Friday, May 1, 2015

Clinton

"On Clinton's age, Republican rivals imply -- but never say -- she's old" - http://www.reuters.com/article/idUSKBN0NM34V20150501

Tetemeko la ardhi Nepal

"Nepal quake toll passes 6,200, $2 billion needed for reconstruction" - http://www.reuters.com/article/idUSKBN0NI12120150501

Thursday, April 30, 2015

SunnrgySystem Limited Yaleta pampu mpya za kusukumia maji kwa njia ya Niashati jua

 Mkurugenzi wa Sunnrgy Energy Limited Sajjad Dharans  akiwa a Kamishana wa majina
 Mhandisi Erick Mhema akiwa eleza wadau mbalimbali namna mashine hizo zinazofanya kazi
 Moja ya mashine ya mfano inayotumia programu ya simu ya Android

Madam Ritha Uso kwa Uso na Zito kwenye Msiba wa Hashim Mbita

 Madam Ritha akiwa na waombolezaji wengine

 Askari wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu
 Bibi akiwa jiwezi akisaidiw ana askari
 Rais Kikwete akiwa mwenye majozni na mkewe Mama Salma Kikwete

Madam Ritha akiwa na Zito Kabwe
Wakiteta jambo na Zito Kabwe

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA DHARURA WA VIONGOZI WA NCHI NA SERIKALI WANACHAMA WA SADC KUHUSU UENDELEZAJI VIWANDA, HARARE ZIMBABWE


Baadhi ya Mawaziri wa Tanzania, waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, wakati akisoma hotuba ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR
 Rais Robert Mugabe akihutubia mkutano huo

 HARARE, ZIMBABWE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatano Aprili 29, 2015, ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa dharura wa Umoja wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Harare, chini ya Uenyekiti wa Rais Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe, Mwenyekiti wa sasa wa SADC pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU). Mkutano huo wa siku moja pia umehudhuriwa na Rais Seretse Ian Khama, Rais wa Botswana na Makamu Mwenyekiti wa SADC, Mfalme Muswati III wa Swaziland, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, Rais wa Namibia Hage Geingob, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Lesotho Pakalitha Mosisili, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na Rais wa Zambia Edgar Lungu.
Awali akifungua mkutano huo Rais Mugabe alisisitiza umuhimu wa nchi za SADC kuwa na mpango madhubuti wa Viwanda kwa kuwa uwepo wa viwanda utasaidia kupunguza tatizo kubwa linalozikabili nchi hizi hasa ajira, pamoja na uchumi duni unaotokana na ukosefu wa viwanda vya kuboresha bidhaa zinazozalishwa katika nchi za ukanda huu. Mkakati huu uliopitishwa na Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaanza mwaka huu 2015 hadi mwaka 2063. Katika mkakati huu nchi za SADC zinalenga kutanua uhuru wa soko katika utatu wa kanda za Kibiashara yaani SADC, EAC na COMESA ikiwa ni pamoja na kutenga eneo huru la ukanda wa kiuchumi wa nchi za kanda hizi, huku lengo likiwa kufanikiwa upatikanaji wa eneo huru la ukanda wa biashara kwa nchi za Afrika. Masuala mengine ni pamoja na kukuza bidhaa zinazozalishwa katika nchi hizi katika masoko ya Asia ambao ni walaji na watumaji wakubwa wa malighafi zinazozalishwa katika nchi hizi.
Rais Mugabe alifafanua pia kuwa, nchi hizi kwa umoja wake zikiunganishwa utakuta ndizo zina rasimali kubwa ya madini ya Dhahabu, Almasi na hata Gesi na kwamba kama mtengamano huu utakamilika nguvu ya pamoja inaweza kugeuza hali ya maisha ya wananchi wa nchi hizi sambamba na maendeleo ya kiuchumi katika nchi hizo.
Awali akizungumza kabla ya hotuba ya ufunguzi ya Rais Mugabe, Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stargomena Lawrence Tax aliishukuru serikali ya Zimbabwe kwa maandalizi mazuri ya mkutano huu ambao ulikuwa ni mwendelezo wa ule uliofanyika Victoria Falls, Zimbabwe Agosti 17, 2014 mkutano uliotaka nchi wanachama wa SADC pamoja na kupitisha mkakati wake wa Kimaendeleo, upange dira ya utanuaji na uendedlezaji viwanda katika ukanda huu.
Matukio mengine katika mkutano huu ni pamoja na makabidhiano ya Kituo cha Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, makabidhiano yaliyofanywa na nchi ya Zimbabwe chini ya Rais wake Robert Mugabe kwa Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt Stargomena Tax. Kufuatia makabidhiano haya, Chuo hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na matumizi yake yatahusisha vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na masuala ya utunzaji amani ndani ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya kuboresha kazi zao kufuatia migogoro kuwa mingi katika nchi mbalimbali Afrika.
Pia Rais Mugabe alitumia muda huo kuutaka Mkutano huu wa Dharura kutoa heshima zao kufuatia kifo cha Brigedia Jenerali Hashim Mbita aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Ukombozi kwa kutambua mchango wake katika uhuru wa nchi zilizomo SADC na pia mchango wake kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizi. Raia Mugabe alimtaja Hayati Brigedia Mbita kama mpiganaji mahiri na kiongozi aliyefanya kazi kwa maslahi ya watu wengi bila kuchoka na kwamba Afrika na SADC vitamkumbuka daima kwa mchango wake huo.
Imetolewa na:    Ofisi ya Makamu wa Rais
                                 Harare, Zimbabwe
                                       Aprili 29, 2015
9 Attachments
Preview attachment 02.jpg
Preview attachment 2.jpg
Preview attachment 03.jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake katika Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Jijini Harare, Zimbabwe, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR

Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Janeth Mbene afanya ziara mtaa wa Viwanda Sido

 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janeth Mbene akiasalimiana na naibu waziri wa kazi na Ajira Makongoro Mahanga
 Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Janeth Mbene akiteta jambo na Naibu waziri wa Kazi na Ajira Makongoro Mahanga katikati ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala na Diwani wa Vingunguti Asaa Simba
 Naibu waziri wa Viwanda na biashara akipata maelezo kutoka kwa mkurugezni wa sido Omar Bakari
 Janeth Mbene akisalimiana na moja ya walemavu wanaomiliki kiwanda  cha baiskeli za walemavu
 Janeth Mbene akiangalia mashine ya kutengeneza chakula cha Samaki
 Janeth Mbene akiangali nguo iliyotengenezwa kwa malighafi za asili
 Janeth aMbene akiwa na mgunduzi wa Sindano ya maajabu
Naibu waziri wa kazi , Makongoro mahanaga akiangalia moja ya Baiskeli zilizotengenezwa na walemavu

Wednesday, April 29, 2015

Mbita ahagwa rasmi Lugalo

Atimaye  mwili wa marehemu brigedia jenerali hashim mbita umeagwa rasmi na kupewa hashima za kijeshi katika hospitali ya  jeshi lugalo

Katika shughuli  hiyo Rais kikwete aliongoza Maria ya waombolezaji kutoka nchini msalimie msalimie barani Afrika


Mazishi ya Hashim Mbita Lugalo


Tuesday, April 28, 2015

Madam Ritha bongostar search itaanza soon

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Benchmark production Ritha Paulsen ametangaza kuwa ule wa kusaka vipaji vya uimbaji maarufu kama bongostar utaanza mapema kuanzia sasa

Madam Ritha Alisema hayo alipokutana na mtoto wa temeke na kumueleza ni namba gani wanajipanga kuanza mapema mwaka huu

"Najua watu wanakiu ya shindano kwasasa kwani awajapata kuona shamra shamra kama za miaka iliyopita lakini lazima wajue Muda  huu  ni kiboko ya zote walizopata kuonan"alisema Madam Ritha

Hivyo alitoa wito kwa vijana wenye vipaji kuanza kujinoa kwa ajili ya michuano huu


Mkapa awafariji watoto wa hashim mbita

Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin mkapa akisaini kitabu cha maombolezo wakati alipofika kutoa pole

kwa ndugu wa marehemu brigedia jenerali hashim mbita chang'ombe na ngeme mbita ambaye ndio mjane wa marehemu


Tff ya ipongeza yanga kwa ubingwa

Shirikisho


Monday, April 27, 2015

Wakufunzi CCP watakiwa kufanya kazi kwa welediNaibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahmani Kaniki akisalimiana na baadhi ya Wakufunzi wa chuo cha Polisi Moshi (CCP) wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua mafunzo yanayoendelea chuoni hapo.Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Matanga Mbushi.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)


 
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahmani Kaniki (kushoto) akiwasili katika chuo cha Polisi Moshi (CCP) wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua mafunzo yanayoendelea chuoni hapo.Katikati ni Mkuu wa Chuo hicho, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Matanga Mbushi na Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna Omar Rashid (Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)

 
 
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Moshi.
 
Wakufunzi wa Chuo cha Polisi Moshi (CCP) wametakiwa kuendelea kutoa mafunzo kwa weledi ili kuweza kupata askari bora ambao watashirikiana na jamii katika kupambana na uhalifu hasa katika kipindi hiki ambapo kumeibuka uhalifu mpya kwa njia ya mitandao na unaovuka mipaka.
 
Wito huo umetolewa jana mjini moshi na Naibu Inspekta Jenerali wa  Polisi, Abdulrahman Kaniki wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi chuoni hapo ambapo alizungumza na wakufunzi hao na kuweka mikakati mbalilmbali ya kuboresha mafunzo katika chuo hicho.
 
Naibu IGP Kaniki alisema, askari wakipata mafunzo bora wataongeza mbinu zitakazowezesha kukabiliana na  uhalifu huo na hivyo kuendelea kuimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kushirikiana na jamii ambayo imekuwa msaada mkubwa wa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.
 
“Ili kuhakikisha kwamba raia wa Tanzania na mali zao wanalindwa ipasavyo, Jeshi la Polisi hatuna budi kuendelea kubuni mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu wa kila aina unaobadilika mara kwa mara na hilo linawezekana kwa kuendelea kuwapatia askari wetu mafunzo yenye viwango vya kupambana na uhalifu unaokua kwa kasi”alisema Kaniki.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Polisi moshi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Matanga Mbushi alisema wanaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa mafunzo wanayotoa yanalenga katika mitaala ambayo wamekuwa wakiiboresha mara kwa mara ili kuendana na wakati kulingana na mazingira ya uhalifu unaotokea katika jamii.
 
Alisema, mbinu za uhalifu zimekuwa zikibadilika kila siku hivyo, na wao kama chuo wamejikita kuhakikisha kuwa askari wanaopita katika chuo hicho wanazipata mbinu mpya na hivyo kuwa zaidi ya wahalifu ili waweze kupambana nao.

Rais Kikwete afika kutoa Salamu za Pole Nyumbani kwa Marehemu, Brigedia Jeneral Hashim Mbita

Kiongozi mkuu wa ACT zito kabwe akitoa pole kwa mke wa marehemu
 Rais Jakaya Kikwete akisaini katika kitabu cha salamu za Rambi rambi
 Rais Kikwete akimsalimia mke wa marehemu Hashim Mbita, Ngeme Shomari Mbita
Rais Kikwete akimuomba akae mke wa marehemu Hashim Mbita ,Ngeme Shomari Mbita
 Rais Kikwete akiapata maelezo kutoka kwa ndugu wa marehemu Hashim Mbita
 Rais kikwete akicheza na mmoja wa wajukuu Marehemu Brigedia Jeneral Hashim Mbita
 Waziri wa mabo ya nje Bernard Membe akitoa pole kwa mke wa marehemu brigedia Jenerali Hashim Mbita
 Katibu mkuu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam akitoa pole kwa watoto wa marehemu
 Balozi wa Afrika Kusini Nchini akitoa pole kwa mke wa marehemu Hashim Mbita na watoto
 Balozi wa Afrika Kusini akisaini kitabu cha wageni


. Nchi mbalimbali za Kusini mwa Afrika zimemlilia marehemu Brigedia Jenerali Hashim Mbita kutokana na mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi hizo ulioratibiwa na Serikali ya Tanzania.
Hashimu Mbita (82) alifariki siku ya Jumapili asubuhi katika hospitali ya Lugalo kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu uliomsumbua kwa miezi nane, huku muda mwingi akilazwa hospitali, na baada ya muda kurejeshwa nyumbani.
Mabalozi kutoka nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Angola na Zambia walifika nyumbani kwa marehemu kuwafariji wafiwa na kumzungumzia Mbita jinsi alivyokuwa na mchango mkubwa katika ukombozi wan chi zao.
Balozi wa Zimbabwe nchini, Edzai Chimonyo alisema marehemu Mbita alikuwa kiini katika mapambano dhidi ya wakoloni walioitawala Zimbabwe kwa muda mrefu na kuwanyonya wananchi wa nchi hiyo.
Chimonyo alisema Mbita alikuwa ni mtu wa kujitolea na alifanya kazi kubwa chini ya maelekezo ya Mwalimu Julius Nyerere. Aliongeza kuwa kumpoteza mtu kama yeye ni pigo kwa Afrika, na kuwa anastahili heshima kubwa.
“Tunafurahi kwa sababu Mbita aliweza kuandika vitabu 9 vyenye historia ya ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika. Tutamkumbuka daima kwa kutuachia historia ya ukombozi katika maandishi kwani vizazi vijavyo vitapata kufahamu historia hiyo,” alisema.
Chimonyo aliongeza kuwa unapozungumzia mchango wa Tanzania katika ukombozi wan chi za kusini mwa Afrika huwezi kuacha kumtaja Mbita kwa sababu alikuwa na mchango mkubwa katika kutekeleza maagizo ya Mwalimu Nyerere.
Ofisa kutoka Ubalozi wa Angola, Joel Cumbo alisema Mbita alikuwa kiungo muhimu katika kupigania uhuru wa Angola. Alisema mbinu na maarifa yake katika mapambano ndiyo yaliyopelekea ushindi dhidi ya mkoloni.
Alisema Angola ilikuwa ikipokea silaha kutoka Urusi kupitia Tanzania. Cumbo aliongeza kuwa mpaka silaha hizo zinaifikia Angola, Mbita ndiye aliyekuwa kiungo na kuwasaidia wanajeshi wa nchi yake mbinu za mapambano.
“Raia wa Angola wanamfahamu vizuri kwa kuwa alikuwa karibu nao katika mapambano dhidi ya mkoloni. Nipo hapa leo kwa niaba ya Serikali ya Angola kutoa pole kwa wanafamilia,” alisema ofisa huyo.

Rai Kikwete akiwa mwenye huzuni huku akipata maelezo kutoka kwa mke wa marehemu Brigedia Jenreali Hashim Mbita, Bi Ngeme Shomari Mbita

WADAU WA MITINDO NA UREMBO WAALIKWA KUSHIRIKI MAONESHO UCHINA

Makamu wa Rais wa Maonyesho ya Wachina Maharufu kama China International Beauty Expo African Hall,Rex Chan akizungumza na Waanddishi w...