Friday, August 7, 2015

Janet Mbene akabidhi msaada wa vitanda vya kujifungulia vyenye thamani ya Milioni 30 Ileje

 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene,akionyesha baadhi ya vifaa vinavyotumika katika hospital ambavyo avimetolewa na Karemjee Foundation kwa ajili ya Hospital ya Ileje.
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene,akionyesha baadhi ya vifaa vinavyotumika katika hospital ambavyo avimetolewa na Karemjee Foundation kwa ajili ya Hospital ya Ileje.
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimkabidhi Vitanda vya Kujifungulia Katibu wa CCMwilaya ya Ileje, Hamida Mbogo, kwa ajili ya Hospitali za wilaya hiyo.
 .Mafundi wa Hospitala wakiunganisha kitanda cha kujifunguliwa kilicholetwa na Mh Janet Mbene kwa ajili  ya hospitalai za ieleje.
Mganga mkuu wa Wilaya ya ilje akiangalaia sehemu ya msaada wa vitanda uliotolewa na Janet Mbene

POSTA BANK YASAIDIA ILEJE MADAWATI YA MILIONI 3

 Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene, akiwa amekaa kwenye madawati amabayo amekabidhiwa na benki ya Posta kwa ajili ya shule za ileje
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akinyoosha kidiole ishara kama akiwa Darasani mara baada ya kupokea madawati kutoka benki ya Posta
 Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene, akiwa amekaa kwenye madawati amabayo amekabidhiwa na benki ya Posta kwa ajili ya shule za ileje
 Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akipokea madawati kutoka kwa meneja wa Tawi la benki ya Posta Tunduma
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimkabidhi katibu wa CCM Wilaya ya Ileje Hamida Mbogo madawati ya kwa ajili ya shule za sekondari na msingi wilayani ileje ambayo yametolewa na benki Posta Tawi la Tunduma.

Mkwasa aita 29 Kujiunga na Stars

MKWASA ATANGAZA 29 STARS
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 29 watakaongia kambini siku ya Jumapili tarehe 9, Agosti katika hoteli ya Tansoma iliyopoe eneo la Gerezani kwa ajili ya kambi ya wiki moja ya mazoezi.

Katika kikosi hicho alichokitangaza cha wachezaji 29, Mkwasa amewajumuisha wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi (Proffesional), ambao baadae watajumuika kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria mwezi Septemba 2015 nchini Uturuki.

Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi ya siku kumi jijini Istambul - Uturuki, ambapo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria.

Wachezaji watakaongia kambini jumapili ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga SC) na Aishi Manula (Azam FC), walinzi wa pembeni: Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC) na Abdi Banda (Simba SC).

Walinzi wa kati; Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub, Kelvin Yondani (Yanga SC), Viungo wakabaji: Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Viungo washambuliaji ni Salum Telela (Yanga SC) na Said Ndemla (Simba SC).

Washambuliaji wa pembeni; Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke, Saimon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano, Farid Musa (Azam FC), huku washambuliaji wa kati wakiwa ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC).

Wachezaji wa kimataifa waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DR Congo), Mrisho Ngasa (Free State - Afrika Kusini) na Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na Adi Yussuf (Mansfield Town – Uingereza)


DIRISHA LA USAJILI SASA KUFUNGWA AGOSTI 20
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limesogezwa mbele kufungwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji kwa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) mpaka Agosti 20 mwaka huu.

Awali dirisha la usajili lilikua lifungwe leo Agosti 6, na usajili mdogo wa ndani ungefungwa Septemba 5, 2015 lakini sasa usajili wote kwa jumla utafungwa Agosti 20, 2015.

Tarehe 21- 28 Agosti, 2015 ni kipindi cha pingamizi, tarehe 29-30 Agosti 2015, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itapitia na kupitisha usajili.

Dirisha la uhamisho wa wachezaji wa Kiamataifa (FIFA –TMS) litafungwa tarehe 06 Septemba, 2015 na Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12, 2015.

TFF inavitaka vilabu kukamilisha usajili huo katika muda huo uliowekwa, ili kupunguza usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho,na dirisha litakapofungwa Agosti 20, litafunguliwa tena wakati wa dirisha dogo mwezi Novemba 15 mwaka huu.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

VijananchiniwatakiwakujitokezakatikamaadhimishoyaSikuyaVijanaDunia:KatibuMkuuwaWizarayaHabari, Vijana, UtamaduninaMichezoBibi. SihabaNkingaakifanyamahojianomaalumkuhusumaadhimishoyaSikuyaVijanaDunianinamwandishiwahabarikutokaRedioyaTaifa TBC TaifaBibi. Betty Tesha. Maadhimishohayokitaifayanaadhimishwatarehe 12 Agostijijini Dar es Salaam.
Na: Frank Shija, WHVUM

VijanawatakiwakujitokezakatikamaadhimishoyaSikuyaVijanaDunianiambayokitaifayatafanyikatarehe 12 Agostijijini Dar es Salaam hukukaulimbiuyamwakahuuikiwani “UshirikiwaVijanakatikamasualayaKiraia
WitohuoumetolewanaKatibuMkuuwaWizarayaHabari, Vijana, UtamaduninaMichezoBibi. SihabaNkingaalipokuwaakizungumzanawaandishiwahabarijanajijini Dar es Salaam.
BibiSihabaamesemakuwamaadhimishohayoyamekuwayakifanyikakilamwakaikiwanikutambuamchangowaVijanakatikakuletamaendeleoyataifanajamiikwaujumlakwakuwandiyokundikubwa la nguvukaziyenyekuletachachuyamaendeleokupitiaubunifu.
“NatoawitokwavijanawotenchinikushirikikatikakuadhimishaSikuhiimuhimukwakujihusishanashughulimbalimbalizakijamiikatikamaeneoyao, kwa wale wa Dar es Salaam nivyemawakajitokezanakushirikimaadhimishiohayoambayokitaifayanafanyikamkoanihapa” AlisemaSihaba.
AidhaKatibuMkuuhuyoaliongezakuwayatafikiakilelesikuyaJumatanoyatarehe 12 AgostiyatatanguliwanaKongamanolitakalofanyikamnamotarehe 10 mwezihuukatikaukumbiwaKarimjeenakushirikishazaidiyaVijana 150 watakaojadilianamadambalimbaliikiwemoushirikiwavijanakatikaUchaguziMkuuwamwaka 2015.
Aliongezakuwasambambanamaadhimishohayosikuyakilelekutakuwavijanawatapatafursayakutoanakupataburudanimbalimbalikupitiamatamashanamichezo, piasikunhiyoitatumikakwavijanakuonyeshakazizaozikiwemozaubunifu.
KatikakuhakikishamaadhimishohayoyanafanyikiwaSerikaliimekuwaikishirikiananawadaumbalimbalikatikamikakatinauendelezajiwaVijananchiniamjbapobaadhiyawadauhaonipamojanaShirika la UmojawaMataifalinaloshughulikiaIdadiyaWatuDuniani (UNFPA), AMREF,ILO, PSI, IYF, Restless Development nawadauwoteambaokwanamnamojaamanyinginewamekuwawakijihusishanavijana.
SikuyaKimataifayaVijanailianzatangumwaka 1991 nchini Australia ikiwanalengo la jumuiyayaKimataifanajamiikwaujumlakupatafursayakusherehekeanakutambuanafasiyaVijanakatikakuletamaendeleoyakiuchuminakijamiikatikanchizao, namwaka 1998 ilikubaliwanajopoMawaziriwanaoshughulikiaVijananahatimayeUmojawaMataifauliridhiarasmikuitambuasikuhiyokuwayamaadhimishoKimataifaambapomwaka 2000 nchiwanachamawaBaraza la UmojawaMataifaikiwemo Tanzania walianzakuadhimshasikuhiyomuhimu.


MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA UZINDUZI WA MFEREJI MPYA WA SUEZ

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Balozi wa Tanzania, nchini Misri, Balozi Mohammed Hamza, wakati wakitoka kwenye Boti baada ya kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Mfereji mpya wa Suez Canal, kwa ajili ya meli za mizigo. Hafla hiyo ilifanyika jana Agosti 6, 2015 jijini Ismailia. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana ameiwakilisha Tanzania katika uzinduzi wa mfereji mpya wa Suez unaounganisha mabara ya Ulaya, Afrika na Asia. Mfereji huu mpya ambao Misri inauita "zawadi mpya kwa Dunia" unalenga kukuza uchumi katika usafiri wa maji na utarahisisha usafirishaji wa mizigo kwa mabara haya matatu, huku Misri ambayo kijiografia iko jangwani ikitegemea kukuza uchumi wake kutokana na meli zitakazopita katika mfereji huo.
Mradi wa ujenzi wa Mfereji huu mpya umejengwa kwa mwaka mmoja licha ya kupangwa kukamilika baada ya miaka mitatu na umetumia kiasi cha dola za Marekani Bilioni Nane ambazo zimechangwa kwa njia ya Hisa na wananchi wa Misri kwa kipindi kisichozidi siku tisa. Mfereji huu ambao umezinduliwa jana, unatoa fursa kwa Meli kupita bila usumbufu tofauti na zamani ambapo ilipaswa Meli kusimama ili kupishana lakini sasa kila upande wa Meli utapita bila kuathiri upande mwingine.
Sherehe hizo za aina yake zimehudhuriwa na viongozi kadhaa wa nchi mbalimbali na kupata kuripotiwa na vyombo vyote vikubwa duniani na hivyo kutoa picha ya kuwa Afrika inapiga hatua katika kukuza uchumi wake pamoja na kuonesha dunia kuwa fursa mpya za maendeleo zipo Afrika.
Sherehe hizo za  aina yake zilipambwa na maonesho ya ndege za kivita zilizotanda anga la Mfereji mpya wa Suez huku zingine zikiruka kwa kasi na kutoa moshi ulioakisi bendera ya Misri, zingine zikipeperusha bendera ya nchi hiyo.
Katika tukio hilo la kuathimisha tukio hilo la kihistoria   serikali ya Misri ilitangaza kuwa  siku hiyo ni ya mapumziko huku ulinzi mkali ukiimarishwa katika miji yote mikuu ya nchi hiyo huku jiji la Cairo walipofikia  viongozi mbalimbali wa kimataifa likiwa chini ya uangalizi wa kijeshi kwenye maoneo yote muhimu. Barabara ya kwenda eneo la Islamelia zilikofanyika sherehe hizo ilifungwa kwa siku nzima,  walioruhusiwa kupita  ni viongiozi na wageni mbalimbali  waalikwa waliotakiwa kuhudhuria tukio hilo la kihistoria.
 Rais wa Misri Abdel  Fatah  Sisi alisema kufunguliwa kwa Mfereji  ni uthibitisho kwamba Misri inaweza na kueleza kwamba njia hiyo itaimarisha zaidi shughuli za usafirisha na kufungua fursa zaidi kwa mataifa  duniani.
Katika moja ya matukio ya  uzinduzi huo Rais Fatah na viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo walisafiri katika meli za kifahari huku kiongozi huyo wa Misri akivalia mavazi maalumu ya kijeshi akiwa juu ya sehemu ya uwazi wa meli hiyo pamoja na kijana mdogo mwanafunzi wa miaka tisa aliyevalia kijeshi na kupeperusha bendera ya  Misri kama ishara ya kufunguliwa rasmi kwa mfereji huo.
Shughuli  ilimazika usiku  kwa  maonesho mbalimbali ya sanaa na utamaduni wa Misri  na kuhudhuriwa na viongozi na wageni wote waalikwa.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene, afanya ziara Bupigu na Bundali

 akisalimia watu wa Bundali
 akisalimiaana na watu wa Bupigu

 akipiokea ungo kutoka kwa watu wa kutengeza ungo Isoko
 Mmoja wa Friends of Mbene akizungumza na watu wa Bupigu
akisalimiana na wanawake wa Bupigu

Janet Mbene atoa Shukrani kwa Watu wa MMbebe

 Janet Mbene akiingia Mmbebe
 Janet Mbene akiongea na watu wa Mmbebe
 Janet Mbene akiongea na watu wa Mmbebe

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...