Saturday, July 11, 2015

Lowasa mbele kwa mbele nndanya mkutano

Mbunge Wa monduli Edward Lowasa ameonesha kuwa no mwanasiasa mkomavu Mara baada ya kutokataa salami za mahasimu wake Wa kisiasa katoka mchakato Wa kuwsnia Urals ndani ya ccm

Mhindi adakwa na mabilioni mjini Dodoma


TRA yadhamiria kufikia malengo katika ukusanyaji wa kodi


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akiwaeleza wajumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi kuhusu kuanza kutumika kwa sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015 na jinsi itakavyobadilisha baadhi ya mifumo ya kibiashara,wakati wa Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) Leo Jijini Dar es Salaa

Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi Bw.Nicholus Duhia akimshukuru Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade kwa kuhudhuria ufunguzi wa semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) na kuahidi kuwa washiriki wazuri katika mabadiliko katika sekta ya Kodi nchini,wakati wa Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) Leo Jijini Dar es Salaa


1-    Baadhi ya wajumbe wa semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) wakimsikiliza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade
2-    Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akimueleza jambo Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi na mwenyekiti wa Kamati ya sekta ya Umma Bw.Nicholus Duhia, katikati ni Bi. Diana Masalla Meneja Elimu kwa Mlipakodi.
Na Hassan Silayo MAELEZO
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imedhamiria kufikia malengo yake katika ukusanyaji wa kodi ili kuiwezesha serikali kufikia shilingi trilioni 22.3 iliyojiwekea katika bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016.
Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar es Salaam na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade wakati wa Semina ya wahasibu iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) ikiwa na lengo la kujadili kuhusu masuala ya kodi, bajeti na uchumi kwa ujumla.
“Moja kati ya malengo tuliyojiwekea sisi kama mamlaka ni kuisaidia serikali katika ukusanyaji wa mapato tukiwa na lengo la kuiwezesha kufikia kiasi cha shilingi trilioni 22.3 zilizopangwa kutumika katika mwaka huu wa fedha” Alisema Bw.Rished.
Akieleza kuhusu sheria mpya ya kodi iliyoanza kutumika julai 1, 2015 Bw. Rished alisema kuwa kuwa sheria hii inategemewa kubadilisha baadhi ya mifumo ya kibiashara nchini.
Pia alieleza kuwa kitu muhimu kwa sasa ni wajumbe wa bodi hiyo kukaa na kuipitia sheria hiyo na kuangalia mabadiliko yaliyomo na wao kama wadau katika sekta hiyo kusaidia katika kuboresha mazingira ya kibiashara.
Naye Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi Bw.Nicholus Duhia alimshukuru Kamishna Mkuu kuhudhuria semina hiyo na kuahidi kuwa washiriki wazuri katika mabadiliko ya sekta ya Kodi nchini
“Ndugu Kamishna Mkuu, umekuwa ukishirikiana na kufanya kazi kwa karibu na bodi hii, hivyo tunakuahidi baada ya kumaliza semina hii tutakuwa washiriki wazuri hasa katika mabadiliko ya sekta ya Kodi nchini” Alisema Bw. Duhia.
Aidha, Mshiriki wa Mafunzo hayo na muwakilishi kutoka Jubilee Insurance Bi. Hellena Mzena alisema kuwa kikubwa anachotegemea kujifunza kutoka kwenye semina hiyo ni jinsi gani sekta ya Bima ilivyoguswa kwa mara ya kwanza katika Sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la Thamani ya mwaka 2014 na jinsi gani wataenda sambamba na mabadiliko hayo.1-   

  Bw. Yona Kilagane akiwasilisha mada wakati wa Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) Leo Jijini Dar es Salaa.

1-  

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo.

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...