwa unamzungumzia mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006.

S.H AMON , MAMA RWAKATALE WAFIKISHW AMAHAKAMANI KWA UKWEPAJI KODI YA MAJENGOWIZARA ya Ardhi  Nyumba na Maendeleo ya makazi imewafikisha mahakamani mashauri 120 ya ukwepaji kodi wa ardhi wakiwemo na bahadhi ya vigogo na wafanyabiashara wakubwa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam janaMwenyekiti wa mahakama hiyo kanda ya Ilala Yose Mlyambha alikiri kupokea mashtaka hayo kutoka kwa kamishna wa ardhi kwa hati ya dharura ambayo inawap nguvu ya kuwashitaki bila yakuw ana utetezi.
Wakati akiendesha mashtaka hayo mwenyekiti huyo aliwataja bahadhi ya wastakiwa ambao walitakiw akatika kesi hiyo ni , S.H. Amon enterprises, Murzah Company, St Mary Internationa Academy  na wengine.

“Yapo majina ya vigogona tasisi kubwa tu za dini na mashirika yasiyo ya kiserikalia mbayo  yamo katika orodha ya watu wanaostakiwa na Kamishna wa ardhi hivyo wakati ukifika nitawataja hila hao wengine mmewaona wenyewe walipokuja kusikiliza ushahidi wao”alisema Mlyambha.

ambao atawataja pindi watakapo pandishw akizimbani.

Mlyambha alisema kuwa kamishna amewafikishakatika mahakama hiyo kwa ajili ya kulinda na kutetea masalhi ya wanyonge kwa kuwa kwa mujibu wa sheria ni kosa kwa mtu yoyote kukwepa kulipa kodi ya aina yoyote ile alipaswa kulipa.

Alisema ukusanywaji wa kodi ndio msingi mkubwa wamaendeleo ya nchi hivyo kila mmoja anapswa kuwa makini na jambo hili kwani watu wengi wamekuwa wa kikwepa ulipaji wa kodi ya majengo na kuona aina msingi kiasi mtu anafikia kuadaiwa mpaka milioni 38.MSAGA SUMU APAGAWISHA UZINDUZI WA MTEMVU CUP

 MSAGA SUMU AKIFANYA YAKE JUKWAANI
 WA MAMA WA TEMEKE WAKIBURUDIKA NA KIGODORO CHA MSAGA SUMU
 KATIBU WA UWT TEMEKE AKIPAGAWA NA MSAGA SUMU
MSAGA SUMU

DAKTARI ASEMA MAHAKAMANI ATUKUMPIMA MTOTO ALIYEBAKWA NA MBASHA

 ile kesi inayomkabili muimbaji wa nyimbo za injili Emanuel Mbasha imeanza kuzaa sura mpya mara baada ya Daktari aliyefika kutoa ushahidi mahakamni leo kusema kuwa mtoto huyo anayesadikiwa kuwa alipabakwa akupelekwa chumba cha maabara kwa ajili ya vipimo kwa wakati muafaka.

akizungumza na mwandishi wa blog ya jijiletu blog .blogsport.com alisema kuwa mtoto huyo amabye anasadikiwa kuwa alibakjwa alipelekwa Hospitali siku ya kwanza kisha kuangaliwa kwenye machao na kuwamuru kuwa waende maabara kwa ajili ya vipimo lakini  ndugu zake na flora awakuweza kufanya na mataokeo yake wakaenda nyumbani na kurudi siku ya nane kwa ajili ya kuchukua vipimo vya kujua kuwa binti huyo amebakwa ama laa

kwa mujibu wa daktari huyo alisema kuwa hivyo ilikuwa ni vigumu kupata ushahidi wa moja kw amoja kuwa alibakw akutokana na ndugu zake hao kukaidi agizo la awali la kitaalamu juu ya swala hilo.

MTEMVU CUP YAZINDULIWA RASMI TANDIKA MWEMBE YANGA Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akiwa na msaidizi wake Piter

 kikundi cha Hamasa cha CCM Temeke kikifanya yake
 Bwanga maratibu mashindano hayoa akifatilia mashindano hayo kwa makini
Mke wa Mbunege wa Temeke Abbas Mtemvu akiwa na katibu wa UWT Temeke wakicheza kigodoro

Tuesday, April 14, 2015

Kocha Kagera Sugara alomwa faini ya 500,000KAMATI YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI YA BODI YA LIGI

Kocha Jackson Mayanja wa Kagera Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kutoa lugha ya kashfa kwa maneno na vitendo kwa waamuzi wa mechi yao na Mtibwa Sugar kuwa walipewa rushwa.


Adhabu dhidi ya Kocha Mayanja kwenye mechi hiyo namba 136 iliyochezwa Aprili 1, 2015 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 40(1) ya Ligi Kuu.


Klabu ya Mtibwa Sugar imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya timu yake kukataa kuingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi namba 142 dhidi ya Stand United iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.  Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.


Nayo Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu baada ya timu yao kugoma kuingia kwenye vyumba vya kuvalia nguo (changing room) kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar. Hatua hiyo ilisababisha wachezaji wakaguliwe kwenye gari lao.


Pia Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kuzingatia kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu baada ya vilevile kugoma kuingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo hiyo namba 146 iliyochezwa Aprili 6, 2015.


Kipa Tony Kavishe wa Polisi Morogoro amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga ngumi mwamuzi msaidizi namba mbili, Hassan Zani kwa kuzingatia kanuni ya 37(5) ya Ligi Kuu. Alifanya kosa hilo kwenye mechi namba 147 dhidi ya Mgambo Shooting iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.KAMATI YA MASHINDANO TFF

Kamati ya Mashindano ya TFF ilikutana jana kupitia maandalizi ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) pamoja na taarifa ya Ligi Daraja la Pili (SDL) iliyomalizika hivi karibuni.


Katika matukio ya SDL, Kamati imeipiga faini ya sh. 300,000 timu ya JKT Rwamkoma ya Mara kwa kusababisha mechi yake dhidi ya AFC ya Arusha kuvurugika. Adhabu hiyo kwa mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 28(4) ya Ligi Daraja la Pili.


Nao makocha wa JKT Rwamkoma, Hassan Makame na Kamara Kadede wamepigwa faini ya sh. 200,000 kila mmoja na kufungiwa mechi sita kwa kumshambulia mwamuzi msaidizi namba moja katika mechi hiyo iliyochezwa Machi 9, 2015.


Wachezaji Shafii Maganga, Saleh Ali, Ismail Salim na Mussa Senyange wa JKT Rwamkoma ambao wanatuhumiwa kwa kushambulia mwamuzi kwenye mechi hiyo suala lao linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa hatua zaidi.


VPL KUENDELEA KESHO

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho jumatano katika viwanja viwili nchini, jijini Tanga wenyeji Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribisha timu ya Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani.


Mjini Morogoro wakata miwa wa Mtibwa Sugar watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la Magereza nchini timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya, mchezo utakaopigwa katika dimba la Manungu Turiani.TTF YAFUNGUA SEMINA YA WAAMUZI VIJANA

Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine leo amefungua rasmi semina ya waamuzi vijana wenye umri wa miaka 12- 17, inayofanyika katika hostel za TFF zilizopo Karume.


Akiongea na waandishi wa habari, Mwesigwa amesema semina hiyo ya vijana imejumuisha vijana 27 kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaandaa kuwa waamuzi wa kimataifa baadae.


Vijana hawa mnaowaona hapa wanatoka katika viuto vya kufundishia waamuzi vijana nchini, wakikua na kufuata misingi ya kazi baadae watakua waamuzi bor nchini kwa sababu watakua wameanza tangu wadogo na kufuata maelekezo ya wakufunzi wao.


Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi nchin Bw. Salum Chama akiongea na wandishi wa habari kabla ya kumkaribisha katibu mkuu, amesema malengo yao ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na waamuzi wa kimataifa wengi.


Mwaka huu Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa kutoa waamuzi 18 wenye beji za FIFA barani Afrika, nyuma ya Misri yenye waamuzi 22, Lengo ni kuhakikisha tunawaanda vijana wengi waje kuwa waamuzi wa kimataifa.


Semina hiyo ya siku 5 inatarajiwa kufungwa ijumaa tarehe  17 Mei, 2015 inajumuisha vijana kutoka mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Zanzibar, Mwanza, Arusha na Mbeya, kati ya vijana 37 waamuzi wawili ni wanawake.


Wakufunzi wa semina hiyo ni Soud Abdi, Riziki Majala na Joan Minja.IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


Ismail amuanika Mpenzi wakeNa Humphrey Shao, Dar es Salaam


MWANAMUZIKI mahiri wa muziki wa kizazi kipya na wa asili kutoka bendi ya Mjomba Ismail ameweza kumuanika wazi kipenzi chake ambacho kina sumbua roho yake.


Ismaili ambaye ailonkena mara kadhaa katika viwanja vya chuo kikuu cha mwalimu nyeyere akliwa ameketi na mdada huyo ambaye jina lake alikuweza kufahamika huku wakicheka na kunywa kila naposhuka kuimba


 


Wakati akifanya hivyo vyote kamera yetu ilimnasa na picha hizo hapo chini

Rais Kikwete azindua Kibweta Cha mwalimu

 Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Fimbo Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Pius Msekwa, kama isharaya kumsimika kuwa mwenyekiti wa kwanza wa Kibweta cha Mwalimu Nyerere katika hafla uzinduzi wa kozi maalumu ya maadaili katika chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.Picha na Humphrey Shao


Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kibweta cha mwalimu katika chuo kikuu cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam. Picha na Humphrey Shao
Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kibweta cha mwalimu katika chuo kikuu cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam. huku mvua ikiwa inanyesha Rais Jakaya Kikwete, akizungumza jambO wakati wa uzinduzi  Kibweta cha Mwalimu Nyerere huku Mwenyekiti wa Kibweta hicho , Pius Msekwa akifatilia kwa makini. Picha na Humphrey Shao

 askari akiimarisha uliniz huku mvua ikiwa inanyesha


BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...